Watanzania waendekeza dezo "Tumaini Revolving Fund"

NgomaNzito

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2008
Posts
559
Reaction score
28
Baada ya DECI kusitisha huduma zake check hii

Mwananchi jana lilifika katika taasisi ya Tumaini Revolving Fund (TRFI) iliyo Tabata jijini Dar es Saam na kushuhudia wakazi mbalimbali wakiomba kupewa maelezo ya jinsi ya kujiunga na taasisi hiyo huku wengine wakivuna fedha zao.

Kwa mujibu wa masharti ya taasisi hiyo mshiriki anayetaka kujiunga anatakiwa kuweka fedha kwenye akaunti iliyo benki ya Dar es Salaam Community (DCB).

“Mimi ndio nimekuja kujiunga nataka kupata maelekezo tu maana huko Deci hata hakufai. Serikali imewavalia njuga viongozi wetu mpaka wamesitisha huduma,” alisema mmoja wa watu aliyekuwa kwenye ofisi hizo.

“Lakini walichokifanya wala sio suluhisho kwani tutazidi kupanda na kuvuna. Hapa nimesikia mpaka mikopo wanatoa tena kwenye vikundi... unaona sasa Mungu anatupenda; inakufa Deci, tunaibukia sehemu nyingine,” alisema mtu mwingine aliyefika katika taasisi ya TRFI.

Mmoja wa wafanyakazi waliokuwa wakielekeza watu jinsi ya kujiunga na taasisi hiyo, akiwatahadharisha kutoihusisha taasisi hiyo ya
TRFI na Deci kwa madai kuwa ni vitu viwili tofauti.

“Hii ni tofauti sana na Deci naomba msiifananishe kabisa. Masharti yetu ni kwamba kila mwanachama anayetaka mkopo anatakiwa kuwa katika kikundi cha watu watano hadi 50. Tunawahimiza wanachama wapya kufika ofisini na kupewa maelekezo kabla ya kuweka fedha kwenye akaunti ya DCB,” alisema akielekeza wanachama hao watarajiwa.

"Kwa awamu ya kwanza hadi ya tatu, mwanachama atachukua wezesho tu, lakini awamu ya nne mwanachama atachukua mbegu yake na ongezeko la asilimia 15 tu, baada ya kumaliza awamu ya nne ya mzunguko wa kwanza mwanachama anaweza kuanza mzunguko mwingine kwa kiingilio pungufu cha asilimia 20.

"Mwanachama anayejiunga atalipa kiingilio kutegemeana na kianzio anachotaka kuweka."

Kwa mujibu wa masharti ya taasisi hiyo ya mikopo midogo iliyosajiliwa kwa ajili ya kusaidia wale wenye kipato kidogo kama ilivyo Deci kianzio chake ni Sh10,000 na kiingilio kinaanzia Sh5,000. Wezesho linaanzia Sh4,400 kwa miezi miwili na Sh6,600 kwa miezi mitatu.

Mmoja wa wanachama waliofika katika kituo hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa yeye alianza kuweka fedha katika taasisi hiyo siku nyingi na kufafanua kuwa, mpaka hivi sasa ameshafaidika vya kutosha, hivyo hata ikifungwa hatakuwa na hasara kama wale wanaojiunga hivi sasa.

Mwananchi mwingine alisema amewekeza fedha zake Deci, TRFI na taasisi nyingine aliyoitaja kwa jina la Malingumu Investment aliyodai ipo maeneo ya Kitunda Jijini Dar es Salaam.

“Mimi hapa nimeanza kuja baada ya kuanza kuona Deci mambo hayaendi vizuri, kule Malingumu nimeanza kama miezi miwili iliyopita, na kule tunavuna bwana sio kama hapa,” alisema mwananchi huyo akionyesha baadhi ya fomu za Malingumu.
Fomu hizo zinaonyesha kuwa mwanachama anaanza kupanda Sh 20,000 hadi 1,000,000 na kuvuna fedha mara moja na nusu ya fedha aliyoipanda katika kipindi cha wiki nne mpaka 12.

My take
Watanzania hatupendi kusoma na kufanya kazi kwa bidii ili tupate mafanikio ndioo maaana sie kila siku maskini tutaendelea kuibiwa tuu
 
Pia sababu kubwa ya wananchi kukimbilia kwenye taasisi hizi za upatu ni kutokana kutokuwepo na sera madhubuti katika serikali hii ya CCM za kuwainua wananchi wake check Bilioni za kikwete zilipokwenda hakuna mwananchi hata mmoja anayeweza kutoa ushuhuda bilioni zile zilimwinuaje nadhani ni wakati muafaka tunapoelekea uchaguzi tuone ni jinsi gani kuwaondoa viongozi wasio na vision ya kuwakomboa watanzania na hali hii
 
Haya jamani.
Ila ukweli unabaki pale pale. Siku moja kuna watakolia. wengi wanasema ujanja ni kuwahi. na nadhani walio wengi wanatumia kauli mbiu hii kwamba kila mmoja anataka awe wakwanza ili wachelewaji waliwe.

Ila tutumie utu jamani huu ni wizi mkumbwa uliofichika. Mtu ukijua dhahiri kuwa hawa kina deci na wengineo hawana shunguli ya uzalishaji isipokuwa kurevolve funds na unakubali kujiunga, hii inamaanisha ni kuwa tiyari kuwaibia wachelewaji watakaokuwa na matumaini kama nao watavuna.

Mi nadhani upatu mzuri ni ule wa kupanda na kuvuna ulichopanda. La sivyo watu wajiunge pamoja wapande mfululizo bila kuvuna kwa malengo ya kukuza mtaji. Kisha fedha zikitimia mtaji watengeneze management yao na sheria za kujiendesha waanzishe mradi ambao utawapa faida ya walichokipanda.

