Watanzania wote tungekuwa na bidii kama wauza icecream za ukwaju za Bahresa nchi hii ingekuwa zaidi ya US

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Hawa jamaa wametapakaa mitaa yote.

Nimejaribu kuwalinganisha na watafutaji wengine hawa wako aggressive na wanakomaa bila aibu wala kujishuku huku wakiwa na sura zilizojaa ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya asubuhi hata jioni.

Kiufupi hawa jamaa nawakubali sana, na ndio role model wangu wa kukomaa hadi sasa.

Mungu awabariki wakuu. kama una wanajf humu wanasukuma zile icecream za kuwaju wale wanavaa nguo za orenji.

Nawapenda sana.
 
matunduizi,

Ni kweli kabisa mkuu wako vizuri watanzania wote tunge fanya juhudi zile lazima tufikie mafanikio. Kijana acha uvivu chapa kaz usibague kazi wewe humbi kazi, na wala kazi haiumbwi pambana kila kukicha.
 
Yaani hata mie nikiwaona nawaza mengi. Unakuta mtu kavaa kale kabegi amekaweka kwa mbele kifuani, wanatembea juani. Halafu mkaka kama huyo umwambie atume na ya kutolea, unapata dhambi!
Nilipita sokoni juzi kati jamaa anasema hata ukwaju sasa sokoni unapungua watu wanapelekea huko huko. Itafika kipindi kama wakiendelea kukomaa ukwaju utakuwa unapatikana kwa njia ya hizo icecream tu.

Hapo lazima hawa wajasiliamali waanze kupiga pesa zaidi.
 
Wengi wao ni graduate wa udsm.

ILa unaweza kuniambia kwa diamykaramga zimeishia wapi?
Ukimwambia afungue yake aanze kuuza anaamka saa nne asubuhi, ila ukimrudisha kwa Bakhresa saa kumi yuko macho.
Graduate mwisho gatemaji huku wakija lazima wakubali chochote kitakachowezena ili maisha yaende wakati wanasubiria maisha ya waliyosomea kama ikitokea yapo.
 
Watanzania ni mamburura hata ukianzisha biashara ya kuuza mavi watakuja uwaaajili hali kila mmoja ana choo kwao.
Jwisi ya ukwaju tumeanza kunywa zamani sana hapo mnazi mmoja karibu na kituo cha polisi. Leo jitu lenye misuli linatembea na sharubu zake linauza ukwaju eti limeajiliwa, limeshindwa kwenda polini kuokota ukwaju na kuja kugandisha na kuuza. Yameshindwa hata kukopi teknolojia ya kufunga tu. Wauza ukwaju hongeleni sana kwa kuajiliwa.
 
Ni kweli kabisa mkuu wako vizuri watanzania wote tunge fanya juhudi zile lazima tufikie mafanikio. Kijana acha uvivu chapa kaz usibague kazi wewe humbi kazi, na wala kazi haiumbwi pambana kila kukicha.
Wale ulaya wanakatwa makato serikalini, mfano Bima etc.
 
[emoji3][emoji3]sasa tutatoaje jamani
Yaani hata mie nikiwaona nawaza mengi. Unakuta mtu kavaa kale kabegi amekaweka kwa mbele kifuani, wanatembea juani. Halafu mkaka kama huyo umwambie atume na ya kutolea, unapata dhambi!!!
 
Hawa wanapovaa vile vibegi wanalemaa mikono kwa sababu wanatembea kama maroboti vile.
 
Nilimuuliza mmoja kuhusu mfumo was biashara yao akaniambia kuwa wanachukua kwa mali kauli, wakiuza wanarudisha ile fedha ambayo angepaswa kuitoa wakati ananunua ba faida ndio haki yake.

Lazima wakimbizane na upepo kwani ice cream ukilala nayo hugeuka juisi.

How you sell, how you get.
 
matunduizi,

Yaani kila siku nikipanda daladala lazima nikutane nao wamesambaa kila kona.
Na ulivyowaza ww hata nilifikiria hvyohvyo nilifurah sana kuona the way wako very serious.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…