Luqman Van Maliki
Member
- Aug 19, 2021
- 6
- 7
.
Uzalendo ni msamiati au neno gumu sana kwa baadhi ya watanzania hasa ukitazama na kukumbuka jinsi mambo mengi yanavyokwenda na kuchukuliwa nchini.
Mapema wiki hii tarehe 3 ya mwezi Septemba bondia wa ngumi za kulipwa nchini Hassan Mwakinyo alikuwa anapigana na bondia kutoka Namibia Julius Munyelele Indongo wakipigania taji la masumbwi. Hassan Mwakinyo alishinda kwa KO raundi ya nne, watanzania wengi walisonya na kubeza ushindi ule.
Kabla hata ya pambano na wakati wa pambano lenyewe maeneo mengi hasa ya vibanda vya kuonesha mipira vilivyoonesha pambano lile watu wengi walikuwa wakitaka na kutamani Mwakinyo apigwe. Sababu? Wengi kati yao walikuwa ni mashabiki wa bondia Twaha Kiduku kutoka Morogoro.
Twaha Kiduku ni bondia anayekuja juu katika ngumi za kulipwa nchini, mashabiki wengi wa masumbwi wanalitaka sana pambano la kati ya Mwakinyo na Twaha Kiduku ili kukata kiu na shauku ya kujua nani bora zaidi kwa sasa nchini kwa upande wa tasnia ya ngumi. Tatizo ni moja tu Hassan Mwakinyo hataki kupigana pambano hilo ambalo kwake analiita la kuwaridhisha watu.
Mara nyingi Mwakinyo amesikika na kukariwa na waandishi wa habari wakati wa mahojiano yake mbalimbali anayoyafanya na waandishi akisema hawezi kupigana na bondia ambaye sio hadhi yake katika mizani ya ngumi huku akiongeza kuwa kwake ngumi ni ajira hawezi kumridhisha mtu bila ya yeye kupata maslahi.
Baada ya kauli zake hizo zenye kuchukiza kwa baadhi ndipo mashabiki wengi wa masumbwi nchini wakaanza kumbeza na kumuombea apoteze mbele ya Mnamibia. Huku ni kukosa uzalendo kulikopita kiasi.
Wakati ule bondia kutoka mkoani Morogoro Francis Cheka akiwa katika ubora wake mwaka 2012 alipigana na bondia kutoka nchini Marekani, katika pambano lile Cheka alishinda ila watanzania wengi walinuna hawakutaka Francis Cheka ashinde, baadhi walisema Cheka amempiga kinyozi tu kutoka Marekani. Kisa yule bondia alikuwa anamiliki saluni. Watanzania walisahau kama Cheka akiwa nje ya ulingo anaokota makopo na kuyauza, kama angepigwa pengine wangesema mmarekani amempiga muokota makopo. Ndivyo tulivyo hatujipendi.
Kwa wenzetu uzalendo ni kama pete na kidole. Wenzetu wanajipenda, wanapendana na wanajikubali. Sisi jambo hilo ni gumu kama kupata maziwa ya kuku. Wakati wa pambano la ngumi kati ya Floyd Mayweather na mfilipino Pacquiao wakati ule, wamarekani kibao walijaa kwenye ukumbi wa MGM arena kumshangilia Mayweather.
Walikuwepo nyota kibao wa muziki wa Marekani kama Kanye West, Lily Wayne na wengineo kibao, pale kwao ilikuwa Marekani kwanza, sisi huku Mwakinyo akishinda dhidi ya mpinzani kutoka nje tunachukia. Hatuna uzalendo na haijulikani uzalendo umekwenda wapi.
Ukijaribu kuchungua mambo kwa karibu utaona kwa bara zima la Afrika siyo tu kwa Tanzania neno uzalendo sio kitu muhimu na cha kushtua mioyo yetu tofauti na wazungu.