La sivyo hatari kubwa sana. Nimeshuhudia wamasai morogoro wakiuza ngombe wao na kupanda deci mnyororo wa milioni tatu na hii ilikua January 2009. Nina uhakika kama kavuna kutoka kwenye hiyo milioni tatu kavuna mara moja ama mbili. Na walikua morani kibao wanashuka mahesabu ya kulikimbia pori kwa madai deci itawawezesha kupata faida sawa na kuuza ngombe wawili kila wiki kitu ambacho hawajawahi kuota maishani mwao.

Sasa deci Kaputi, Ngombe Hawana, Sijui Hali zao kwa sasa zitakuaje.

Ila jamani tuache wizi.
 
Baada ya DECI kusitisha huduma zake check hii

Mwananchi jana lilifika katika taasisi ya Tumaini Revolving Fund (TRFI) iliyo Tabata jijini Dar es Saam na kushuhudia wakazi mbalimbali wakiomba kupewa maelezo ya jinsi ya kujiunga na taasisi hiyo huku wengine wakivuna fedha zao.

Kwa mujibu wa masharti ya taasisi hiyo mshiriki anayetaka kujiunga anatakiwa kuweka fedha kwenye akaunti iliyo benki ya Dar es Salaam Community (DCB).

“Mimi ndio nimekuja kujiunga nataka kupata maelekezo tu maana huko Deci hata hakufai. Serikali imewavalia njuga viongozi wetu mpaka wamesitisha huduma,” alisema mmoja wa watu aliyekuwa kwenye ofisi hizo.

“Lakini walichokifanya wala sio suluhisho kwani tutazidi kupanda na kuvuna. Hapa nimesikia mpaka mikopo wanatoa tena kwenye vikundi... unaona sasa Mungu anatupenda; inakufa Deci, tunaibukia sehemu nyingine,” alisema mtu mwingine aliyefika katika taasisi ya TRFI.

Mmoja wa wafanyakazi waliokuwa wakielekeza watu jinsi ya kujiunga na taasisi hiyo, akiwatahadharisha kutoihusisha taasisi hiyo ya
TRFI na Deci kwa madai kuwa ni vitu viwili tofauti.

“Hii ni tofauti sana na Deci naomba msiifananishe kabisa. Masharti yetu ni kwamba kila mwanachama anayetaka mkopo anatakiwa kuwa katika kikundi cha watu watano hadi 50. Tunawahimiza wanachama wapya kufika ofisini na kupewa maelekezo kabla ya kuweka fedha kwenye akaunti ya DCB,” alisema akielekeza wanachama hao watarajiwa.

"Kwa awamu ya kwanza hadi ya tatu, mwanachama atachukua wezesho tu, lakini awamu ya nne mwanachama atachukua mbegu yake na ongezeko la asilimia 15 tu, baada ya kumaliza awamu ya nne ya mzunguko wa kwanza mwanachama anaweza kuanza mzunguko mwingine kwa kiingilio pungufu cha asilimia 20.

"Mwanachama anayejiunga atalipa kiingilio kutegemeana na kianzio anachotaka kuweka."

Kwa mujibu wa masharti ya taasisi hiyo ya mikopo midogo iliyosajiliwa kwa ajili ya kusaidia wale wenye kipato kidogo kama ilivyo Deci kianzio chake ni Sh10,000 na kiingilio kinaanzia Sh5,000. Wezesho linaanzia Sh4,400 kwa miezi miwili na Sh6,600 kwa miezi mitatu.

Mmoja wa wanachama waliofika katika kituo hicho ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa yeye alianza kuweka fedha katika taasisi hiyo siku nyingi na kufafanua kuwa, mpaka hivi sasa ameshafaidika vya kutosha, hivyo hata ikifungwa hatakuwa na hasara kama wale wanaojiunga hivi sasa.

Mwananchi mwingine alisema amewekeza fedha zake Deci, TRFI na taasisi nyingine aliyoitaja kwa jina la Malingumu Investment aliyodai ipo maeneo ya Kitunda Jijini Dar es Salaam.

“Mimi hapa nimeanza kuja baada ya kuanza kuona Deci mambo hayaendi vizuri, kule Malingumu nimeanza kama miezi miwili iliyopita, na kule tunavuna bwana sio kama hapa,” alisema mwananchi huyo akionyesha baadhi ya fomu za Malingumu.
Fomu hizo zinaonyesha kuwa mwanachama anaanza kupanda Sh 20,000 hadi 1,000,000 na kuvuna fedha mara moja na nusu ya fedha aliyoipanda katika kipindi cha wiki nne mpaka 12.

My take
Watanzania hatupendi kusoma na kufanya kazi kwa bidii ili tupate mafanikio ndioo maaana sie kila siku maskini tutaendelea kuibiwa tuu

Sisi sijui tumelogwa, yani tuna mawazo ya kimasikini sana. Tunafikiria kupanda na kuvuna. Itatuchukua muda mrefu sana kupata maendeleo kama tutabaki na mawazo ya kupenda bure bure namna hii.
 
Pia sababu kubwa ya wananchi kukimbilia kwenye taasisi hizi za upatu ni kutokana kutokuwepo na sera madhubuti katika serikali hii ya CCM za kuwainua wananchi wake check Bilioni za kikwete zilipokwenda hakuna mwananchi hata mmoja anayeweza kutoa ushuhuda bilioni zile zilimwinuaje nadhani ni wakati muafaka tunapoelekea uchaguzi tuone ni jinsi gani kuwaondoa viongozi wasio na vision ya kuwakomboa watanzania na hali hii
ukiwa raisi kilaza ndio taabu hii.....
 
Back
Top Bottom