Watanzania wanne wafungwa miaka 15 Mauritius

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,325


Mambodia ridhaa wanne wa Kitanzania wamehukumiwa kifungo cha miaka 15 kila mmoja nchini Mauritius baada kupatikana na makosa ya kuingiza nchini humo madawa ya kulevya aina ya heroin yenye uzito wa kilo nne.

Wanandondi hao waliiambia mahakama kuwa waliingiza madawa hayo kwa sababu walikuwa wanahitaji pesa kwa ajili ya matunzo ya familia zao. Walikamatwa mwaka 2008 walipokwenda nchini humo kwa ajili ya mashindano ya ndondi za ridhaa ya Afrika (African Cup of Boxing).

Wanandondi hao wanajulikana kwa majina ya Ramadhani Fills, Nathanael Elia Charles, Ally Rajabu Msengwa and Petro Charles Mtagwa. Inasemekana wote walikuwa na future nzuri sana ya kuwa mabondia wa kimataiafa mpaka pale walipokamatwa Juni 2008 baada ya polisi kuvamia hoteli kwenye mji wa Quatre Bornes, uliopo kilomita 15 kutoka mji mkuu wa Port Louis, baada ya kikosi cha madawa ya kulevya nchini humo kupata habari za kinteligensia.

Wakijitetea mahakamani hapo, wanandondi hao waliomba radhi kwa taifa la Mauritius na pia kudai kuwa wao ni maskini na wana majukumu mazito ya kifamilia, watoto na wazee wanaowategemea nyumbani. Aidha walidai kama wangefanikiwa kuyauza madawa hayo, wangepata kiasi cha Dola za Kimarekani 5,200.

Akitoa hukumu hiyo, Jaji Marie Joseph alisema kuwa pamoja na majukumu yao ya kifamilia, kukubali makosa yao na kusaidia kukamatwa kwa mwenyeji wao, kosa walilotenda ni kubwa sana kustahili hukumu ya miaka 15. Hata hivyo, Jaji amesema kuwa siku 1,722, ambazo wamekaa gerezani, zitapunguzwa katika vifungo vyao.
 
nimesoma heading tu nikajua ndo yale yale ya madawa ya kulevya!
 


Hapo kwenye red, ni kweli dola 5,200 au umekosea kuquote!?
 
Hapo kwenye red, ni kweli dola 5,200 au umekosea kuquote!?

Vipi ni nyingi sana? Basi ngoja ni-convert kwa sarafu ya Kitanzania.

Aidha walidai kama wangefanikiwa kuyauza madawa hayo, wangepokea kiasi cha Sh. 8,504,556.74
 
Hapo kwenye red, ni kweli dola 5,200 au umekosea kuquote!?

Kamanda Limbani ,inaelekea unajua bei za bidhaa hizi walizokamatwa nazo hawa mburula!!!Je hizo $5,200 kwa kilo nne ni ndogo?
 
Kamanda Limbani ,inaelekea unajua bei za bidhaa hizi walizokamatwa nazo hawa mburula!!!Je hizo $5,200 kwa kilo nne ni ndogo?

Kidogo nimwulize hivyo pia.

Kosa ni kosa regardless ya kiasi walichokuwa wanategemea kupata.
 
Mtuhumiwa halisi mahakama zetu zimemwachia huru....



HATIMAYE Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemwachia huru aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Alhaj Shaban Mintanga aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kusafirisha dawa za kulevya nchini Mauritius baada kumuona hana kesi ya kujibu.

Alhaj Mintanga, hadi kuachiwa jana, alikuwa amesota Gereza la Ukonga kwa takribani miaka minne, kabla ya kesi yake kutolewa hukumu.

Uamuzi huo umetolewa jana na Jaji Dk. Fauz Twaib na kusababisha mtuhumiwa huyo aliyekuwa akitetewa na mawakili maarufu wa kujitegemea nchini, Jerome Msemwa na Yasin Memba, kurejea uraiani na kuungana na familia yake.

Akitoa uamuzi huo, Jaji Dk.Twaib alisema, ameisikiliza kesi hiyo tangu ilipohamishiwa mahakamani hapo mwaka juzi, ikitokea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako upande wa Jamhuri ili kuthibitisha kesi yao, walileta mashahidi wanne na vielelezo.

