Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,187
Wamasai ni jamii ya Nilo-Hamitic walioingia Afrika Mashariki kutokea eneo la Sudan na Ethiopia. Ni mojawapo ya jamii maarufu za Ki-Nilotes zilizotapakaa katika Afrika Mashariki hasa Kenya na Uganda. Wamasai kama ilivyo kwa Wanilotes ni wafugaji kwa asili na wanaoishi kwa kutegemea nyama, damu na maziwa.
So, ili kujihakikishia malisho na maji, wamekuwa wakihamahama na hivyo kujikuta wakipigana na jamii wanazokutana nazo. Wamasai pamoja na Wataturu (Wadatooga) ndio makabila ya Nilotes yaliyojipenyeza Kusini kabisa hadi kwa Wabantu ambao traditionally ni wakulima na wanaoishi kwa amani.
Kujipenyeza kwa Wamasai na Wataturu katika jamii za wakulima wa kibantu kulisababisha wawe wanavamia jamii za Wabantu mara kwa mara na kupora mifugo yao. Kwa woga wa kuuawa na kuporwa mifugo muda wote, jamii za makabila jirani zilianza kuiga baadhi ya mila za kimasai ikiwemo mavazi ya kimasai. Wasukuma (Wanyantuzu), Wambulu, Wambgwe, Wagorowa, Waalagwa, Warangi, ni baadhi ya walioathirika na hofu dhidi ya Wamasai.
Hata hivyo, Wamasai nao walikuwa na mbabe wao, indeed ni ndugu zao Wataturu (Waberbaig/Wadatooga), walioishi katika eneo linalozunguka Mlima Hanang (Hanang & Mbulu). Wataalamu wanadai kuwa almost kila Wamasai walipopigana na Wataturu, walipigwa mweleka na hivyo kuwafanya Wataturu kuogopeka zaidi na Makabila yanayowazunguka ya Wambulu, Wasukuma, Wanyilamba, Waisanzu, Waiambi, Wanyaturu, Wasandawe, Wahadzabe (Watindiga), Wagorowa (Wafiome), Waalagwa na Warangi.
Sema tu kuwa, Wataturu walikuwa wachache na waki-cover eneo dogo kulinganisha na Wamasai. Kumbukeni Wamasai wanna eneo kubwa kuanzia Kenya na Wamasai walioko Kenya ndio wengi kuliko walioko Tanzania.
Probably kuwa kwao Nairobi, Serengeti, Masai Mara, Ngorongoro, Tsavo, Engaruka, Tarangire, Manyara, Ziwa Natron (Flamingo) kuliwafanya wajulikane sana kidunia kuliko Wataturu.
Nawasilisha wazee.