Watawala tumefanikiwa kudhibiti kipindupindu au uwepo wa Covid unaathiri kutokea kwa kipindupindu?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Kipindi hiki cha December kuelekea January, ni kipindi cha msimu wa maembe, matunda ambayo msimu wake huambatana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.

Hata hivyo, kwa miaka karibu mitatu sasa , sijasikia habari ya mlipuko wa kipindupindu katika maeneo yoyote ya nchi yetu kama ilivyokuwa imezoeleka hasa katika kipindi hiki(kama taarifa hizo zipo, basi mnijuze).

Maswali:
Watanzania tumepiga hatua katika swala zima la usafi na hivyo kudhibiti mlipuko wa kipindupindu?

Au kuna uhusiano baina ya ujio wa Covid na kutokomea kwa kipindupindu? Utafiti unahitajika?

Au ugonjwa upo ila taarifa hazitoki?

Hongereni watanzania.

Mods naomba heading isomeke watanzania na sio watawala
 
Ndo utagundua kwamba watanzania tulikuwa tunakula uchafu (m.A.v.I) sana ndo maana kipindupindu kimesumbua sana miaka ya nyuma. Lkn baada ya uviko19 kuingia watu wakaamasishwa kunawa mikono kwa wingi na hivyo kupunguza tatizo la kula vima.
 
December kuelekea January?aloo unatufanya sisi dagaa
 
Kuna vijiji maji salama ya kunywa ni ndoto, unafikiri ukiyapata utahangaika tena na kuni za kuuachemsha!

Juu ya hayo tunaambiwa tujiajiri katika kilimo, maji ya kunywa ni shida hayo ya kumwagilia mazao sijui tuyatoe wapi.

Tunaishi kwa kudra za Mwenyezr Mungu.
 
Maji Machafu hayasababishi kipindupindu.

Kipindupindu kinasababishwa na mdudu anaitwa E.Coli anayepatikana kwenye mavi.

Mtu akijisaidia, halafu mvua ikanyesha maji yakatirisha kinyesi kwenda kwenye maji halafu hayo maji watu wakanywa tayari kipindupindu kinalipuka.

KILA mtu akiwa na choo na akakitumia, miradi ya sanitation ikifanyika vizuri na watu wakizoea kunawa maji tiririka ( sasa hivi kaya nyingi hata vibuyu chirizi vipo ), hutasikia tena kipindupindu.

Sasa hivi siyo kama zamani, angalau kidogo ndani ya Wizara ya Afya Kuna kitengo cha Kinga na kinapewa nguvu kidogo siyo kama zamani.
 
Unafafanua nilichoandika, kama hakuna maji salama yanayosukumwa kuwafikia wananchi inamaana wananchi hawawezi kuwa na uhakika wa maji ya kunywa yasiyo na maambukizi na hata maji ya kunawa mikono.
 
Kunawa mikono Kwa sabuni Kwa maji tiririka kill muda na kuvaa barakoa kipindupindu kitatokea wapi...
 
Maji Machafu hayasababishi kipindupindu.

Kipindupindu kinasababishwa na mdudu anaitwa E.Coli anayepatikana kwenye mavi.

Mtu akijisaidia, halafu mvua ikanyesha maji yakatirisha kinyesi kwenda kwenye maji halafu hayo maji watu wakanywa tayari kipindupindu kinalipuka.

KILA mtu akiwa na choo na akakitumia, miradi ya sanitation ikifanyika vizuri na watu wakizoea kunawa maji tiririka ( sasa hivi kaya nyingi hata vibuyu chirizi vipo ), hutasikia tena kipindupindu.

Sasa hivi siyo kama zamani, angalau kidogo ndani ya Wizara ya Afya Kuna kitengo cha Kinga na kinapewa nguvu kidogo siyo kama zamani.
E. COLI???? Sayansi ya wapi hii tukiwa kidato kama cjakosea cha pili tulifundishwa ni Vibrio cholerae??
 
Maji Machafu hayasababishi kipindupindu.

Kipindupindu kinasababishwa na mdudu anaitwa E.Coli anayepatikana kwenye mavi.

Mtu akijisaidia, halafu mvua ikanyesha maji yakatirisha kinyesi kwenda kwenye maji halafu hayo maji watu wakanywa tayari kipindupindu kinalipuka.

KILA mtu akiwa na choo na akakitumia, miradi ya sanitation ikifanyika vizuri na watu wakizoea kunawa maji tiririka ( sasa hivi kaya nyingi hata vibuyu chirizi vipo ), hutasikia tena kipindupindu.

Sasa hivi siyo kama zamani, angalau kidogo ndani ya Wizara ya Afya Kuna kitengo cha Kinga na kinapewa nguvu kidogo siyo kama zamani.
Ni kweli usemayo na hata mimi nafahama, ila naona kama changes zimekuwa za ghafla mno na sio za kidogo kidogo na ukizingatia karibu nchi nzima ndio maana nimejiuliza maswali mengi.
 
Back
Top Bottom