pichani ni mchezaji maarufu zaidi NBA Lebron James futi 6'8 / sentimita 208
Siku ya jana nilikuwa nimeenda kupasha mazoezi uwanjani kukimbia raund zangu, nilienda kupumzika kwenye court ya baketball nikawa nawasikia vijana wanapeana moyo wa kucheza nba, vimo vyao hakuna hata moja aliefika futi 6'1 (sentimita 186 ) mrefu yupo kwenye 5'8 (sentimita 177)
Nilibaki kushangaa kwasababu huwa nachukulia wanacheza kujifurahisha kumbe wapo serious wana ndoto za kufikia NBA
Marekani ligi ya wanaume NBA urefu wa wastani ni futi 6'6 / mita 2 / centimeter 200, wachezaji wafupi maarufu ni kina Stephe Curry mwenye 6'2 (Centimeter 182)
ligi ya wanawake wnba urefu wa wastani ni futi 6'0 / mita 1.83 / centimeter 183, wachezaji maarufu ni
- Angel Reese , mita 1.91 / centimeter 191
- Caitlin Clark , mita 1.83 / centimeter 183
Tukirudi kwetu hapa wenye wenye 6'2 (Centimeter 182) bado ni wachache sana, wakipita wanaacha gumzo, inaweza kuwachukua mwezi mzima kukutana na waliolingana au kuwazidi. kwa wenye 6'3, 6'4 na kuendelea wapo ila wanahesabika, huonekana ni watu wa ajabu.
Ingefaa tujikite zaidi kwenye mpira wa miguu kina Samata wameweza, sarakasi kama Ramadhan Brothers, kukimbia kama Filbert Bayi, n.k.