Treni ya umeme imeanza safari yake ya kwanza kwenda Morogoro ikitokea Dar. Hili ni jambo la kushukuru na kuipongeza sana Serikali. Tumeona mara nyingi kitu kipya kikianza kwa mbwembwe na kwa huduma nzuri lakini baadaye huduma yake ikidorora kwa kasi kubwa.
Treni ya umeme isifikie huko. Mifano hai ni Usafiri wa mwendo kasi ya hapa Dar. Mwanzoni huduma ilikuwa nzuri sana lakini fika pale leo, vituo vimechakaa, mabus yamechakaa, vyoo havitamaniki. Kwanini?. Mfano wa pili ni Uwanja wa Mkapa. Mwanzoni uwanja ulikuwa super kwa maana ya viti, muonekano, miundo mbinu kama vyoo,n.k.
Leo hii nenda pale. Watazamaji wanavunja viti kwa makusudi, vyoo vya pale havitamaniki. Watu wanajisaidia mpaka kwenye sinki za kunawia mikono. Inatisha. Sasa treni ya umeme imeanza kwa huduma nzuri. Chonde chode Watanzania tutunze treni hii ili idumu kwa muda mrefu.
Pia soma:Mazuri ya treni ya umeme