Watch "Tanzania's BRT system has been running for 3 years" on YouTube

mwenye mada kakimbia, mara ya mwisho alionekana kivukoni ferry, sijui sasa kafikia wapi.
 
Mradi ununuliwe na kampuni binafsi halafu nauli iongezwe 1,000 ili kuongeza ufanisi, hapo ndio mtateleza kwa raha zenu, lakini hili la kutegemea ruzuku ya serikli, mtakwama sana.

Ndio shida nipo hapa UDSM napiga Bachelor of Art in Development studies. Public private partnership ilinivutia kinyama, sema ndio hivyo waafrika hatukubali kuendeshwa na waliochini yetu.

Na matatizo yanaanzia kwenye kupeana connection watu hata hawana determination wanapewa mradi waipige Nchi bora huko Kenya mnajitahidi.

Ila sio kihivyo kuna sehemu viongozi nao wanazingua, acha tu.

Mwendokasi naiona inalipa kichizi
 
Unataka kuniambia mpaka leo hujasafiri hata nchi moja ya ulimwengu wa Kwanza kiasi cha kutoelewa Rush hours zinakuwaje duniani kote?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio kwa style ya kwenu hapo, full pasua kichwa, hivi hujaona hayo hayo mabasi ya BRT watu wakiingilia dirishani.
 
Dogo soma shule Kisha Tafuta hela, Tafuta bilioni 4000Tsh halafu zungumza na Tanroads ujenge Highway toka Dar hadi Arusha, funga tolls watu tukulipe, tukamue vitoyota vyetu masaa matatu hadi arusha,
Unadhani kupata huo mpunga ni Kitu simple huku africa? Waliochini unataka wafanyaje? Serikali inahitaji sana hao wawekezaji but kwa good terms, vinginevyo mtauzwa mstuke nchi yenu imekuwa ya kichoko tu kama Kenya, kumpata mtu aliye tayari kuwekeza kwenye miradi mikubwa sio kitu rahisi, hata walio na mtaji wanahitaji kufikiria na kujihami sana, mradi wa Nairobi Mombasa highway hadi leo politics tupu pamoja na kuwa mwekezaji ni US pesa si shida kwake .
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna circumstances, kunakuwa na Mafuriko au hiyo siku madereva waligoma, but katika hali ya kawaida mradi uko poa sana, na nitatuma mapichapicha wakati wa kurudi ukitaka

Sent using Jamii Forums mobile app

Hizo circumstances mbona kama za kila siku, hivi kando na nyie waimba mapambio MaCCM wa kila siku umeona Mtanzania mwingine humu akisifia? Maana watu wanajua kero wanazokumbana nazo kila siku, mimi nikiwa Dar nilikua nazikwepa maana sikuona haja ya kupata tabu zote hizo. Nilijaribu mara kadhaa kuzitumia nikaishia kero na kukata tamaa.

Ukianzia Kimara maana huko ndio mwisho zinakoanza zikiwa tupu utaenda freshi, ila anza kuzisubiri maeneo ya kati kama Ubungo utakoma ubishi.
 
Kuna circumstances, kunakuwa na Mafuriko au hiyo siku madereva waligoma, but katika hali ya kawaida mradi uko poa sana, na nitatuma mapichapicha wakati wa kurudi ukitaka

Sent using Jamii Forums mobile app
Kiuhalisia mwendokasi kama ilivyo sasa ni kero sana inahitaji maboresho mengi sana, nashukuru mimi kwetu Tabata hayapo lakini nawaonea huruma watu wa Kimara na Mbezi
 
Kwa mfano ipi?
 

Sawa mzee nimekuelewa, nataka uelewe pia private sector haimaanishi wazungu tu tuna waafrika hapa ndani wapo tayari just tenda itangazwe na kuwe na check up zaidi.

Hiyo kozi niliyotaja haiangalii zaidi foreign investment inaangalia effective and efficient utilization of country scarce resources in achieving goals.


