Watanzania wengi wanaamini serikali inateka wakosoaji wake, na wale wakosoaji wasiotekwa huitwa watu wa vitengo

Watanzania wengi wanaamini serikali inateka wakosoaji wake, na wale wakosoaji wasiotekwa huitwa watu wa vitengo

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
Kwema Wakuu!

Nazungumza Kwa uzoefu wàngu binafsi.

Úkiwa mkosoaji wa viongozi wa serikali au serikali Kwa ujumla Bila kujali Nia yako kuwa ni Njema au mbaya, Bila kujali upo Chama gàni au hauna Chama.

Watu kuanzia Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wàtakuambia Bila kificho kuwa unajiingiza kwèñye matatizo Makubwa, yani NI kuwa unakanyaga waya weñye umeme Mkubwa àmbao Kwa hakika utakuangamiza.

Watanzania wanaamini kuwa serikali Yao haihitaji kukosolewa. Watanzania wengi hujua kuwa serikali inateka, kuangamiza, kukuwekea zengwe na kukutia matatizo endapo utakuwa kinyume nayo hasa ukiwa Frontline.

Watanzania wengi huamini kuwa mkosoaji asiyepatwa na panga la serikali Basi atakuwa sehemu ya serikali yàani Mtu wa kitengo.

Ni lini mitazamo hiii ya Watañzania kuhusu serikali yao itaondoka?

Yàani Watañzania wasomi kwa wasiosoma wengi waô huogopa kueleza maoni Yao juu ya serikali
Mfano. Huwezi kukuta mtangazaji wa kipindi cha redio au luninga akiweka Msimamo wake wa kutomkubali labda Rais au Chama kilichopo madarakani. NI ngumu

Au Kiongozi wa Dini au Mwalimu, au Daktari au Mwanamuziki au muigizaji umkute akiwa Huru kujieleza kuihusu serikali. Asilimia kûbwa hushindwa ila wachache Sana ndîo hujieleza Kwa Uhuru.

Je, viongozi u serikali kama serikali inachukuliaje uwèpo wa Jambo hili katika wananchi wake?

Mchana mwema.
 
Back
Top Bottom