SoC04 Watanzania wanaweza kuwa wawekezaji wakubwa wa rasilimali asili ndani ya nchi yao

Tanzania Tuitakayo competition threads

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Na Constantine J. S. Mauki
June, 2024

Utangulizi
Miaka ya nyuma, kipindi cha serikali ya awamu ya kwanza, aliyekuwa rais, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema watanzani mmekalia uchumi. Baadhi ya watu walidhani alikuwa anafanya mzaha, lakini alimaanisha watu wamezungukwa na rasilimali nyingi kama ardhi, maji, misitu, madini na kadhalika lakini bado ni MASIKINI!

Historia Fupi Kuhusu Bara la Afrika
Tukirejelea historia yetu kwa ufupi, utakumbuka mwaka 1884 - 1885 kulifanyika mkutano mjini Berlin, nchini Ujerumani, maarufu kama 'Berlin Conference'. Ni mkutano uliojumuisha mataifa yaliyoendelea kiviwanda wakati huo, yakiwemo, Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno na Ujerumani (ambayo ni mwenyeji).

Huu ndio mkutano uliogawa bara la Afrika kwa mataifa yaliyotajwa hapo juu kama makoloni yao.

Nchi yetu, Tanganyika ilitawaliwa na Ujerumani, ingawa baadaye ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa ('United Nation Leage' wakati huo) baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, mwaka 1919.

Tukiendelea kurejea historia yetu, utambuka kwamba kabla ya ukoloni barani Afrika, kulikuwa na biashara kubwa ya utumwa, ambapo watu wetu walichukuliwa kikatili na Waarabu na kuuzwa Ulaya na Marekani kwenda kufanya kazi za uzalishaji, hasa mashambani.

Pia, kabla ya kugawa bara la Afrika, baadhi ya mataifa ya Ulaya, yalikuwa yanatuma watu maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kongo kufanya Upelelezi na kuchukuwa rasilimali mbalimbali hasa madini. Mpelelezi maarufu sana katika karne ya 15, ni Vasco Dagama kutoka taifa la Ureno.

Pamoja na ukweli kuwa karibu nchi zote barani Afrika ziliondokana na ukoloni miaka ya sitini, wakoloni hawa wanaendelea kuchota rasilimali za Afrika kupitia mifumo mbalimbali waliyoitengeneza. Hii ni pamoja kununua bidhaa au malighafi kutoka Afrika kwa bei ndogo wanazopanga wao, kuingia mikataba na watawala wa Afrika ya kuwawezesha kuchota rasilimali, inayowanufaisha zaidi wao, huku wananchi wakiendelea kubakia masikini.

Najaribu kukupitisha katika historia hii, ili kwa pamoja tufahamu kwanini nchi yetu ni masikini ilhali ina rasilimali nyingi sana.

Vita vya Rasilimali Asili
Vita vingi vinashuhudiwa katika nchi mbalimbali barani Afrika hasa katika maeneo yenye rasilimali nyingi kama madini na mafuta. Nigeria ni mzalishaji mkubwa barani Afrika wa mafuta ya petroli; kuna migogoro mingi kati ya wawekezaji na wenyeji katika maeneo ya uzalishaji. Mfano mwingine ni Congo DRC, ambapo kuna makundi mengi yanapigana na serikali katika maeneo ya mashariki ambapo kuna madini mengi mbalimbali. Makundi haya yanapigana huku yakipora madini.

Utajiuliza, makundi haya yanapata wapi silaha za kupigana na serikali kwa muda mrefu? Na pia, haya madini yanauzwa wapi? Majibu ni kwamba kuna makampuni makubwa kutoka mataifa makubwa yako nyuma ya mizozo hii; ili yapate madini, huku yakifanya biashara ya silaha. Na mataifa haya ni yale yaliyotawala bara hili huko nyuma. Kwa maneno mengine, kinachoendelea sasa ni UKOLONI MAMBOLEO!

Rasilimali Asili Tulizonazo Tanzania
Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi asili, ambazo zikitumiwa vizuri, umaskini utabaki kuwa historia. Zifuatazo ni baadhi ya rasilimali asili zilizopo nchini:

1. Bahari na maziwa: Tuna sehemu ya bahari ya Hindi iliyozunguka visiwa vya Zanzibar, na sehemu ya mashariki ya mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara. Pamoja na maziwa madogomadogo, tuna maziwa makubwa kuliko mengine barani Afrika, ambayo ni Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa. Hizi ni rasilimali zinazoweza kutumika kutengeneza uchumi wa Buluu.

2. Misitu: Karibu mikoa yote Tanzania ina misitu ambayo ni muhimu katika swala la utunzaji wa mazingira, nishati, ujenzi na utalii.