Dk. Twaib alisema, baada ya kupitia kwa kina vielelezo na ushahidi uliotolewa na mashahidi hao wa upande wa Jamhuri, imebaini ni havifu na umeshindwa kuishawishi mahakama imuone Mintanga ana kesi ya kujibu, hivyo inamwachilia huru.

Jaji Dk.Twaib, akiuchambua ushahidi huo, alisema kwa mujibu wa cheti kilichotolewa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania na ambacho kilikuwa kimesainiwa na Mkuu wa tume hiyo, Christopher Shekiondo, kinaonesha dawa za kulevya alizokuwa akituhumiwa Mintanga kuzisafirisha kwenda Mauritius, zina uzito wa kilo 4.9 na cheti kilichotolewa na Interpol, kinaonesha zilikuwa na uzito wa kilo 6.

"Kwanza mahakama hii imejiuliza ni Shekiondo ndiye aliyethibitisha dawa zile aina ya Heroin zina uzito huo ambao unatofautiana na uzito wa ulitolewa na Interpol, mahakama imejiuliza ni kwanini basi upande wa Jamhuri umeshindwa kumleta mahakamani hapa Shekiondo ambaye anaishi Dar es Salaam ili athibitishe ni yeye ndiye aliyetoa cheti hicho, kinachoonesha uzito huo na kama kweli aliziona dawa hizo kwa zilizokamatwa kwa macho na kisha akazipima na kutoa hati ile.

"Kwani kuna baadhi ya mashahidi waliieleza mahakama kuwa, Shekiondo licha kutoa cheti kile cha kuonesha thamani ya dawa zile, hakuwahi kuziona kwa macho dawa hizo," alihoji Jaji Dk.Twaib.

Jaji huyo alisema, hata hivyo ushahidi wa mashahidi hao umekuwa ukipingana, kwani mshitakiwa alikuwa anakabiliwa na kosa la kusafirisha dawa za kulevya, lakini shahidi wa nne ambaye ni ofisa wa Jeshi la Polisi, Charles Ulaya, aliiambia mahakama kuwa, Mintanga alipaswa kushitakiwa kwa kosa kula njama tu, sio kusafirisha dawa hizo.

"Hata kama hivyo ndivyo kama alivyoeleza Ulaya, lakini mahakama hii imeona pia upande wa Jamhuri umeshindwa kulithibitisha kosa hilo la kula njama, kwani wameshindwa kuleta ushahidi unaoonesha Mintanga na wenzake hao walikaa wapi, lini, saa ngapi na wakapanga njama za kusafirisha dawa hizo haramu aina ya Heroin na kwa sababu hiyo, mahakama hii inamwachilia huru mshitakiwa, kwa sababu imemuona hana kesi ya kujibu," alisema Jaji Dk.Twaib.

Aidha, Jaji huyo alisema, karibu mashahidi wote walikuwa wakilitaja jina la mtu mmoja aitwaye (Michael), ambaye hakuwepo mahakamani.

Naye Charles Ulaya ambaye ndiye alikuwa akipeleleza kesi hiyo, alisema jina la Michael walipewa na Interpool na siyo jina la Mintanga katika sakata hilo la kusafirisha dawa za kulevya, ambalo mwisho wake lilisababisha Mintanga kufunguliwa kesi hiyo mahakamani hapo.

Jaji huyo akipangua hoja ya mawakili wa Jamhuri, iliyodai kuwa namba ya simu ya Mintanga ndiyo iliyotumika kufanyia ‘booking' kwenye kampuni za usafirishaji kwa njia ya ndege, alisema, baada ya kupitia vielelezo, amebaini ile namba ya simu ni mali ya ofisi ya BFT, na ndiyo maana namba hiyo ipo kwenye ‘headpaper' za shirikisho hilo na kwamba, mfanyakazi yoyote wa shirikisho hilo anaweza kuitumia, hivyo simu ile siyo mali ya Mintanga binafsi ni mali ya shirikisho.
 
