Watawala wetu wameshindwa hata hili?

Kibunango,
Baba acha kutuvika kamba za shingio mkuu huyu mtu anauliza pengine kama anaweza pata hotel maeneo ya usahilini..
Lini mzungu akajifunza Usafi wa mji kwa kuokota taka kwa mikono mitupu ambayo haina hata gloves?...tena basi hawa wenzetu wana nyenzo za kuokoteza hata vumbi, duh.
Mkuu wangu utanisamehe lakini nadhani propaganda za serikali hii zinatisha na sijawahi ona dunia nzima. Mfano mnalazimisha watu kujiunga na ujenzi wa shule tena huko wilayani kila nyumba ni lazima itoe mtu kisha serikali inatangaza kwa wananchi hao hao walojenga kuwa imeweza kujenga shule kadhaa ktk milaya kadhaa. Hapa unamwambia nani hasa kama mjenzi ni mwananchi mwenyewe?...
Hizi habari za usafi wa mazingira kuhudumiwa na wananchi wenyewe zinatoka wapi haswa? ndio Ujamaa Mambo leo ama, na wakati gani haswa hawa watu wanatakiwa kwenda kazini, huko walikoajiriwa!
Utanisamehe mkuu wangu lugha yangu siku zote huwa nzito nakuomba ipokee kama hoja.
 

Hapa tutarudi kule kule...hatufuati sheria kwa vile ndivyo tulivyo~~~~
 
Mkandara:
Kuhusu hiyo picha, amini usiamini, hapo kuna wadau toka ulaya na afrika. Lengo lilikuwa ni kutembelea CBO na NGO zinazoshughulika na usafi wa mazingira. Katika picha hiyo wadau hao wanaangalia utendaji wa mojawapo ya CBO mjini Mwanza.

Aidha CBO zimetokana na kamati za maendeleo za mitaa ambazo awali zilikuwa zikifanya kazi kwa kujitolea zaidi. Ili shughuli zao ziwe endelevu, ndio zikazaliwa CBO. Kazi za kujitolea mara nyingi hufanyika katika siku za mapumziko.
Jiji la Mwanza kupitia CBO hizo limeweza kuwa Jiji safi kabisa kwa kushika nafasi ya kwanza mara mbili mfululizo.

Usishangae sana kuona watu hao wakifanya kazi bila ya kuwa na PPE(Personal protective equipment)! Wengi wao wanadai kuwa protective gloves na leg and foot protector zina joto sana, hivyo kuwafanya wasiweze kufanya kazi kwa ufanisi. Ukiingia kwenye Ofisi zao, PPE zote katika utunzaji wa mazingira wanazo, lakini hawazitumii.!


Shughuli za kujitolea Jijini Mwanza.




 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…