Majuzi hapa nyota wa Morocco anayekipiga kwenye klabu ya Chelsea ya Uingereza Hakim Ziyech aliondolewa kwenye kambi ya timu ya taifa na mwalimu wao Herve Renard kwa kuongopea anaumwa kisa hataki kucheza timu ya taifa.
Kwa Afrika tumeshuhudia nyota wengi wanaocheza Ulaya kama kina Prince Boateng mara kadhaa wakigomea kucheza timu zao za taifa wakati kwa wazungu wanatamani sana kuyawakilisha mataifa yao.
Matatizo mengi ya Tanzania na Afrika nzima yanasababishwa na ukosefu wa uzalendo wa kweli. Nchi nyingi viongozi wengi wazawa wanashirikiana na wageni kutorosha mali za umma na kuwaacha wananchi wakiteseka na maisha magumu.
Kwa watanzania mambo kama hayo ni kawaida, hata katika soka tumeiona Simba ilicheza mechi za kimataifa nyingi hadi baadhi ya timu zimepata nafasi kushiriki kimataifa baada Simba kufanya vizuri na kuiwakilisha nchi vema, lakini wakati Simba ikikomboa timu nyingine bado mashabiki wa timu hizo wameendeelea kuibeza na kuipuuza. Kukosa shukrani na uzalendo. Kwenye ngumi napo mambo ni vile vile tu hakuanza kupingwa Mwakinyo hivi majuzi mambo haya yalianza zamani hizo. Muda mrefu watanzania kwao neno uzalendo lilibaki kama neno linalotamkwa mdomoni pekee na sio kwa vitendo.
Katika soka mashabiki wengi wa Simba wanamuona Simon Msuva kama bado anacheza Yanga hata akiwa timu ya taifa, Msuva akifunga watu wanachukia ni kama ilivyo mashabiki wa Yanga wanavyomchukulia Mbwana Samata kama mchezaji aliyetokea Simba licha ya sasa akicheza soka Ulaya. Watanzania tunapenda kujichukia na tunachukia kujipenda, tunajidharau na hatuna uzalendo.
Hata watu wenye maisha ya kimaskini neno uzalendo kwao ni kitu kigeni cha kawaida. Vijana wengi utawakuta kwenye mifuko yao ya suruali wakiwa na vitambaa vya kufuta jasho vikiwa na bendera ya Jamaica au Marekani. Huku ni kukosa uzalendo kwanini wasiwe na vitambaa vya bendera ya Tanzania?.
Sina hakika kama kuna nchi duniani inafundisha somo la uzalendo bali ni kujipenda kwao na kujithamini. Waingereza kuna nyakati wanakasirisha dunia. Wanajipenda kupitiliza, wana uzalendo uliopita kipimo cha uzalendo wa kawaida. Wenyewe wanaamini hakuna jiji zuri duniani kama London. Unapata wapi ujasiri wa kusema London ni bora kuizidi miji kama Tokyo au Beijing na Rio de Jeneiro? Huu ni uzalendo uliokithiri lakini kwa Tanzania huwezi kukuta kitu kama hicho.
Pengine watanzania kuna mahala tulikosea tangu zamani tujifunze kuwa wazalendo tuthamini vya kwetu. Rais Samia Suluhu Hassan kwa sasa anajitahidi kuandaa filamu ya kuitangaza Tanzania ili kuiambia dunia madini ya Tanzanite yanapatikana nchini pekee. Huku ni kuchelewa na kukosa uzalendo kwa wengi wetu kushindwa kuitangaza Tanzania.
Tumeshindwa kujitangaza kwa kukosa uzalendo.
Mbunge wa Kawe mchungaji Josephat Gwajima alisema nyakati fulani alidhuru nchi ya Japan lakini ajabu ni kwamba wakazi wengi wa nchi ile wanafahamu Mlima Kilimanjaro upo Kenya.
Haya ni matusi makubwa kwa watanzania. Tubadilike, tujithamini, tujipende na tuwe wazalendo.

Upvote
1