Watch "The ways Tanzania’s President Dr MAGUFULI shows how to lead an African country" on YouTube

Wazungu wamvulia kofia Magufuli.

Kawadanganye wajinga wenzio. Hakuna mtu mwenye akili timamu atakaetengeneza documentary inayolenga audience ya watumia lugha ya Kiingereza halafu aweke hotuba ya Kiswahili muda mrefu hivyo na asitoe tafsiri ya kinachosemwa.
Msichojua kuwa katika kumpamba huyo mtu wenu ndio mnamuaibisha zaidi.
 
[emoji23][emoji23][emoji23] Kuna ile nyingine, tuzo ya ukombozi Afrika ambayo Jiwe 'alishinda'. Ila meli ya waliokuwa wanasafiri nayo hadi Tz kuja kumkabidhi ilizamia baharini kama ndege ya Malaysia.
 
mlisemaga Trump amkubali jiwe mwisho mkaishia kuwatumbua waandishi wa habari waliopika hiyo taarifa. ni mwendo wa vibweka tu
 
Mkuu hiyo ni software inasoma text document.
Adobe Reader inafanya, na google search engine inafanya au ms windows inayo hiyo tool kwa ajili ya walemavu wa macho au mikono n.k.

Tunampenda Magufuli lakini sio kwa propaganda za kitoto hivyo.
 
Hahahahahahaha, endelea kuumia ila dunia inajua na Tanzania inasonga mbele.
 
Hahahahahahaha, endelea kuumia ila dunia inajua na Tanzania inasonga mbele.

Dunia ipi inayoijua Tanzania? Endeleeni kujitia ujinga na kuuamini usanii wenu wenyewe. Si nyie ndio mlitunga eti Trump kamsifia huyo mtu wenu? Halafu vipi; ile tuzo mliyojitungia ya yeye kuwa kiongozi bora katika kuendesha uchumi mlishampa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…