Watanzania wanataka Katiba Mpya!

Watanzania wanataka Katiba Mpya!

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,252
Reaction score
8,003
Ukweli ni kwamba kuna watu au kundi la watu halitaki kusikia kabisa hii kitu, Lakini kuna mwamko Mkubwa sana na spirit iliyowajaa watanzania katika haji ya juu kutaka kupata katiba mpya itakayowakomboa wao pamoja na vizazi vyao.

Kwa hali inavyoonekana ni kwamba ndio watanzania kwa sasa wanaona ni mzigo pekee ulioko mbele yao, mzigo huu wanaona kua ni mzito sana kuliko wanavyofikiria. Kibaya zaidi ni pale ambapo kundi moja la watu halitataka kusikia kitu kama hicho lakini wananchi walio watahitaji.

Watanzania wameshagundua kua matatizo ya taifa lao yanasababishwa na kukosekana kwa katiba mpya na bora, hivi sasa katiba inaenda kua habari ya mjini.

NB: kama wengi wanahitaji katiba, wachache hawahitaji katiba, basi wale wachache ndio kikundi cha watu.
 
Pendekezwa au ya Warioba au mpya kabisa? Ni ipi wanataka?
 
Wapinzani hawajui nini wanataka.Wengine katiba mpya,wengine tume huru,bahati mbaya yote hayo si kipaumbele kwa sasa.Fanyeni kazi
 
Watanzania wengi mambo ya katiba mpya siyo priorities. Cha msingi hihi iliyopo tuifanyie amendment kwenye madaraka ya Rais hasa kwenye kuteua..Rais anateua watu wengi sana. Kingne tufanye amendment kwenye Tume ya uchaguzi hasa kwenye sheria ya Tume na uteuzi wake..
 
Wapinzani hawajui nini wanataka.Wengine katiba mpya,wengine tume huru,bahati mbaya yote hayo si kipaumbele kwa sasa.Fanyeni kazi
Si wapinzani tu ni swala la wananchi wote. Wewe uliyejikinga kwa watawala yakikukuta kwa sababu yoyote ile utatamani kuwa na Katiba nzuri e.g. Kingunge, Kolimba, Sumaye etc

Katiba nzuri ni afya kwa taifa itazaa na tume huru
 
Kama sio sitta sasa hivi tungekuwa na katiba nzuri kabisa ya warioba bila kumwaga damu, sasa sina hakika kama tutaipata bila kumwaga damu
 
Hii inaitwa HAMISHA GIA ANGANI....ili mradi tu NCHI ISITAWALIKE
 
Si wapinzani tu ni swala la wananchi wote. Wewe uliyejikinga kwa watawala yakikukuta kwa sababu yoyote ile utatamani kuwa na Katiba nzuri e.g. Kingunge, Kolimba, Sumaye etc

Katiba nzuri ni afya kwa taifa itazaa na tume huru
Wananchi wote na akina nani?wengine hawajui hata kama kuna katiba.Fanyeni kazi
 
ngosha apigwe presure mapema alete katiba. kabla hajanogewa na madaraka I'll itumike nguvu kidogo
 
Kwanza hata TUME HURU YA UCHAGUZI tu inatosha, huyo atakaye chaguliwe anaweza weka utaratibu wa katiba inayofaa.
 
Sasa nani wakwenda kusimamia katiba mpya wakati ukawa walisusa na mkuu amesema sio kipao mbele chake
 
Wapinzani hawajui nini wanataka.Wengine katiba mpya,wengine tume huru,bahati mbaya yote hayo si kipaumbele kwa sasa.Fanyeni kazi
Wewe ni wa kuimba mapambio na kushangilia. Huna kipaumbele hata siku moja. Ilani ya uchaguzi wa CCM 2015 yataka katiba mpya. Ungekuwa mkweli na kumwambia ukweli Mkullu, ungekuwa mpenzi wa Mungu. Sasa hivi ni wa bk7 man.
 
Katiba mpya ianzie kwenye vyama vyenu kwanza.Acha tunyooshe nchi
 
Back
Top Bottom