Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
TANZANIA imefungua ukurasa mpya wa kuwa na watalaamu wa ndani katika taaluma ya kuzalisha umeme baada ya kikundi cha watu 20 kufanikiwa kutengeza mtambo wa kuzalisha umeme wa upepo.
Mtambo huo unaojulikana kwa jina la Hugh Piggot Wind Turbine, umetengenezwa mahsusi kupunguza tatizo la umeme vijijini.
Watanzania hao wameweza kutengeneza mtambo huo baada ya kuhudhuria mafunzo yaliyoandaliwa na Kituo Cha Maendeleo ya Nishati Endelevu na Kisasa (Sadec) cha jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa mafunzo hayo, Emmanuel Yesaya alisema washirki walifanikiwa kutengenza mashine tatu za kuzalisha umeme kwa kutumia upepo huku asilimia kubwa ya malighafi zilizotumika zikitokea hapa nchini.
Washiriki wamefanikiwa kutengeneza mashine tatu za kuzalisha umeme, moja inazalisha umeme wa Wati 350-1000,230 V (ukitumia inveta) mashine hizi zina ufanisi kwa asilimia 55 hadi 60alisema Yesaya.
Yesaya alizitaja malighafi zilizotumika kutengeneza mtambo kuwa ni mbao ambazo hutumika kutengeneza mapanga,Chuma hutumika kutengeza nguzo na nyaya za shaba na sumaku.
Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Uholanzi Dk Roland Valckenborg alisema kazi yake ilifanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani alifundisha kwa vitendo zaidi kuliko nadharia.
Washiriki wamejifunza kwa vitendo zaidi na wamefanikiwa kutengeneza mtambo huu wa Hugh Piggot Turbine,hii ni ishara kuwa sasa nimeacha kitu hapa Tanzaniaalisema Valckenborg,mtaamu wa umeme wa upepo kutoka Uholanzi.
Alisema umeme wa upepo ni jibu mwafaka kwa nchi ya Tanzania ambayo asilimia kubwa ya watu wake wanaishi vijijini huku wakikabiliwa na ukosefu wa umeme unaotokana na gridi ya taifa.
Nimekuja kwa lengo moja la kutoa mafunzo hapa Tanzania,nawapongeza wahitimu kwakuwa waliyazingatia mafunzo hayoalisema Valckenborg.
na kuongeza Hii ni ishara kuwa kazi ya kutengeneza na kusambaza umeme katika maeneo ya vijijini ambayo ambayo hayajafikiwa na Umeme wa Gridi ya Taifa itakuwa endelevualisema.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa TaTEDO Leonard Pesambili aliwapongeza wahitimu hao kwa kupata mafunzo hayo na kuwataka kusambaza taaluma hiyo kwa jamii kuhusu umeme wa Upepo.
Alisema hadi sasa ni asilimi 2 tu ya watu wa vijijini ndio wanaopata huduma ya umeme na kwamba hali hiyo inatokana na eneo kubwa la nchi kutofikiwa na Grid ya Taifa.
Alisema kutokana namafunzo hayo Aasi yake inayojishughulisha na kazi yakuhifdhi mazingira itaendela kuwatumia katika kusambaza elimu kwa watanzania wengine ambao hawajaipata.
Niimani yangu kuwa mafunzo haya yamewapa uelwa juu ya uhusiano uliopo kati ya Nisharti,Maendeleo,utunzaji Mazingira na kupunguza umasikini,mafunzo haya yamewapa wigo mpana wa uelewa juu ya Teknolojia ya kisasa kuhusu nishati endelevualisema Pesambili
Pesambili alitaja faidi za umeme wa Upepo kuwa ni pamoja na kuendelza kuhiofadhi mazingira hapa nchini kuinua uchumi kwa wanchi wanaoishivijijni.
Alisema TaTEDO wanafanya kazi ya kuhifadhi mazingira hivyo kusambazwa nisharti ya umeme unaotumia nguvu ya upepo kutasaidi kuhifadhi mazingira na kuwaletea maendeleo wakazi wa vijijini.
Mafunzo hayo ya wiki mbili yaliyoandaliwa na TaTEDO kwa kushirikiana na Dk Roland yalihudhuriwa na washiriki 20 kutoka katika Taaisi mbalimbali za mikao ya Tanzania bara na Visiwani.
Chanzo: Watanzania watengeneza mtambo kuzalisha umeme
Nawaunga Mkono hao Watanzania walioweza Kutengeneza Umeme unaotokana na Upepo nawapa Hongera Watanzania kumbe wanao akili ya kuvumbuwa kitu.
Chanzo. Watanzania watengeneza mtambo kuzalisha umeme