watanzania wenzangu usikubali kurubuniwa na kulishwa hadaa na chuki dhidi ya katiba pendekezwa

watanzania wenzangu usikubali kurubuniwa na kulishwa hadaa na chuki dhidi ya katiba pendekezwa

singidadodoma

JF-Expert Member
Joined
Nov 11, 2013
Posts
4,394
Reaction score
1,536
Wakati tukielekea katika kura ya maoni inayotarajiwa kufanyika katikati ya mwaka huu kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi. Napenda kuwaasa watanzania wenzangu usikubali kurubuniwa na kulishwa hadaa na chuki dhidi ya katiba pendekezwa.


Kumekuwepo viashiria mbalimbali za watu wenye nia ovu ya kutaka kutugawa watanzania pamoja na kutuvuruga kwa kutumia kura ya maoni, tumeona wameanza kutoa matamko na kauli za kutisha ustawi wa taifa letu wakiwamo wanasiasa wanaotaka kurudi bungeni kwa njia yeyote ile pamoja na viongozi dini.


Watanzania wenzangu tusikubali kurubuniwa na kulazimishwa kwa namna yeyote ile hata kama na viongozi wetu wa dini amabo tumekuwa tukiwaheshimu mno, tusitoe nafasi kwa wahadhifina kuteka huu mchakao kwani watatuladhimisha tufike watakapo wao na si matakwa yetu.


Hatua mbili muhimu zimeshapita ya kwanza ilikuwa ya ukusanyaji wa maoni ambapo tume ilifanya kazi yake bila kuingiliwa na hatua ya pili ni ile ya bunge maalum la katiba amabalo lilikaa na kufanya kazi yake kwa mujibu wa sheria na bunge hilo amabalo lilikusanya watu kutoka kada mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini wanaotoa matamko ya leo kila kukicha.


Jambo la kufurahisha wale waliokuwa wakiikosoa tume ya Warioba ndio hao hao walikuja kuikubali na kuipigia chapuo, na huku wale waliokuja wakiifurahia walikuja kuwa maadui wa tume hiyo, leo hii wanakuja kwetu kutulaghai tuikate katiba pendekezwa kwa kuwa maoni yaliyokuwa katika rasimu ya Walioba wamenyofolewa.


Swali la msingi kwa hawa wahadhifina, ikiwa hawakutaka rasimu ya Warioba ipunguzwe au kuongezwa jambo, kwanini walikubali kuwepo kwa bunge la katiba baada ya Warioba kumaliza klazi yake? Si wangetuletea moja kwamoja wananchi tukaipigia kura?

Watanzania wenzangu tuwapuuze hawa wasioitakia mema nchi yetu, tuisome katiba pendekezwa na kuielewa kisha tuchukue hatu ya kuwashangaza ili waache siasa zao za uhanaharakati.


Watanzania tusiwakubali wanaotishia uhai wa ustawi wa amani ya nchi yetu, watanzania tuna utaratibu wa kujadilana kwa amani na tusikubali kushawishiwa kwa naman yeyote ile jambl lolote baya likitokea waathirika ni sisi hao wanaotushawaishi watakuwa wakwanza kupanda ndege na kukimbia nchi.
 
wahadhifina wanatakiwa kujua kuwa hakuna nchi yeyote duniani amabayo iliandikwa mara moja na ikakidhi matakwa na mahitaji ya raia wote. hata katiba ya Marekani inaelezwa imeshafanyiwa marekebisho kutokana na mahitaji na wakati mara 28 tangu ilipoandikwa mara ya kwanza mwaka 1770.

ikiwahata katiba ya marekani amabo wanajinasibu kaka baba wa demokrasi duniani wanaendelea kufanyia marekebishokatiba yao mpaka sasa, hata katiba pendekezwa itakuja kufanyiwa marekebisho kutokana na mahitaji na nyakati.
 
Wahi chooni unanuka mnooo.... angalia nzi wanavyokufuata!
 
Wahi chooni unanuka mnooo.... angalia nzi wanavyokufuata!

Mpishe sasa apite aelekekee huko mbona wee mwenyewe umekawia kutoka huko???pisha basi! Kumbe mchwa humu kibao kazi kulinda kumbikumbi tu huna unalolifanya isipokuwa kuchafua hali ya hewa huna hoja potea!!
 
mkulimawakiteto kwenye hiyo katiba ya chenge kama kuna kifungu kinakataza watumishi wa umma kuwa na acount nje ya nchi mi nitakuwa wa kwanza kupiga kura ya "NDIO "
 
Last edited by a moderator:
Mawazo yako mazuri lakini yanakinzana kwani kinachotumika na kufanyika ni ubabe wala si kujali mawazo ya wananchi. Hususani katika madaraka ya Rais kufanya uteuzi umepewa nafasi kubwa na unakera kwani wanaoteuliwa huwa hawakidhi vigezo bali undugu, uswaiba na kujuana. Pia ningefurahi zaidi kama Waziri asingetokana na ubunge.
 
mkulimawakiteto kwenye hiyo katiba ya chenge kama kuna kifungu kinakataza watumishi wa umma kuwa na acount nje ya nchi mi nitakuwa wa kwanza kupiga kura ya "NDIO "
Wewe kiazi acha ushamba wako, kasome Katiba Inayopendekezwa IBARA YA 29-(2)(b) au isome Ibara yote kwa faida yako, kwahiyo katiba inaeleza kuwa Bunge itatunga sheria ya kuainisha kwamba ni nani anaruhusiwa kufungua akaunti na nani haruhusiwi na kwa wakati gani wa kufungua hizo akaunti, hivyo msingi wa ufunguzi wa akaunti nje ya nchi uko kwenye katiba hiii, haya lete swali lingine nkujibu maana umekuwa kilaza ana mvivu wa kusoma.
 
Mawazo yako mazuri lakini yanakinzana kwani kinachotumika na kufanyika ni ubabe wala si kujali mawazo ya wananchi. Hususani katika madaraka ya Rais kufanya uteuzi umepewa nafasi kubwa na unakera kwani wanaoteuliwa huwa hawakidhi vigezo bali undugu, uswaiba na kujuana. Pia ningefurahi zaidi kama Waziri asingetokana na ubunge.
WEWE KIJANA NAKUSHAURI KABLA HUJATOA LAWAMA KASOME IBARA YA 81 INAELEZA WAZI WAZI KUHUSU MADARAKA YA RAIS! umeelewa?
 
Back
Top Bottom