Mchimwachimego
JF-Expert Member
- Jun 15, 2020
- 358
- 271
Nakumbuka katika kampeni za 2015 na kurudi nyuma hoja kubwa za upinzani ilikuwa ni ufisadi na ubadhilifu wa mali za umma, alipoingia Rais John Joseph Magufuli amefanya mengi kuakikisha anayafuta kabisa, ametumia nguvu nyingi kuyaondoa lakini kwa kipindi hicho pesa ilikuwa nyingi sana lakini Watanzania hawakujua kuwa uwepo pesa nyingi mtaani kulisababishwa na huo ufisadi, wizi wa rasilimali, madawa ya kulevya, rushwa, mauaji ya tempo,mauaji ya albino, utoroshwaji wa madini,watumishi kutowajibika, wafanyakazi hewa, vyeti bandia,
magendo, uvuvi haramu, utakatishaji pesa haramu nk.
Wakati watu wamechoka haya mambo katika serikali na jamii hawakufanya tasmini kuwa sisi watanzania uchumi wetu haukua halisi kwa maana ya pesa halali kwa Malipo ulikuwa uchumi wa pesa haramu kila kitu kilikuwa dili, kuanzia bandarini,serikalini,tenda,hospitali na kila mahali. Sasa alipoingia Magufuli amesafisha na kuanza upya kwa maana kujitasmini kujaribu kudhibiti watu walewale wanalia kuwa uchumi mgumu tulieni jamani "no pain no gain" ili ufanikiwe lazima ujibane.