SoC01 Watawala, wanasiasa tuhurumieni vijana wenu, msiturithishe jamii zenye maisha ya kikoloni

SoC01 Watawala, wanasiasa tuhurumieni vijana wenu, msiturithishe jamii zenye maisha ya kikoloni

Stories of Change - 2021 Competition
Joined
Jul 22, 2021
Posts
7
Reaction score
5
TUENZI YA WAASISI WETU KWA USTAWI WA JAMII ZETU.

Na Nkurumah wa Karne ya 21.

Ni hudhuni, ni majonzi, ni machozi na taharuki kubwa kwa kijana, mwana wa Afrika Mwenye uzalendo na fikra chanya kwa jamii yake, hakika Kesho haitabiriki.

Wazee wetu waliifia nchi, Uhuru wakiutafuta, babu zetu waliuawa hakika wakoloni waliwatesa ndugu zetu kwa maumivu makali, shingo nyuma ziligegeuzwa, mikufu walifungwa shingoni na kuning'inizwa wakafa kama kwale mtegoni.

Licha ya mzungu kujenga shule bora Sana kama Tabora boys na girls, Bihawana na Saint Mary's na hata Pugu sekendari, babu zetu waliudai Uhuru; licha ya watawala wa wakati huo kujenga reli imara na kujenga vituo vya afya bado wazee wetu waliona amani yao, haki na furaha ilikuwa na thamani kuliko yote hayo na hakika waliudai Uhuru.

Licha ya watawala kuwa na jeshi la kikoloni lenye silaha za Moto, babu zetu walijua hitaji lao ni Uhuru utakaowapa amani, haki na furaha, walijua kukaa kimya hawakuwa salama kwa mkoloni na kupambana naye kungeleta madhara makubwa lakini hata kumng'oa mkoloni wangeweza, hamasa hii iliwaingiza katika mapambano ambayo yalipelekea kuuawa maelfu ya baba, mama na babu na bibi zetu, oooh ni hudhuni Sana.

Watemi wetu (wapinzani) wa wakati huo waliuawa kikatili na wengine kuzeekea magereza.

Mkwawa alinyongwa, Kinjekitile Ngwale aliuawa, Abushir bin Sultani wa Pangani kikatili aliuawa na watawa dhalimu wa kikoloni akiudai Uhuru wa taifa lake.

Isike aliuawa, Milambo alikufa, Bwana Heri wa Uzigua aliuawa, Mtemi Kigole wa Dodoma aliuawa na hata Mwami Tagarara wa ujiji (Kigoma ya Sasa) aliuawa na watawala Hawa.

Mbali na waliokufa, Mandela alizeekea gerezani baada ya kufungwa miaka 27 kwa kesi ya ugaidi uliogezwa jina kutoka katika uzalendo wake kwa nchi yake, Kwame Nkuruma alifungwa miezi sita, Mwl. Nyerere wa Tanzania alihukumiwa gerezani miezi sita baada ya kutoa maneno ya kulaani uonevu uliokuwa ukitendwa na maliwali na maakida (wakuu wa wilaya) kwa wakati huo kupitia gazeti la sauti ya TANU mnamo mwaka 1958 ambapo baadaye alitoa faini ya fedha aliyochangiwa na watanzania, utamaduni wa Watanzania kuchangia haki kwa watetezi wao upo tangu enzi na enzi.

Jomo Kenyatta alihukumiwa kufungwa miezi sita na wakoloni huku wanaharakati kadhaa akiwemo John Biko wa Afrika Kusini wakiuawa kwa kuburuzwa kwa kufungwa minyororo kwenye magari.

Baadaye Afrika, ikianzia Misri 1922 na baadaye Ghana 1957 na baadaye mataifa mengine yote na Tanzania mwaka 1961 ikijipatia Uhuru wake Afrika ilipata tumaini jipya, Watawala wakawa weusi miongoni mwa walionusurika kuuawa na watawala hao wa kikatili (wakoloni)

Huzuni kali, majonzi Mapya yalirejea kwa aina mpya baada ya watawala weusi, wanaojua vema sababu ya watanzania kuukataa utawala wa wazungu na kutaka Uhuru,walipokuja kuanza kutumia nguvu ya ziada kuwarudisha waafrika katika madhila zaidi ya waliyoyapitia katika utawala katili wa wazungu.

