Watanzania wengi hatujui kujenga hoja (Make a Case): Ebu msikilize Profesa Kitila Mkumbo akijenga hoja

Watanzania wengi hatujui kujenga hoja (Make a Case): Ebu msikilize Profesa Kitila Mkumbo akijenga hoja

the power

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
407
Reaction score
799
This goes without say. Hata humu ndani ya jumuiya yetu ya jamii forum utagundua udhahifu mkubwa sana kwenye suala la namna tunavyojenga hoja, au kujibu hoja, au kutetea hoja. Suala la kujiuliza ni zipi sababu za udhaifu wetu huu mkubwa? je ni elimu yetu mbovu? je ni jinsi tulivyokuwa groomed? je ni social cultural issues zetu? je ni madhara ya uswahili wetu? au ni sula la IQ ndogo?. Tena utakuta baadhi ya wasomi wetu nguli humu ndani ndio wanaongoza kwa udhaifu huu.

Screenshot 2024-06-06 164648.png

Ebu msome waziri wa nchi ofisi ya Rais , Mipango na uwekezaji Professor Mkumbo akimake a case, akijibu hoja ya kuhusu taarifa iliyotolewa na Sauti ya America kuhusu mkopo uliosainiwa juzijuzi huko Korea , jamaa walitangaza ni mkopo wa miaka 40 kati ya Tanzania na Korea na kwamba mkopo umetoa masharti dhaifu ya kuiachia Korea kuchimba madini baharini.

Sasa anayejibu anatakiwa; Kwanza kusema je ni kweli mkataba umesainiwa? je ni wa miaka mingapi? je ni kweli wameachiwa kiurahisi tu kuchimba (kuchota) madini baharini, je hiyo ni sehemu ya colateral ya mkataba? kama sio ni kitu gani kuhusu madini kilisainiwa?. Angalau atoe high level update kuondoa sintofahamu hii kwani tunajua mikataba hii huwa ya siri kubwa sana.

"Huo ni Urongo! kuhusu madini ya Kimkakati (strategic mineral resources) Mkakati wa Tanzania ni kutafuta wawekezaji watakao wekeza katika utafiti, uchimbaji na kuongeza thamani ya maliasili hiyo kwa kujenga viwanda na kuexport end producst (betries etc)". Hayo ndiyo yalikuwa majibu ya professor, hakika hivyo ndivyo mtaalamu wetu, kiongozi wa sekta husika alivyojenga hoja (make a case) pinzani, kupinga tuhuma nzito na za kutia hofu toka Sauti ya America.

Politically ni bora husijibu kama huna majibu yanayojitosheleza kwani majibu yako dhaifu yatatengeneza maswali zaidi na kujenga hofu hasa linapokuja suala la current increasing trend, au observed epidermic au pandemic ya uuzwaji wa maliasili za nchi kwa wageni bila wenye nchi , wenye mali kujua details zake.

Swali la msingi la mada hii ni je? huyu professor wetu ameweza kujenga hoja? ameweza kuivunja hoja pinzani? ameweza kukosha mioyo ya Watanzania walio na shahuku kusikia kauli sahihi ya Serikali yao pendwa? Je alitakiwa kujibu nini kuhusu miaka ya mkataba? je kuruhusiwa kuchimba madini ni sehemu ya collateral binding of the signed contract? sawa labda wameruhusiwa je? watafungua viwanda humuhumu kama Country Strategic Mineral Resources development plan inavyosema?

Kikubwa kwenye kizungumkuti kama hiki ni kuhusu hoja ya mkataba uliosahiniwa umewaruhusu wakorea kuchimba madini au hapana? to the contrary, Mheshimiwa katoa jibu la kuelezea the current Country strategic mineral resources development plan, kweli kwani hilo ndilo lilikuwa swali? Basi OK umetaka strategically kuficha specific content kama professor basi tulitegemea ungesema suala si kuruhusiwa kwani our strategic mineral resources development plan iko wazi kwa wawekezaji ila angesema wameweza kutimiza masharti husika kwamba hawa wenzetu sio tu wamekidhi vigezo bali wamefuata masharit yote , kufanya utafiti, uchimbaji na kukubali kuanzisha viwanda vya kuzalisha end product ili kuuza nchi za nje kwa manufaa makubwa ya nchi.

