Watengeneza Maudhui wa Tanzania wanatumia vibaya taarifa za watu, TCRA isaidie hili

Watengeneza Maudhui wa Tanzania wanatumia vibaya taarifa za watu, TCRA isaidie hili

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Kuna vijana wengi wanatengeneza maudhui ili kujipatia umaarufu au fedha mtandaoni. Hii sio shida, shida inakuja pale ambapo unatumia sura ya mtu bila kuwa na idhini yake. Tulishazungumzia hili kwa ma-mc wanachukua watu video na kuweka kwenye page zao, ambazo video hizo zinakuwa zinatweza utu wa mtu huyo ili tu MC apate umaarufu.

Kitu kama hicho kinatokea kwa vijana wengine ambao wapo kwa jina la uchekeshaji, mathalani kijana mmoja huwa anaenda vyuoni na kuhoji watu, tena zaidi anahoji wanawake. Kuna video unakuta wale mabinti wanaficha sura zao, au pia hawataki kuzungumza chochote na mtengeneza maudhui huyo lakini bado baadae anapost vitu hivyo. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za faragha za watu na uhuru binafsi.

Najua watu wengi kwa sasa wanaogopa kucheza mziki kwenye mashere kwa kuwa wanajua watapigwa picha na kutumiwa na ma-MC. Kitu kama hicho pia kipo kwa hawa wachekeshaji wanaotumia upuuzi unaoitwa pranks.

Naomba niwataarifu wadau wanaofanyiwa unyanyasaji huu kuwa, sheria ipo na kanuni zimeshatunga, ni muhumi kuanza kuwa-sue hawa watu wanaoleta ujinga kwenye faragha za watu. Aidha, kama ambavyo serikali imekuwa msatari wa mbele kuhakikisha raia wako salama, ni muhimu TCRA kuwafundisha watengeneza maudhui kuheshimu faragha za watu.
 
Kitu kama hicho kinatokea kwa vijana wengine ambao wapo kwa jina la uchekeshaji, mathalani kijana mmoja huwa anaenda vyuoni na kuhoji watu, tena zaidi anahoji wanawake. Kuna video unakuta wale mabinti wanaficha sura zao, au pia hawataki kuzungumza chochote na mtengeneza maudhui huyo lakini bado baadae anapost vitu hivyo. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za faragha za watu na uhuru binafsi.
Kama ni Kiredio, yule dogo kila kitu anachotoa kipo staged. Niko sure 100% na nimeshuhudia video zake nyingi sana na baadhi nimehusika katika post.
 
Kama ni Kiredio, yule dogo kila kitu anachotoa kipo staged. Niko sure 100% na nimeshuhudia video zake nyingi sana na baadhi nimehusika katika post.
Awe wa kwanza kushtakiwa, ajifunze kwamba mtu akikataa hatakiwi kupost
 
Back
Top Bottom