3. Milima: Tuna mlima Kilimanjaro na mlima Meru; mlima Kilimanjaro ni wa kwanza kwa urefu barani Afrika, na wa pili duniani. Hii ni muhimu kwa ajili ya utalii wa ndani na nje.

4. Mbuga za wanyama. Tuna mbuga nzuri na maarufu duniani, zikiwemo Manyara, Ngorongoro, Serengeti, Mikumi, Saadan, Gombe, na kadhalika

5. Madini na Vito: Tuna madini mengi kama dhahabu, chuma, urani, chumvi, mafuta, gesi asilia; na Vito kama Almas, Tanzanite, na kadhalika. Hivi vikitumika vyema vitainua uchumi wa nchi na wa MTU mmojammoja.

6. Ardhi Inayofaa kwa Kilimo: Kila wilaya, miongoni kwa wilaya zaidi 160 za Tanzania, zina ardhi ya kutosha inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na ya biashara.

7. Mito na Mabwawa: Vipo maeneo mengi nchini, ambavyo ni muhimu kwa ajili ya matumuzi ya nyumbani, viwandani, mashambani (kilimo cha umwagiliaji), uvuvi, utalii na kuendesha mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme.

Tanzania Tuitakayo 2025 -2050
Serikali kuu igatue mamlaka ya kumiliki rasilimali mbalimbali kwa serikali za mitaa na sekta binafsi. Kwa sasa serikali kuu ndio yenye mamlaka juu ya umiliki wa rasilimali nyingi hapa nchini, kama madini, gesi, na mbuga za wanyama. Na wawekezaji kutoka nje ya nchi humilikishwa rasilimali hizi wakati wenyeji wakihamishwa kutoka maeneo ya miradi na kupelekwa maeneo mengine bila kunufaika chochote na miradi husika.

Tunaweza Kubadilika
Mfano: Watu binafsi, asasi za kiraia au vijiji, vinaweza kuwezeshwa kuwa na hati miliki ya rasilimali asili kama ardhi yenye madini, gesi asilia, vitalu vya kuwindia wanyama pori, ardhi ya kilimo na kadhalika; ambavyo vitakuwa mtaji kwao kuweza kukaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza na hivyo kuwa wabia badala ya kuwa watazamaji. Serikali itakuwa mwezeshaji tu, kuhakikisha mikataba imekaa vizuri ili kila upande unapata stahiki zake katika miradi husika, na kuhakikisha mirabaha na kodi stahiki zinalipwa kikamilifu na kwa wakati.

Mageuzi yanahitaji maamuzi magumu!! Lakini faida ni nyingi sana; kila wilaya itakuwa na wawekezaji wazawa wengi, watakaotoa ajira kwa vijana wengi, wigo wa kodi utapanuka - jambo litakalofanya serikali kuacha kutegemea maeneo manyonge kupata kodi, na hivyo kumwondolea mwananchi tozo za moja kwa moja kama kodi ya ardhi, majengo, tozo za simu, na kadhalika. Mkakati huu, utachechemua uchumi wa mtu mmojammoja na wa taifa na hivyo serikali kupunguza utegemezi kutoka nje.

Vilevile, mageuzi haya yatapunguza, kama sii kumaliza kabisa migogoro kati ya wawekezaji na wenyeji, kama inavyoshuhudiwa mkoani Mara (Wawekezaji katika Mgodi wa dhahabu - Nyamongo na wenyeji). Na mwisho, mazingira ya rushwa yatapungua kwa kiasi kikubwa.

HITIMISHO
Ni vizuri kila mmoja ajue kuwa hatuwezi kutoka kwenye umasikini kwa kutegemea misaada na mikopo kutoka nje; tukubali kufanya MAAMUZI MAGUMU juu ya rasilimali tulizonazo, TUTATOKA hapa tulipo bila SHAKA!!

Rejea
Gazeti la Mwansnchi, Machi 17, 2021, Ukoloni Mamboleo na namna Viongozi Afrika Walivyonaswa.
www.trtafrika.com Ukoloni Afrika
 
Upvote 7
Kubadili fikra juu ya swala la uwekezaji inahitaji ujasiri wa kufanya maamuzi magumu. Dhana ya uwekezaji kwa wananchi wengi, na bahati mbaya hata kwa baadhi ya viongozi, ni kwamba wawekezaji ni watu kutoka nje, (tena WAZUNGU). Hii ni kasumba ambayo haitatusadia kututoa kwenye lindi la UMASIKINI!
 
Ukisoma makali hii na kuchangia, utakuwa umetoa mchango mkubwa sana katika uzungushaji wa gurudumu hili!!
 
Mwafrika hawezi kuwa na maendeleo kwa sababu maendeleo ni mfumo wa ulaya sio Africa
 
Viongozi wanapaswa kubadili fikra!! Mwekezaji namba moja ni Mtanzania, na wengine wanafuata.
 
