Watengeneza maudhui ya kimtandao walia na Kodi mpya

Watengeneza maudhui ya kimtandao walia na Kodi mpya

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Mtandao.jpeg

Sheria mpya inayoweka kodi ya 15% kwenye mapato ya watengeza maudhui mtandaoni yaanza kufanya kazi Kenya, lakini haijapokelewa vizuri na vijana ambao wengi ndio watengeza maudhui ya mtandao. Rais Ruto alipitisha sheria hiyo Julai.

"Nadhani wanapaswa kupitia upya Sheria ya Fedha kwa sababu watu wengi wataumia, haswa watengeneza maudhui, na itakuwa ngumu kwetu kupata kazi ambazo zitakidhi mahitaji yetu," alisema Samantha Dedra, mtengeneza maudhui mwenye zaidi ya wafuasi 800,000 TikTok, akizungumza na DW.

Watengeneza maudhui wamesema kodi hii inaongeza mzigo mwingine kifedha.

"Serikali haifanyi sawa kutoza kodi ubunifu wa mtu. Sababu unapoanza, unanunua vifaa kutoka kwenye akiba yako, unajarikbu kutengeza stori ukitumia jukwaa lako mwenyewe," alisema Dedra. "Kisha unatozwa kodi, kwasababu tu serikali inaona kama fursa ya kupata pesa zaidi."

Mtengeneza maudhui wa TikTok, Diana Nikita, anakubaliana na hilo pia akisema, "Kenya hatuna ajira. Hata kutoka nje na kutengeneza maudhui unahitaji pesa. Kwa hivyo, siamini wanafanya haki na kwa sasa kila kitu kinatozwa kodi nchini Kenya."

Wakati janga la COVID-19 lilipoikumba dunia, idadi ya watengeneza maudhui kwenye majukwaa kama Instagram, TikTok, na YouTube ilianza kuongezeka kote Afrika, vijana wengi Kenya wamechangamkia majukwaa haya kuuza bidhaa na kujipatia kipato.

DW
 
Nchi za Kiafrika bhana. Wao wanaona ukiwa na channel Youtube, blog au una account kwenye mitandao ya kijamii basi unaingiza hela.
Ruto nchi imemshinda
 
Kazi kwelikweli, badala ya kuwapa watu unafuu wanaongeza mzigo
Hapa Tanzania ilipokuwepo kipindi cha Mwendazake. Ikatolewa
Hakuna kazi ngumu km kutengeneza pesa mtandaoni. Youtube yenyewe kufikisha Subscribers 1000 na watch Hours 4000 ni kazi ngumu.
Cha kusikitisha bando za internet kila siku zinabadilika na kuwa ghari zaidi. Kwa 2Gb unainunua kwa hela za kitanzania 4200. Wakati zamani ilikuwa kwa 1,000 tu.
 
Back
Top Bottom