Reactions: EMT
Camaraderie, hapa kwetu systems zetu zote zimeoza vibaya! DPP, Polisi na Mawakili wa serikali hushirikiana ktk kufinyanga na kuharibu kesi ili zikose hoja za kisheria baada ya kuchukua chao mapema! Kinyume chake huwa vilevile katika kutengeneza kesi kwa watu walio kinyume na maslahi yao au ya mabwana zao.
 
Kamanda Limbani ,inaelekea unajua bei za bidhaa hizi walizokamatwa nazo hawa mburula!!!Je hizo $5,200 kwa kilo nne ni ndogo?
Hizo ni ndogo sana kwa kilo nne, jamaa wanameza gramu mia kadhaa na wakirudi bongo mtaani hatukai kwa raha! Mikoko kadhaa na mpaka kununu nyumba so ukiniambia kilo 4 ni USD 5,200 ambayo haizidi hata Tsh 10 milioni sio kweli!
 
Vipi ni nyingi sana? Basi ngoja ni-convert kwa sarafu ya Kitanzania.

Aidha walidai kama wangefanikiwa kuyauza madawa hayo, wangepokea kiasi cha Sh. 8,504,556.74

Ni kidogo sana mkuu
 
Who is behind these innocent guys ambao wamekatiwa miaka yote hiyo jamani.Huenda yeye yupo tu anapeta, mimi siwezi kufa kishujaa namna hiyo lazima nimtaje alienituma
 

Interesting. Ina maana kesi yake ilikuwa na connection na hii ya waliohukumiwa Mauritius baada ya kukubali makosa yao?

Ushahidi huo wa mazingira ambao upande wa mashtaka uliuegemea ni namba za simu zilizodaiwa kukutwa kwenye tiketi za watu wanaodaiwa kukutwa na dawa hizo nchini Mauritius.
 

Huyu ndie aliyewatuma na kuwabebesha unga, jamaa wa Mauritius walimtaka sana apelekwe kule kuunganishwa na hawa jamaa lakini kama unavyojua bongo yetu ilipigwa danadana mwisho akaachiwa huru. Kilo moja ya unga ni around Tsh 100ml kwa soko nzuri, hiyo USD 5200 ni bei ya Colombia "shambani"
 
Reactions: EMT
Hizo ni ndogo sana kwa kilo nne, jamaa wanameza gramu mia kadhaa na wakirudi bongo mtaani hatukai kwa raha! Mikoko kadhaa na mpaka kununu nyumba so ukiniambia kilo 4 ni USD 5,200 ambayo haizidi hata Tsh 10 milioni sio kweli!

Labda Dola za Kimarekani 5,200 zingekuwa gawio lao na nyingine kwenda kwa mwenye mzigo?
 

Kamanda Limbani, kuhusu biashara ya bidhaa hii nimekuaminia!!
 
Reactions: EMT

Halafu hawa jamaa walikuwa amateurs.

Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.

Kifuko kimoja kinaweza kuwa bei gani?
 
Halafu hawa jamaa walikuwa amateurs.

Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.

Kifuko kimoja kinaweza kuwa bei gani?

Calculation mkuu! 4639.04gm/358 = approx. 13 grams per pipi. Then 1000gm = 100ml Tsh(lets say), then 13 grams (one kete aka pipi) ni sawa na 13 X 100,000,000Tsh/1000gm = 1.3m Tsh! Amazing business! Ndio maana nikashangaa kuniambia its only $5,200.. sababu jamaa wanameza kete/pipi 10-15 na wanarudi na vurugu bongo, so kwa kilo 4 its lots of money
 
Reactions: EMT
Halafu hawa jamaa walikuwa amateurs.

Kwa pamoja walimeza gram 4639.04 za heroin zikiwa katika vifuko 358 vijulikavyo kama pipi.

Kifuko kimoja kinaweza kuwa bei gani?
Haijalishi ni wazo lao au wazo la mtu mwengine, tanzania tunatia aibu nchi yetu sasa, kila kukiwa na mashindano ya kimichezo ndani na nje ya nchi lazima wachezaji wabebe madawa ya kulevya!! sikuzote michezo inahamasisha vijana kuwa na tabia njema, sasa mwana michezo kuuza unga ni sawa na mchungaji au ustadh kufungua danguro.... hivi hapa kwenye uwanja wetu wa taifa hakuna ving'amuzi vya haya madudu..????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…