Tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kumekuwa na ripoti za kuenguliwa kwa wagombea, hususan wa upinzani, na wanaotekeleza hayo ni ninyi watendaji wa mitaa. Naomba kuwaasa ndugu zangu, epukaneni na mtego huu.
Kumbukeni kuwa wale wanaowaagiza mfanye hivyo wana ulinzi masaa 24. Wanalindwa kikamilifu, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi na hata baada ya uchaguzi.
Ninawaona kama mmetolewa kafara kwa manufaa ya watu wengine.
Igeni mfano wa watendaji kadhaa huku kwetu ambao wamekataa katakata kufanya hujuma hizo na wamesema wako tayari kufukuzwa kazi kwa ajili ya msimamo huo. Huku kwetu, hakuna mtu hata mmoja aliyeenguliwa.
Nawatakia majukumu mema.