Labda Dola za Kimarekani 5,200 zingekuwa gawio lao na nyingine kwenda kwa mwenye mzigo?
.....kila kukiwa na mashindano ya kimichezo ndani na nje ya nchi lazima wachezaji wabebe madawa ya kulevya!!
Calculation mkuu! 4639.04gm/358 = approx. 13 grams per pipi. Then 1000gm = 100ml Tsh(lets say), then 13 grams (one kete aka pipi) ni sawa na 13 X 100,000,000Tsh/1000gm = 1.3m Tsh! Amazing business! Ndio maana nikashangaa kuniambia its only $5,200.. sababu jamaa wanameza kete/pipi 10-15 na wanarudi na vurugu bongo, so kwa kilo 4 its lots of money
Ila wala sembe wana moyo aisee.
Yaani wanakula sembe ambayo imemezwa na kutolewa kupitia haja kubwa ya watu wengine?
Inawezekana ndio ulikuwa ujira wao pamoja na posho ya kupendelewa kwenda Mauritius kupeleka unga. Maana Nassor Michael yeye alikuwa bondia wa ukweli na walikuja kumwachia baada ya kugundua kuwa yeye hakuwemo kwenye huo mpango!
Hivi huwa wanabeba au wanabebeshwa hayo madawa?
Wachezaji ambao ni amateurs (siyo professionals) wanapata wapi kilo nne za heroin?
Kwani Bongo tuna shamba la heroin?
[TABLE="width: 0"]
[TR]
[TD]
Yea, nadhani Nassor Michael alikuwa kocha wa hiyo timu. Wapo mabondia wengine waliachiwa pia. Pia issue inaonekana ilikuwa serious kipindi hicho.
[TABLE="width: 0"]
[TR]
[TD]BONDIA Emillian Patrick aliyekamatwa nchini Mauritius Juni, 2008 kwa tuhuma za kuingiza dawa ya kulevya aina ya heroin zenye thamani ya shilingi milioni 600 amerejea nchini kuungana na familia yake.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Taarifa za uhakika ambazo timu ya Nifahamishe.com imezipata bondia huyo alirejea nchini mwishoni mwa wiki na mara alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere alishikiliwa na maofisa Uhamiaji na wale wa kitengo cha kuzuia dawa za kulevya.
Na baadaye, alitoa maelezo yake kwenye kitengo cha kuzuia dawa za kulevya ambako aliachiwa kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na ndugu zake.
Patrick alikamatwa akiwa na bondia mwenzake Petro Mtagwa na kocha wao Nassor Michael hotelini wakati walipokuwa nchini humo kushiriki mashindano maalum ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki iliyofanyika China.
Wakati huo, tayari Patrick ambaye anapigana kwenye uzito wa bantam (kilo 54) alikuwa amefuzu kwa michezo hiyo na kupata tiketi ya kuiwakilisha Tanzania baada ya kupata medali ya fedha nchini Namibia, lakini kwa vile alikuwa mahabusu hakuweza kwenda China kuiwakilisha Tanzania.
Hata hivyo, hatima ya Nassor na Mtagwa bado haijajulikana na wanaaendelea kushikiliwa na mamlaka za dola za nchini Mauritius. Alipotafutwa kwa njia ya simu, Patrick aligoma kuzungumza na mwandishi wetu lakini pia akikacha kupokea simu zozote kutoka kwa watu asiowajua.
Wakati wa sakata la kukamatwa kwao, timu hiyo ya Tanzania iliunganishwa na watu wengine watatu ambao hawakuwa mabondia, lakini walionekana kuwemo kwenye orodha ya timu na kujitambulisha kama viongozi waliomo kwenye msafara huo. Kutokana na kashfa hiyo, timu ya ngumi ya Tanzania ilitimuliwa kushiriki michuano hiyo ya Mauritius.
Baada ya kukamatwa kwa mabondia hao, walisomewa mashtaka yao katika mahakama ya Mahébourg kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya.
Kutokana na kukamatwa kwao, aliyekuwa rais wa Shirikisho la Ngumi Tanzania, Shaaban Mintanga, alikamatwa jijini Dar es Salaam kabla ya kupelekwa mahakamani kusomewa mashtaka ambayo yalikuwa yakilingana na yale waliyosmewa mabondia huko Mauritius. Kesi yake bado inaunguruma.
Lakini pia, Tanzania ilisimamishwa uanachama wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa, ABC, kabla ya kurejeshwa baada ya kamati nzima ya utendaji iliyokuwa chini ya Mwintanga kujiuzulu kupisha uchaguzi mkuu kufanyika na kumwingiza madarakani Joan Minja.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Bondia Aliyekamatwa na Madawa ya Kulevya Mauritius Arejea Nchini[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Biashara ngumu sana hii mkuu, kabla ya kumeza hakuna kula ni mwendo wa biskuti na maji ili usipate choo ukaacha mzigo chooni. No alcohol (late msanii wetu) utavuruga chemistry tumboni. Its a risky businessm but always risky business pays well!
Watumiaji sasa. Wanakuwa wanajua kabisa kuwa kitu kililala tumboni mwa mtu kwa siku kadhaa kabla ya kutolewa kwa njia ya haja kubwa? Au wanakuwa wanadhani ni raw material imetoka direct shambani?
Miongoni mwa hawa jamaa huyo Elia Nathaniel ni mchezaji wa Zamani wa Simba SC winga msimu wa miaka 1997- 2000 na haikuwahi kutokea kuwa bondia hata siku moja.. inashangaza sana inaonekana alikubali kubebe mzigo ili mradi agange njaa ...
| Ushahidi ulitolewa na Jamhuri dhidi ya Alhaji Shaban Mintanga unachanganya. Kwa mfano, shahidi wa pili wa upande wa mashtaka, Nassoro Michael Irenge aliyekuwa kocha wa timu hiyo wakati wanaenda nchini Mauritius alidai kuwa watu waliokamatwa na dawa hizo walitambulishwa kwake na mshtakiwa (Alhaji Shaban Mintanga) kuwa wataambatana na timu hiyo kama mashabiki. |
Kukiwa na misafara ya kwenda nje kwa wanamichezo, wafanyabiashara ndio wanatumia "opportunity" ya kufanya mambo hayo. Sasa kama huyi dogo Elia Nathaniel yeye alikuwa mcheza mpira na alishachezea mpaka Simba SC, lakini akaingia msafara wa wanandoni kwenda Mauritius! Ndio maana nasema Mzee Mwintanga ndiye muhusika mkuu akiye organise hii kitu na kupewa "mizigo" na wafanyabiashara awasafirishie mali yao. Ila kwa kuwa "wafanyabiashara" wenyewe wamejikita kwenye CCM na serikali yake yeye anapeta tu!
Kwa stahili hiyo, hata wao wote kukubali makosa si inatia wasiwasi?
Usijekuta ni covering tuu na mwisho tutakutana nao kitaaa.
Jamaa huwa wanaambia msijali yataisha, mtakaa miaka kadhaa then nje huku familia yao ikipewa pesa nzuri ya kujikimu ili tu wasiseme nani kawabebesha! wale jamaa hawana uwezo wa kununua hata nusu ya kilo ya unga na kupeleka Mauritius, walikuwa makontena tu!
Nimesoma Mbwana Matumla nae amekamatwa na madawa huko Spain.