Hakika tunasafari ndefu kama haya ndiyo majibu ya professor wetu na yeye alikuwepo na kausoma mkataba mwezi au miezi kabla ya kusahiniwa na na aliweza kutoa ushauri process iendelee, je unategemea sisi wengine kajamba nani uwezo wetu utakuwaje kwenye kujenga hoja?
 
The source of the problem most likely stems from the education system which doesn’t emphasis on critical thinking.

No wonder we keep losing cases in arbitrations.
 
Kiswahi fasaha ni "hebu" sio "Ebu" kama ulivyo tumia kwenye andiko lako.

Tatizo pia linaanzia kwenye matumizi fasaha ya lugha. na hapa namaanisha lugha zote; kiswahili na kizungu.
 
KAMA WANASHINDWA KESI MA PROFESA WANAOFUNDISHA SHERIA WATAWEZA KUJENGA HOJA.

MIMI NILIACHA KUMSIKILIZA PROF KABUDI "MAGUFURI KANITOA MAJALALANI"
 
Hili kiukweli ni tatizo kubwa sanaa, na bahati mbaya zaidi kuingia kwa uchawa, ambako hakuangalii ujengaji na ujibu wa hoja bali kupayuka na kusifia mambo wanayopenda kuyasikia wanaonawtuma, ndiyo kumekuza tatizo ambalo tayari lilikuwepo.
 
And you believe you have strongly made your case?

Eti Watanzania Wengi! Watanzania wengi ni wangapi?
"Humu Jamii Forums" pamoja na Interview ya Waziri Mmoja. ni Watanzania wengi?

Kwa Ushahidi upi huo?
Kwa Utafiti upi huo?
 
And you believe you have strongly made your case?

Eti Watanzania Wengi! Watanzania wengi ni wangapi?
"Humu Jamii Forums" pamoja na Interview ya Waziri Mmoja. ni Watanzania wengi?

Kwa Ushahidi upi huo?
Kwa Utafiti upi huo?/hoja

Nafikiri swali lingekuwa umetumia kigezo gani kusema "watanzania wengi". Nafikiri unajua kuna njia nyingi za kumake conclusion; zingine ni rough estimation, zingine ni scientific research etc.

Kujibu swali lako, Nakuomba upitie issues /hoja /mada critical zinazotolewa na wanajamii mahili humu ndani. Halafu pitia responses zetu ndipo utajua ninamaanisha nini. utakuta asilimia zaidi ya 50% wamemuattack mtoa mada au wamemdhihaki au wametoa hoja pinzani ambayo haiendani kabisa na hoja ya mtoa mada, au wameingiza siasa kwenye hoja ya msingi Hapa huitaji kufanya sampling ni quick observation. Lakini pia nenda kwenye makundi mengine ya whats up etc, huko nako fanya nilivyosema utagundua the same. Kibaya njoo makazini kwetu, fanyisha interviews na kama ulishafanya interviews kwa watanzania tena hata kwenye post kubwa za umenager, COP, directorate position, sikiliza content na namna ya responses za wasomi wetu. Pia sikiliza tu watanzania tunavyojenga hoja kwenye maongezi ya kawaida ndipo utajua niko sahihi.

Zaidi unaweza kulinganisha na wenzetu wa nchi nyingine wala sio mbali hata Kenya, south afrika n.k ndipo utagundua tuna tatizo, tumia vigezo hivyo hivyo. Sioni haja ya kubisha , nimesema watanzania wengi maana yake na mimi nimejiweka. Suala si kubisha , suala ni kujiuliza what exactly happened kama ambavyo wengi wamejaribu kujibu. Nimekupa mfano wa professor alivyojibu hoja hapo juu, kumbuka huyu ni professor, na ndivyo watu wengi tunavyojenga hoja.

Kuna msemo unasema mficha uchi hazai. "Let us openly discuss about our problems " . Let avoid our denial from limiting our ability to openly discuss critical issues which directly affect our daily life.

Bottom line sijasema sual la IQ kwani hapo ndipo ungeniuliza a scientific and justifiable methodology kwani kuna steps na variable nyingi za kuconsider kabla ya kumake conclusion. Nimesema namna tunavyojenga hoja kitu ambacho ni just observation. Ifike mahali tukubali ukweli
 
The source of the problem most likely stems from the education system which doesn’t emphasis on critical thinking.

