Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Watendaji wa kata, vijiji au mitaa wametakiwa kuacha tabia ya kuwakamata watuhumiwa na kuwaweka ndani saa 24 ikielezwa kuwa hawana mamlaka kisheria.
Kauli hiyo imetolewa na Mkufunzi wa Elimu ya Uraia na Utawala Bora kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, Iddah John wakati akitoa ufafanuzi wa swali lililoulizwa na Mtendaji wa Kata wa Misungwi, Vicent Wana ambaye aliomba kupata ufafanuzi wa sheria inayowapa mamlaka watendaji kuruhusiwa kumkamata na kumweka ndani mtuhumiwa ndani ya saa 24.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akiunga mkono hoja hiyo Afisa Tawala Mwandamizi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Mashaka Makuka amewataka watendaji kuacha tabia hiyo huku akisisitiza kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo husika vyenye mamlaka ya kukamata na kuweka ndani.
CHANZO: Jambo TV