Watengeneza maudhui yahusuyo bidhaa za vyakula waonywa kutengeneza au kusambaza maudhui yanayoweza kuathiri afya za watu

Watengeneza maudhui yahusuyo bidhaa za vyakula waonywa kutengeneza au kusambaza maudhui yanayoweza kuathiri afya za watu

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
TAARIFA KWA WATENGENEZAJI WA MAUDHUI MITANDAONI (SOCIAL MEDIA CONTENT CREATORS) YANAYOHUSU BIDHAA ZA CHAKULA

Dar es Salaam, 08 Januari, 2025
Hivi karibuni, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limebaini uwepo wa mwenendo wa baadhi ya watengeneza maudhui kutengeneza na kusambaza picha mjongeo (video) katika mitandao ya kijamii zinazoonesha maudhui potofu yahusuyo bidhaa za chakula ikiwemo juisi inayoandaliwa kwa kukanyagwa kwa miguu.

Kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Sura 130 na Kanuni zake, hairuhusiwi kwa mtu yeyote kutengeneza, kuandaa, kusambaza, kuuza na kutangaza bidhaa ambazo zinaweza kuathiri afya ya mtumiaji pamoja na maudhui ambayo yanapotosha watumiaji.

Aidha, hairuhusiwi kutangaza au kuuza bidhaa za chakula katika maeneo ambayo hayajasajiliwa na TBS.

TBS inashirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha wahusika wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja kwa namba
0800110827.

Imetolewa na;
Đaul
Deborah C. Haule
Kaimu Meneja wa Uhusiano na Masoko


Video ya mtengeneza juisi iliyozua taharuki mtandaoni
 
Kuna fufunu kuhusu bidhaa za Mo kuwa na viwango hafifu,wenye kujua zaidi naomba kujua kama ni kweli au laa.
 
Back
Top Bottom