GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Viongozi wa Mataifa makubwa kama USA ni generational thinkers! Siyo ajabu, akina Biden na Trump wanaiplan Marekani ya miaka mia moja mbele, miaka mingi baada ya wao kuondoka madarakani na hata duniani!
Sisi kama Taifa, viongozi na wananchi kwa ujumla, tuna yapi tunayoyaandaa kwa sasa kwa ajili ya vizazi vyetu miaka mingi mbeleni?
Ningelikuwa na mamlaka, ningeweka mpango utakaowawezesha Watanzania kutambulika kwa sifa zifuatazo miaka 20 mbeleni, labda mwaka 2045. Kwamba, watu wa Mataifa mengine wawafahamu Watanzania kuwa:
1. Wanafanya kazi kwa bidii sana kuzidi siafu
2. Waaminifu mno na wazalendo kwa nchi yao. Hawatoi wala kupokea rushwa
3. Wanaojiamini na ni wajasiri hivyo wanasikilizwa na viongozi wao
4. Wana ushirikiano wa hali ya juu mithili ya nyuki
5. Wanaiheshimu Katiba yao kuliko kitu kingine chochote
6. Wanakimanya Kiswahili na Kimombo kwa ufasaha na hivyo wataalam wao wa lugha wamesambaa sehemu mbalimbali duniani kufundisha lugha ya Kiswahili
7. Wana exposure kubwa sana kwa sababu ni wasomaji hodari wa vitabu na wanaosafiri mara kwa mara kwenda sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi yao
8. Ni wabunifu wanaoambukizana tabia za ubunifu kwa sababu ya ushirikiano walio nao
9. Wako nchi mbalimbali duniani kikazi, kimasomo, na kibiashara kwa sababu wanapenda kutafutiana na kupeana fursa za kimaendeleo
10. Ni waandishi mahiri wa vitabu vinavyosomwa sana duniani
11. Ni kati ya nchi yenye mabilionea wengi barani Afrika
12. Ni wastaarabu sana lakini usije ukalogwa ukawachokoza
Natamani ifikie hatua Watanzania wawe wansongelewa hivyo na Wakenya, Waganda, Wanyarwanda, Warundi, na watu wa Mataifa mengine huko duniani?
Tunawezaje kufika huko?