Watanzania waliopo Afghanistan

Watanzania waliopo Afghanistan

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
10,589
Reaction score
35,268
Wiki hii tumeshuhudia rabsha za hapa na pale nchini Afghanistan, jeshi la serikali ya Afghanistan limeshindwa kuwakabili wahuni wa Taleban wasiojua kukata tamaa au kushindwa, wanajeshi karbia wote wa Afghanistan walikimbia na Raisi wao pia akachochora.

Na kuna news za kimya kimya zinadai Makamanda wa Jeshi la Afghanistan wali-colaborate na wajuba, ili Marekani asepe maana ametengeneza makundi mawili yenye uadui na hvyo kuwaachia msala wa vita ya wenyewe kwa wenyewe

Vifaa vya kijeshi ambavyo jeshi la Afghanistan lilikabidhiwa na Marekani pamoja na nchi zingine vyote sasa hivi vinamilikiwa na Wataleban.

Sa hivi kila nchi inapambana kuondoka raia wake Afghanstani, huku wataleban inasemekana wameanza kufunga njia zote za kutokea hata njia ya kuelekea airport sa hv ipo kwenye great danger , vip raia wenzetu wa kibongo waliopo kule , washaridhika na life linaloendelea au mamlaka ndo zipo busy na Tozo.

000_9LE6N6-1-e1629532786251-640x400.jpg

Watalebani wakiwa wanaswali sku ya ijumaa
 
Wiki hii tumeshuhudia rabsha za hapa na pale nchini Afghanistan , jeshi la serikali ya Afghanistan limeshindwa kuwakabili wahuni wa Taleban wasiojua kukata tamaa au kushindwa , wanajeshi karbia wote wa Afghanistan walikimbia na Raisi wao pia akachochora...
Hakuna Mtanzania hata mmoja huko. Na kama alienda huko bas alienda kisiri ili kujifunza Ugaidi. Kwani miaka yote nchi hiyo ilikuwa kwenye vita. Je yeye alifurahishwa nini kwenda nchi ya hatari kama hiyo?
 
Nitahamia talebani mimi nikaishi huko
 
Hakuna Mtanzania hata mmoja huko. Na kama alienda huko bas alienda kisiri ili kujifunza Ugaidi. Kwani miaka yote nchi hiyo ilikuwa kwenye vita. Je yeye alifurahishwa nini kwenda nchi ya hatari kama hiyo?
Akili za Vijana wa kijani hizi, watu walikuwa wanazamia mpk kwa mungiki unadhani maisha Ni bongo tu
 
Ukiona mtanzania ameenda huko ni wale wanajificha kwenye dini kumbe wameajiriwa kujiunga na makundi ya kigaidi
 
Hivi Pale Afgan kuna nn kingine pengine kuna kitu cha mhimu zaidi hatukijui...Mimi siamini mmarekani azamie tu pale pasi na sababu...
 
Bora waishi huko maana bongo ni tozo juu ya tozo
 
Hivi Pale Afgan kuna nn kingine pengine kuna kitu cha mhimu zaidi hatukijui...Mimi siamini mmarekani azamie tu pale pasi na sababu...
Kutokana na Taliban kusupport Al-Qaeda, Marekani walivamia Afghanistan mwisho wa mwaka 2001. Lengo lao lilikua kuwafurusha Taliban nje ya Afghanistan na kutengeneza serikali mpya baada ya ile ya zamani kutwaliwa na Taliban.
 
Na imewashinda 😀 , urusi walilost Zaid ya askar 15000 , aisee hawa jamaa ni amsha, sema mmarekani mbishi atawatengenezea kikundi kingine cha kuwa-harras wataleban...!!only kama ataona bado kuna benefit Afghanistan
 
Ukizingatia muda Marekani imetumia kuisambaratisha Taliban, pesa zilizotumika na wanajeshi waliofariki halafu ulinganishe na speed Taliban waliochukua kuirejesha Afghanistan mikononi mwao ni kituko na aibu kwa Marekani.
 
Si bure mkuu, there is something behind, time will tell.
 
Ukizingatia muda Marekani imetumia kuisambaratisha Taliban, pesa zilizotumika na wanajeshi waliofariki halafu ulinganishe na speed Taliban waliochukua kuirejesha Afghanistan mikononi mwao ni kituko na aibu kwa Marekani.
Kwa vyovyote vile kuna unafki amefanyiwa
 
Back
Top Bottom