EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,325
Mambodia ridhaa wanne wa Kitanzania wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja nchini Mauritius baada kupatikana na makosa ya kuingiza nchini humo madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo nne.
Wanandondi hao waliiambia mahakama kuwa waliingiza madawa hayo kwa sababu walikuwa wanahitaji pesa kwa ajili ya matunzo ya familia zao. Walikamatwa mwaka 2008 walipokwenda nchini humo kwa ajili ya mashindano ya ndondi za ridhaa ya Afrika (African Cup of Boxing).
Wanandondi hao wanajulikana kwa majina ya Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa and Petro Charles Mtagwa. Inasemekana wote walikuwa na future nzuri sana ya kuwa mabondia wa kimataiafa mpaka pale walipokamatwa Juni 2008 baada ya polisi kuvamia hoteli kwenye mji wa Quatre Bornes, uliopo kilomita 15 kutoka mji mkuu wa Port Louis, baada ya kikosi cha madawa ya kulevya nchini humo kupata habari za kinteligensia.
Wakijitetea mahakamani hapo, wanandondi hao waliomba radhi kwa taifa la Mauritius na pia kudai kuwa wao ni maskini na wana majukumu mazito ya kifamilia, watoto na wazee wanaowategemea nyumbani. Aidha walidai kama wangefanikiwa kuyauza madawa hayo, wangepata kiasi cha Dola za Kimarekani 5,200.
Akitoa hukumu hiyo, Jaji Marie Joseph alisema kuwa pamoja na majukumu yao ya kifamilia, kukubali makosa yao na kusaidia kukamatwa kwa mwenyeji wao, kosa walilotenda ni kubwa sana kustahili hukumu ya miaka 15. Hata hivyo, Jaji amesema kuwa siku 1,722, ambazo wamekaa gerezani, zitapunguzwa katika vifungo vyao.