Watanzania wanataka nini?

Watanzania wanataka nini?

Mkwanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,293
Reaction score
5,163
Watanzania wanataka barabara nzuri za juu na chini, wanataka reli ya kisasa, wanataka huduma bora za afya na elimu bure, wanataka mbolea na mafuta kwa bei nafuu, hapo bado wanataka na ajira zenye mishahara minono na wale walioajiriwa na serikali wanataka nyongeza mara dufu, lakini hawataki kulipa kodi wachangie.

Cha kushangaza pia hawataki serikali yao ikope kwa ‘mabeberu’, hawataki pia tupewe misaada, ukiamua kuwekeza kwenye rasilimali zetu kwa makampuni makubwa yenye mitaji ili upate kodi bado pia wanalalamika wanaibiwa rasilimali zao.

Wanataka tax base ile ile iendelee kuhenyeka kuwapa yote haya, hata kodi kama withholding tax on rent ambazo zilikuwepo miaka nenda rudi bado watu waliopangisha majumba hawataki kulipa wanataka walipe walewale wa siku zote alafu wenyewe waendelee kufaidi.

Je, Watanzania wanataka nini? Very confusing nation!
 
Watanzania tunataka pesa tu hakuna cha ziada tunahitaji pesa ajira na maisha mazuri
 
Ukitaka kukosana na mabwanyenye wa serikali wewe waambie wapunguze matumizi.

Wapunguze marupurupu au wajikate kodi.
 
Back
Top Bottom