Watanzania wanathamini wafu kuliko walio hai

Ila alivyomkamata Sabaya ndiyo alikuwa anafanya Vizuri,au siyo!?
Tulitegemea baada ya Sabaya angefuata Makonda, Ndugai, na wengine wengi ikiwa ni pamoja na m/kiti na mkurugenzi wa tume ya taifa ya uchaguzi n.k. Sasa badala ya kuwakamata wahalifu hao wa kitaifa na kimataifa anamkamata mtu anayewaelimisha watanzania kuhusu umuhimu wa katiba mpya! Inahuzunisha!
 
Nina mashaka na elimu yako, hayo yote uliyoyaorodhesha, mtu mweusi ameshiriki katika uundaji, uvumbuzi na mambo yote walivyo fanya wazungu na wengine. Ilivyo kwamba, siyo wazungu wote ni wavumbuzi wa technology, vile vile kuna weusi wengi waliovumbua vitu vingi! Na wanaendelea kuvumbua. Pia ujue kwamba kitu kikianza kufanya kazi - mfano redio, simu, treni au dawa (chanjo), ujue vinajumuisha vikorokoro vingi ambavyo kati ya hivyo unakuta gwiji wake alikuwa ni "mutu omunyaama" (mtu mweusi)! Samahani niliposema ninatia shaka elimu yako maana nilitegemea haya unayajua! Na wazungu wanajua Michango ya watu weusi katika maendeleo ya technologia duniani.
Uliyoyaandika siyo ya kweli na nakuomba uutafute ukweli kusudi ngozi yako iwe huru mwilini mwako. Usije ukafikia kufa ili hali unajichukia.
 
Unaetia mashaka juu ya elimu ni wewe ambae unaandika vitu bila ushahidi.Yaani unadai kuwa mtu mweusi ameshiriki pia bila kutaja kuwa ameshiriki wapi na lini.Hii ndiyo elimu yako unayoringia?

Ni katika uvumbuzi upi ambao mtu mweusi amelead?Nauliza ni katika uvumbuzi upi ambao mtu mweusi alishiriki kwa kuanzisha mapambano?Na kama yeye hutumika tu kama kisaidizi ni kwa nini?Yaani kwa nini yeye awe anatumika tu kama mtu alieshiriki na siyo mtu alieongoza mapambano?Wewe huoni kuwa hapa pana shida kama vile elimu yako ya kuandika vitu bila ushahidi ilivyo na shida?
 
Weusi wamevumbua vingi vya kusaidia kurahisisha maisha hapa duniani na wana patents (Hati miliki) za uvumbuzi huo. Ka-google utaona ni nyingi mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…