Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa ameikuza sekta ya comedy Kenya yeye mwenyewe from 'scratch'!Miaka michache iliyopita hakukuwa hata na 'stand up comedians' wala hata comedy show za maana Kenya!Naelewa unachosema,jamaa si m'funny' hata kidogo lakini amewapa vijana wengi sana fursa ya kukuza talanta zao na kutumia talanta zao kujikimu kimaisha.Zile 'auditions' zake za Churchill Show amezitumia kuzunguka nchi nzima na vijana wengi wenye talanta kule vijijini wamepata fursa ya kujikuza ambayo hawangeipata kamwe maishani mwao.Kando na hayo kuna tuhuma nyingi dhidi yake.Nasikia jamaa ni nyang'au kweli!Anawalipa pesa ndogo sana hao vijana wanaovutia watu kwenye show zake huku akijitajirisha na mamilioni ya hela anazookota kwenye show hizo.Wadhamini wa show zake wanamlipa hela nyingi tu ili watangaze biashara zao kwenye show yake!Vijana wake hawafaidi wala kunusia hela hizo!Too sad!Kwani mnapendea mini Churchill?