No wonder we keep losing cases in arbitrations.
Nakubali kabisa, na mojawapo ya variable muhimu kwenye kujenga hoja ni critical thinking. Hili pia ni janga, kumbuka education inabidi iweze kuimarisha our thinking yetu.
 
And you believe you have strongly made your case?

Eti Watanzania Wengi! Watanzania wengi ni wangapi?
"Humu Jamii Forums" pamoja na Interview ya Waziri Mmoja. ni Watanzania wengi?

Kwa Ushahidi upi huo?
Kwa Utafiti upi huo?
Huu pia ni mfano wa hoja yangu juu, Eti ushahidi, eti utafiti; hivi umeshindwa kutumia sources mbalimbali za interaction formal and informal kumake a plausable random estimation. Sio kitu kinahitaji formal research inategemea na issue under discussion.
 
Hili kiukweli ni tatizo kubwa sanaa, na bahati mbaya zaidi kuingia kwa uchawa, ambako hakuangalii ujengaji na ujibu wa hoja bali kupayuka na kusifia mambo wanayopenda kuyasikia wanaonawtuma, ndiyo kumekuza tatizo ambalo tayari lilikuwepo.
Kuna jamaa chini hapo anabisha kwamba si sahihi. Yaani sisi wabongo bwana tunakataa hata vitu vya msingi. Na ndio maana hatubadiliki. Once you are clouded by ego or denial, you are automatically limiting your brain from thinking outside the boxes.
 
Siwezi kumwamini mtu anayesema uwongooooo kila siku ,kitila ni mmojawapo
 
And you believe you have strongly made your case?

Eti Watanzania Wengi! Watanzania wengi ni wangapi?
"Humu Jamii Forums" pamoja na Interview ya Waziri Mmoja. ni Watanzania wengi?

Kwa Ushahidi upi huo?
Kwa Utafiti upi huo?
Sasa wewe ushahidi wako uko wapi? Infact hiki ulichoandika hapa ni ushahidi mwingine wa hoja ya mleta uzi. Wewe umetoa any data ku justify kwamba hana strong case?
 
Jitahidi uwe unafanya reasoning. Usiwe kama mbwa koko
Huu ndio mfano halisi wa uwezo wetu wa kujenga hoja. Ninachoweza kusema watu wa namna hii either uwezo wao ni mdogo sana au wametumwa kudiscourage wanajamii wanaotoa michango mizuri. Yaani huyu anawakilisha hao niliowasema kwenye hoja ya msingi, watu wenye uwezo mdogo wa kujenga hoja;mara nyingi wanapenda kumuattach personal mtoa mada na matusi. Kwa kweli jamii yetu inapoteza ustaarabu na uvumilivu wa hoja pinzani kabisa.
 
Sasa wewe ushahidi wako uko wapi? Infact hiki ulichoandika hapa ni ushahidi mwingine wa hoja ya mleta uzi. Wewe umetoa any data ku justify kwamba hana strong case?
Nimejaribu kumpatia maelezo kwamba kuna vitu vingine havihitaji formal statistical research, unaweza kutumia random sampling kumake reasobale and justifiable conclusion. Nakubaliana na mtoa mada mmoja kwamba elimu yetu ni moja ya sababu zilizotufikisha hapa na aina ya majibu haya ni sample moja ya uwezo wetu mdogo wa kujenga hoja.
 
The source of the problem most likely stems from the education system which doesn’t emphasis on critical thinking.

No wonder we keep losing cases in arbitrations.
For so long, education system haitengenezi critical thinkers , inatengeneza wanao kariri, na wanao kariri ndio wanapewa priority.

Result tunapata wasomi wasio na potential, huko dunian wakienda wanaonekana hawana uwezo
 
Absolutely correct!
 
Kiswahi fasaha ni "hebu" sio "Ebu" kama ulivyo tumia kwenye andiko lako.

Tatizo pia linaanzia kwenye matumizi fasaha ya lugha. na hapa namaanisha lugha zote; kiswahili na kizungu.
Sawa boss, ila kwenye hoja nzito kama hii hicho ndicho ulichoambulia tu.
 
Back
Top Bottom