Natamani Mradi wa daraja la Mlm Nyerere la Kigamboni, ungekuwa mfano katika utekelezaji wa miradi mingine, maana ulitekelezwa bila mkopo kutoka nje. Ingawa bado kulikuwa na uwezekano wa asilimia 40 za serikali, kubebwa na watu binasfsi na serikali ikabaki na jukumu la uratibu na uwezeshaji.
 
Mtanzania akiwekewa mazingira bora atakuwa mwekezaji bora, naye atakuwa na fursa ya kuwaalika wawekezaji kutoka nje ya nchi!!
 
Utangulizi
Miaka ya nyuma, kipindi cha serikali ya awamu ya kwanza, aliyekuwa rais, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema watanzani mmekalia uchumi. Baadhi ya watu walidhani alikuwa anafanya mzaha, lakini alimaanisha watu wamezungukwa na rasilimali nyingi kama ardhi, maji, misitu, madini na kadhalika lakini bado ni MASIKINI!

Historia Fupi Kuhusu Bara la Afrika
Tukirejelea historia yetu kwa ufupi, utakumbuka mwaka 1884 - 1885 kulifanyika mkutano mjini Berlin, nchini Ujerumani, maarufu kama 'Berlin Conference'. Ni mkutano uliojumuisha mataifa yaliyoendelea kiviwanda wakati huo, yakiwemo, Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno na Ujerumani (ambayo ni mwenyeji).

Huu ndio mkutano uliogawa bara la Afrika kwa mataifa yaliyotajwa hapo juu kama makoloni yao.

Nchi yetu, Tanganyika ilitawaliwa na Ujerumani, ingawa baadaye ilikuwa chini ya utawala wa Uingereza kwa udhamini wa Umoja wa Mataifa ('United Nation Leage' wakati huo) baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia, mwaka 1919.

Tukiendelea kurejea historia yetu, utambuka kwamba kabla ya ukoloni barani Afrika, kulikuwa na biashara kubwa ya utumwa, ambapo watu wetu walichukuliwa kikatili na Waarabu na kuuzwa Ulaya na Marekani kwenda kufanya kazi za uzalishaji, hasa mashambani.

Pia, kabla ya kugawa bara la Afrika, baadhi ya mataifa ya Ulaya, yalikuwa yanatuma watu maeneo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Kongo kufanya Upelelezi na kuchukuwa rasilimali mbalimbali hasa madini. Mpelelezi maarufu sana katika karne ya 15, ni Vasco Dagama kutoka taifa la Ureno.

Pamoja na ukweli kuwa karibu nchi zote barani Afrika ziliondokana na ukoloni miaka ya sitini, wakoloni hawa wanaendelea kuchota rasilimali za Afrika kupitia mifumo mbalimbali waliyoitengeneza. Hii ni pamoja kununua bidhaa au malighafi kutoka Afrika kwa bei ndogo wanazopanga wao, kuingia mikataba na watawala wa Afrika ya kuwawezesha kuchota rasilimali, inayowanufaisha zaidi wao, huku wananchi wakiendelea kubakia masikini.

Najaribu kukupitisha katika historia hii, ili kwa pamoja tufahamu kwanini nchi yetu ni masikini ilhali ina rasilimali nyingi sana.

Vita vya Rasilimali Asili
Vita vingi vinashuhudiwa katika nchi mbalimbali barani Afrika hasa katika maeneo yenye rasilimali nyingi kama madini na mafuta. Nigeria ni mzalishaji mkubwa barani Afrika wa mafuta ya petroli; kuna migogoro mingi kati ya wawekezaji na wenyeji katika maeneo ya uzalishaji. Mfano mwingine ni Congo DRC, ambapo kuna makundi mengi yanapigana na serikali katika maeneo ya mashariki ambapo kuna madini mengi mbalimbali. Makundi haya yanapigana huku yakipora madini.

Utajiuliza, makundi haya yanapata wapi silaha za kupigana na serikali kwa muda mrefu? Na pia, haya madini yanauzwa wapi? Majibu ni kwamba kuna makampuni makubwa kutoka mataifa makubwa yako nyuma ya mizozo hii; ili yapate madini, huku yakifanya biashara ya silaha. Na mataifa haya ni yale yaliyotawala bara hili huko nyuma. Kwa maneno mengine, kinachoendelea sasa ni UKOLONI MAMBOLEO!

Rasilimali Asili Tulizonazo Tanzania
Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi asili, ambazo zikitumiwa vizuri, umaskini utabaki kuwa historia. Zifuatazo ni baadhi ya rasilimali asili zilizopo nchini:

1. Bahari na maziwa: Tuna sehemu ya bahari ya Hindi iliyozunguka visiwa vya Zanzibar, na sehemu ya mashariki ya mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara. Pamoja na maziwa madogomadogo, tuna maziwa makubwa kuliko mengine barani Afrika, ambayo ni Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa. Hizi ni rasilimali zinazoweza kutumika kutengeneza uchumi wa Buluu.