Hebu fikiria UDART wakitenga siku maalumu au usiku kwa ajili ya Services ya mabasi ili asubuhi hadi jioni wahakikishe mabasi yote yako on services wanaweza kusaidia kidogo na pia wakiweka wahudumu ndani ambao watajua idadi ya nafasi zilizobaki wawataarifu walio kituoni ili wajue abiria wangapi wanaingia itazuia kubanana hovyo.


I am Tanzanian i believe we have power to change without foreign intervention tatizo ni soft infrastructures, kama zinatukomoa na sio kusaidia.
 
Naongea vitu nilivyoona kwa macho, nilikuwa na foreigners kwenye kituo hapa ubungo terminal, basi lilifika watu washaanza kujaa walipoingia niliwahurumia bado Shekilango, manzese, magomeni, kagera, fire na walikuwa wanaenda kivukoni unadhani wakifika watarudia tena?

Mradi una Matatizo ambayo yatapunguzwa hata kumalizwa kwa menejiment bora na shirikishi pamoja na elimu ya abiria waache mentality ya kubanana pengine iwe shuruti kupanga abiria wanaoingia kupitia kuajiri wahudumu watakaokua kwenye mabasi na kuhesabu nafasi zilizobaki.


Kama basi halina nafasi lipite kituo isipokuwa kama kuna mtu anashuka.

Ni hayo tu, mwendokasi ni mradi bora Tanzania ila hautumiki kama ilivyotakiwa wakati unafunguliwa.

Sorry brother Game Over kama nimekukera.
 

Duh mzee unakaa muhimbili au Morocco?

Maana hizo ndizo ruti za raha.

Jioni saa tisa au kumi nakuomba simama Gerezani panda basi za kimara.


Hatuna ubaya na miradi ila changamoto zinazidi na wahusika chali. Hebu watutatulie asee.


Huwa napanda mina ya saa 4 au sita ndio inakuwa comfortable.


Sorry brother, but mwendokasi ina changamoto.
 
Ndio maana nimekwambia some shule kwa sasa usishuke chini ya GPA ya 3.5, unajua wakati nahitimu digrii ya Kwanza miaka sita iliyopita nilikuwa na nadharia Nyingi kama wewe, huku Mtaani sio kurahisi kama zilivyo ndoto unazoota pale umelala kwenye godoro lako kwenye double dacker ndani ya block flani hapo hostel au ghetto mlilopanga na washkaji mtaani,
Unadhani unaweza mpata mtanzania anaeweza fadhili ujenzi wa Barabara au reli au kinu cha kufua umeme ? Hapa simaanishi mtu binafsi tu, Bali hakuna hata kampuni moja ya mzawa hapa tanzania yenye uwezo huo,
Simaanishi usifikirie nje ya box la hasha bali nakushauri kwa sasa prioritize sana kwenye GPA, yaani ipe 80 ya Muda wako hizo 20% ndio ufikirie hayo mengine,
Lakini nikutie moyo pia, unaonekana una maono.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maisha yangu yote hapa Dar nilipanda mwendo kasi siku moja tu na sitamani tena, nilibanwa mbavu kidogo waniue...
aiseee.....
najaribu kuvuta picha pengine hapo ni asubuhi unaelekea ofisini, umepiga pasi nguo vizuri ukitoka nakupaka kirashi kisha unakutana vurugu sampuli hio ndani ya mwendokasi ambayo umelipia na hata kazi yenyewe bado hujaianza.
nawaza sana yale mangumi, makumbo, mateke, vichwa na tiki-taka uliyopokea kwenye safari hio bila kusahau kunukishwa makwapa na kupakwa majasho ya kila aina.
hapo sasa ukifika kazini unajikuta tu unaumwa na kichwa, na ukirudi nyumbani inabidi ujikande na maji ya moto ndio uweze kutulia.
pole sana kwa yaliyokukuta mkuu.
ipo siku tutafika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…