CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 7,001
- 23,449
Kuna hii kauli ya Mteja ni Mfalme ni moja ya kauli mbaya na ya dharau kwa wafanyabiashara, ni kauli ambayo siiipendi kuisikia hata kuona mtu anaitamka mbele ya macho yangu.
Pesa ni roho inayoambatana na matabia mengi sana nyuma yake,na moja ya tabia za mwenye pesa ni "dharau" hizi dharau zimejaa kwa wateja wengi sana wakiamini kwasababu wameshika Pesa basi bidhaa za wenzao ni taka taka.
leo acha niwambie nyie wateja Mkae mlijue hili kwa ufupi sana.
Hivi umeshawahi kwenda Hardware kutafuta cement ukaingia hardware ya 1 cement hamna (wanakwambia zimeisha) unaenda hardware ya pili (wanakwambia zimeisha pia) Anatokea mtu anakwambia Twende kwenye Hard ware Flani kule cement zipo,kweli unapelekwa unakuta cement ipo.
Hivi kabla hujatoa hiyo pesa yako ushawahi jiuliza maswali kwanini umezunguka hardware zingine zaidi ya 5 umekosa cement??? wakati na wao ni wauzaji wa cement tena wakubwa tu lakini hawana? unafikiri huyo mwenye cement yeye anazitengeneza hizo cement?
Watu wanajitoa hawataki wateja zao mteseke kwa kukosa bidhaaa,huko alipofata cement ukute aliuziwa kwa bei ya juuu lakini akaamua kulipa ili wateja mkija msikose, ukifata cement kuna foleni ya gari sio unaingia tu kiwandani unawekewa cement,magari yanapakia kwa foleni,hivi unajua gharama ya kupambana mpaka gari yako inakaa kwenye foleni kuanza kupakia cement? Tutoke huko..
Umeshawahi kwenda ilala au karume sokoni asubuhi saa 11 au 10 alfajiri ukaona wafanyabiashara wanavyogombania Viatu na Nguo? mimi ni mmoja wa wafanyabiashara ambae nauza viatu vya mtumba,unaweza kwenda karume sokoni kufata viatu vimemwagwa kilaa mtu anachagua kiatu,Bahat mbaya kwenye kuchagua nikashika kiatu cha mguu wa kushoto nimekiona kizuri, sasa inabdi nitafute kiatu cha mguu wa kulia ili pair ikamilike...
wakati natafuta kiatu cha mguu wa kulia kuna mwenzangu pembeni nae kashakidaka kiatu cha mguu wa kulia anatafuta cha mguu wa kushoto,tunakutana uso kwa uso mimi nina cha mguu wa kushoto,yeye ana chamguu wakulia, Namwambia Oyaaaa nipe mguu huo mimi ndio nimewahi kukiona,Jamaaa anakataaa na yeye anasema ndio kawahi,kinachofuata mnajua ni nini nyie wateja?
kama tumekutana wastarabu tunakubaliana mimi nampa hela kidogo ananipa mguu wa kulia,au yeye ananipa hela kidogo mimi nampa mguu wa kushoto,ila kama tumekutana wote tumevurugwa Hiyo siku lazima tushikane shkane vuta nikuvute mwenye nguvu anampokonya mwenzake kiatu... Tutoke huko
Umeshawahi kwenda kariakoo j3 ukaona wale madogo wanaonunua CD wakauze namna wanazigombania zile CD as if wanapewa bure,msukumano wake na mvutano wake ukiwaangalia unaweza hisi zile CD wanapewa bure hawatoi hela, Tutoke huko
Wauza magenge mitaani hivi umeshawahi kuwakuta wakiwa sokoni wanakusanya mzigo wa gengeni namna wanahangaika, ni mara ngapi unaenda gengeni kununua nyanya unakosa karoti? genge la kwanza karoti hamna,la pili karoti hamna, unaenda genge la 4 unakuta ana karoti Hivi unajua imekuaje wenzake hawana karoti halafu yeye anazo,unahisi ana shamba la karoti nyumban kwake nn? Wateja muwe mnajiuliza hayo maswali... Tutoke huko
Hivi mnajua kasheshe za kutoa mzigo pale bandarini? Mpaka kontena lako linafikiwa hivi mtiti wake mnahisi unakuaga automaticaly eeeh? watu wanapigana/wanagombana/wanashushiana heshima/wanalogana/wanauana, nk nk
Mifano ni mingi,unapoenda mahali kununua kitu acheni ujuaji mwingi, Ukitajiwa bei Lipia kama unaona kubwa omba kistarabu upunguziwe usipoeleweka ondoka kistarabu acha kujitia unajua sana bei za bidhaaa kama unamiliki kiwanda cha sukari...
Mteja anakuja dukani unamwambia karibu,Hakujibu kitu unamuacha ashangae unakaa zako chini maana umechoka na mihangaiko,Unamskia bila aibu "we kijana huoni naangalia vitu si usimame" sasa mimi nisimame ili iweje? umetaka nini ukaacha kutolewa? wateja madharau muache Pesa zenu hazina thamani ya nguvu na utu tunaojitoa na kuupoteza kupata hizo bidhaaa mnazoziona zimekaa kwenye mashelf...
Ukija ofisini kwangu Ufalme unaishia huko kwenu,ukiingia ofisini kwangu "we are all equal" Tuheshimiane, pesa yako ingekua na thamani sana ungeikaaanga uinywe na chai, ungeikoroga uinywe uji, lakini ili ujue hiyo pesa yako si kitu haiwezi fanya yote hayo ndio mana umeileta kwangu tubadilishane,sasa usijione kwamba unachonipa kina Thamani kuliko ninachokupa Mimi.
Hiyo sukari ninayokupimia,gas ninayokuuzia,kiatu ninachokuuzia,chakula ninachokuuzia kina Utu wangu ndani yake,nimetukanwa sana kwa ajili ya hiyo bidhaaa,nimepigana sana kwa ajili ya hiyo bidhaa,nimedhalilishwa so Wateja jaribuni kuheshimu tena heshima yenu itoke ndani ya moyo msi force maana wafanyabiashara wanajitoa kuliko hata haya niliyoyaelezea hapa.
Muuzaji na Mteja wote ni sawa
Muuzaji na Mteja wote ni wafalme
Dharau ziache kwako/kwenu ukienda ofisi za watu fata taratibu/kanuni/sheria zilizowekwa hudumiwa sepa zako.