Pre GE2025 Watanzania watakiwa kujitokeza kujiandikisha kwenye Dafrari la kudumu la Wapiga Kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.George Simbachawene ametoa wito kwa Watanzania wenye sifa za kujiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kujitokeza kwa wingi katika vituo ili kupata Kitambulisho cha Mpiga Kura kitakachowawezesha kupata haki ya kuchagua Viongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao .

Pia, Mhe.Simbachawene amewataka Watumishi wa Umma nchini kuhakikisha wanatumia haki yao kujiandikisha kwenye daftari hilo ili kuwawezesha kuchagua viongozi akiwemo Rais, Wabunge pamoja na Madiwani kwenye uchaguzi huo .

Mhe.Simbachawene ametoa wito huo leo Jumatatu Desemba 30, 2024 mara baada ya kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kituo cha Wapiga Kura kilichopo Kata ya Pwaga Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Amesema kitendo cha kwenda kuboresha taarifa katika kituo husika kwa Mtumishi wa Umma ni kujihakikishia usahihi wa taarifa zake pamoja na uhakika wa mahali atakapopigia kura.

“ Nimefika hapa ndani ya muda mfupi nimeboresha taarifa zangu ambapo nimepata kitambulisho kipya kitakachoniwezesha kutumia haki yangu ya kidemokrasia muda utakapowadia wa
kuchagua na kuchaguliwa ”, amesema Mhe.Simbachawene.

Katika hatua nyingine Mhe.Simbachawene ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuboresha zoezi hilo na kufanya kazi kwa weledi inayoimarisha Demokrasia nchini huku akisifu jinsi zoezi hilo linavyoendesha kwa umakini na uharaka ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zingine za kujiingizia kipato

Aidha, Mhe.Simbachawene amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kuendelea kuimarisha Demokrasia nchini na kuendelea kuiwezesha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
 
Warekebisha kwanza mfumo mzima wa uchaguzi. Mambo ya magoli ya maradona hatuyataki tena.
Katiba mpya
Tume huru ya uchaguzi
Tukivipata hivi ndio tuende kwenye uchaguzi.
 
Mnihakikishie kwanza ulinzi wa kura yangu. Haiwezekani mtu apoteze muda wake kujiandikisha, na hata kupiga kura! Halafu msimamizi wa uchaguzi ndiyo aamue mtu wa kumtangaza.
 
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe, Mhe.George Simbachawene ametoa wito kwa Watanzania wenye sifa za kujiandikisha katika Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kujitokeza kwa wingi katika vituo ili kupata Kitambulisho cha Mpiga Kura kitakachowawezesha kupata haki ya kuchagua Viongozi katika Uchaguzi Mkuu ujao .

Pia, Mhe.Simbachawene amewataka Watumishi wa Umma nchini kuhakikisha wanatumia haki yao kujiandikisha kwenye daftari hilo ili kuwawezesha kuchagua viongozi akiwemo Rais, Wabunge pamoja na Madiwani kwenye uchaguzi huo .

Mhe.Simbachawene ametoa wito huo leo Jumatatu Desemba 30, 2024 mara baada ya kuboresha taarifa zake kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Kituo cha Wapiga Kura kilichopo Kata ya Pwaga Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma.

Amesema kitendo cha kwenda kuboresha taarifa katika kituo husika kwa Mtumishi wa Umma ni kujihakikishia usahihi wa taarifa zake pamoja na uhakika wa mahali atakapopigia kura.

“ Nimefika hapa ndani ya muda mfupi nimeboresha taarifa zangu ambapo nimepata kitambulisho kipya kitakachoniwezesha kutumia haki yangu ya kidemokrasia muda utakapowadia wa
kuchagua na kuchaguliwa ”, amesema Mhe.Simbachawene.

Katika hatua nyingine Mhe.Simbachawene ameipongeza Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuboresha zoezi hilo na kufanya kazi kwa weledi inayoimarisha Demokrasia nchini huku akisifu jinsi zoezi hilo linavyoendesha kwa umakini na uharaka ili kuwawezesha wananchi kuendelea na shughuli zingine za kujiingizia kipato

Aidha, Mhe.Simbachawene amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa kinara wa kuendelea kuimarisha Demokrasia nchini na kuendelea kuiwezesha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.
Ninyi wahuni Mwaka 2025 hakuna uchafuzi, Tutafanya juu chini usifanyike.
 
Back
Top Bottom