2. Misitu: Karibu mikoa yote Tanzania ina misitu ambayo ni muhimu katika swala la utunzaji wa mazingira, nishati, ujenzi na utalii.

3. Milima: Tuna mlima Kilimanjaro na mlima Meru; mlima Kilimanjaro ni wa kwanza kwa urefu barani Afrika, na wa pili duniani. Hii ni muhimu kwa ajili ya utalii wa ndani na nje.

4. Mbuga za wanyama. Tuna mbuga nzuri na maarufu duniani, zikiwemo Manyara, Ngorongoro, Serengeti, Mikumi, Saadan, Gombe, na kadhalika

5. Madini na Vito: Tuna madini mengi kama dhahabu, chuma, urani, chumvi, mafuta, gesi asilia; na Vito kama Almas, Tanzanite, na kadhalika. Hivi vikitumika vyema vitainua uchumi wa nchi na wa MTU mmojammoja.

6. Ardhi Inayofaa kwa Kilimo: Kila wilaya, miongoni kwa wilaya zaidi 160 za Tanzania, zina ardhi ya kutosha inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali ya chakula na ya biashara.

7. Mito na Mabwawa: Vipo maeneo mengi nchini, ambavyo ni muhimu kwa ajili ya matumuzi ya nyumbani, viwandani, mashambani (kilimo cha umwagiliaji), uvuvi, utalii na kuendesha mitambo ya kuzalisha nishati ya umeme.

Tanzania Tuitakayo 2025 -2050
Serikali kuu igatue mamlaka ya kumiliki rasilimali mbalimbali kwa serikali za mitaa na sekta binafsi. Kwa sasa serikali kuu ndio yenye mamlaka juu ya umiliki wa rasilimali nyingi hapa nchini, kama madini, gesi, na mbuga za wanyama. Na wawekezaji kutoka nje ya nchi humilikishwa rasilimali hizi wakati wenyeji wakihamishwa kutoka maeneo ya miradi na kupelekwa maeneo mengine bila kunufaika chochote na miradi husika.

Tunaweza Kubadilika
Mfano: Watu binafsi, asasi za kiraia au vijiji, vinaweza kuwezeshwa kuwa na hati miliki ya rasilimali asili kama ardhi yenye madini, gesi asilia, vitalu vya kuwindia wanyama pori, ardhi ya kilimo na kadhalika; ambavyo vitakuwa mtaji kwao kuweza kukaribisha wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza na hivyo kuwa wabia badala ya kuwa watazamaji. Serikali itakuwa mwezeshaji tu, kuhakikisha mikataba imekaa vizuri ili kila upande unapata stahiki zake katika miradi husika, na kuhakikisha mirabaha na kodi stahiki zinalipwa kikamilifu na kwa wakati.

Mageuzi yanahitaji maamuzi magumu!! Lakini faida ni nyingi sana; kila wilaya itakuwa na wawekezaji wazawa wengi, watakaotoa ajira kwa vijana wengi, wigo wa kodi utapanuka - jambo litakalofanya serikali kuacha kutegemea maeneo manyonge kupata kodi, na hivyo kumwondolea mwananchi tozo za moja kwa moja kama kodi ya ardhi, majengo, tozo za simu, na kadhalika. Mkakati huu, utachechemua uchumi wa mtu mmojammoja na wa taifa na hivyo serikali kupunguza utegemezi kutoka nje.

Vilevile, mageuzi haya yatapunguza, kama sii kumaliza kabisa migogoro kati ya wawekezaji na wenyeji, kama inavyoshuhudiwa mkoani Mara (Wawekezaji katika Mgodi wa dhahabu - Nyamongo na wenyeji). Na mwisho, mazingira ya rushwa yatapungua kwa kiasi kikubwa.

HITIMISHO
Ni vizuri kila mmoja ajue kuwa hatuwezi kutoka kwenye umasikini kwa kutegemea misaada na mikopo kutoka nje; tukubali kufanya MAAMUZI MAGUMU juu ya rasilimali tulizonazo, TUTATOKA hapa tulipo bila SHAKA!!

Rejea
Gazeti la Mwansnchi, Machi 17, 2021, Ukoloni Mamboleo na namna Viongozi Afrika Walivyonaswa.
www.trtafrika.com Ukoloni Afrika
🙏🙏🙏🙏
 
Tatizo lililopo hasa katika nchi zinazoendelea, viongozi waliopo madarakani wanafurahia mifumo iliyoachwa na watawala wa kikoloni. Hii ni mifumo ya watu wachache kuhodhi madaraka makubwa na kuamua hatma ya watu wote katika mikoa, wilaya na hata vijiji ambako kuna kuna viongozi pia.
 
Back
Top Bottom