Miaka 100 ya Uhuru wa Afrika, mataifa mengi Afrika Leo hii wakosoaji wa serikali wanasota magerezani, mataifa mengi ya Afrika leo wapinzani wa kisiasa wanavunjwa nyonga kwa risasi za Moto mchana kweupe, mataifa mengi ya Afrika leo wanaosema hadharani makosa ya watawala weusi ambao ni ndugu zao wa damu wa, leo wanasota kwa kesi Kali zikiwemo za ugaidi, uchochezi, uhujumu uchumi nk. Za kuchongwa na vibaraka wa watawala ili kudhaifisha ari za watu kuwadhibiti viongozi wanaowachagua wenyewe pindi wanapokosea.

Leo hii hata vijana waliozaliwa baba zao wakiwa Marais hapa Afrika wanalazimishwa kuonja maisha ya kikoloni yaliyowatesa babu zetu, watoto wa Afrika huru tunalazimishwa kuyaonja madhila ya tawala za kikoloni, ni huzuni Sana kwa kijana Mwenye ubongo usio na kutu Bali wasakatonge hawawezi kuliona hili.

Kinachoumiza zaidi ni kwamba watekelezaji wa madhila haya NI vijana na watu wasomi, aidha watumishi wanaoishi kwa Kodi za wananchi wanaowatesa, hawa wanaongozwa na aidha uoga, usakatonge wakidhani kwa kujipendekeza kwa wenye mamlaka za serikali ama vyama ama kwa mabeberu ya Ughaibuni watapata manufaa binafsi na wengine wanafanya haya kwa kukosa maarifa tu, uwezo wao wa kuyatazama maisha ya jamii za watu na mustakhabali wa jamii umeishia hapo. Ni huzuni Sana kwa kijana Mwenye ubongo usio na kutu.

Na katika hili, hakuna nchi ya Afrika leo inayoweza kusimama hadharani ikajikosoa kwa andiko hili, Ni utawala wa Kenye kidogo tangu 2007 na Tanzania kidogo awamu ya nne chini ya Mzee Jakaya Kikwete Maana ya Uhuru walioufia babu zetu ilijaribu kufafanuliwa.

Watawala na wanasiasa wengi wa Afrika huru ya leo wamekuwa wakijitahidi Sana kutafuta maneno matamu, lugha zote tamu na maneno yanayopendwa na jamii kama demokrasia, amani, umoja, mshikamano, haki nk. Huku vitendo vyao ni kinyume Mara kumi zaidi katika yale wanayoyatamka, hali hii imefanya waafrika kuiona siasa kama mchezo mchafu, hali hii imewafanya waafrika kumtafsiri mwanasiasa kama mtu Mwenye maneno mengi ya ushawishi na mwongo Sana, leo hii mtu yeyote asemaye Sana ama anayekosa uaminifu watu wa Afrika humwita mwanasiasa, huu Ni ithibitisho kuwa wanasiasa, watawala wa Afrika huru wameturudisha kwenye enzi za ukoloni na udikteta.

"Jamii ikichagua viongozi ikaacha kuwadhibiti, watu wakaishi kwa kujipendekeza kwa viongozi wake basi jami hiyo itazalisha watawala madikteta" ni maneno aliyowahi kiyatamka Mwl. Nyerere Rais wa Kwanza wa Tanzania huru.

Pengine ni kutokana na jamii kuacha nasaha hizi za wahenga wetu Hawa ndiyo Maana haya yanatupata.

Watawala, wanasiasa tuhurumieni vijana wenu, msiturithishe jamii zenye maisha ya kikoloni.

0689990248
 
Upvote 0
Back
Top Bottom