KASHIFA YA WATERGATE (WATERGATE SCANDAL)
Wakati kashifa hii inagonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari duniani miaka ya sabini hapa bongo sisi tulikuwa tunaisoma sana katika gazeti la Newsweek gazeti hili lilikuwa linatoka Marekani kila week na ndege ya shirika la ndege la marekani la TWA ( Trans world Airline) na lilikuwa linauzwa sh 7.
Ilikuwa na very interesting (thrilling) kuisoma ikianza huachi.
Kwa kifupi sana kashifa hii ilitokana na uchaguzi wa urais wa Marekani mwaka 1972. Mgombea wa chama cha republican alikuwa ni rais aliyekuwa madarakani bwana Richard Nixson. Chama cha republican kilikuwa kina dalili ya kushindwa kutokana na kukosa imani nacho kwa wanainchi wa Marekani hasa kushindwa kwa marekani katika katika vita vya Vietnam zote mbili Hanoi na Saigon. Kutokana na sababu hiyo republican ilipunguwa kabisa mvuto kwa maana wakati wanashindwa wanakimbia wenyewe ndio walikuwa madarakani. Vita ya Vietnam na Marekani ilikuwa miaka ya sitini mwishoni kwa hapa Tanzania ilikuwa inatangazwa katika taarifa ya habari ya RTD saa mbili, nakumbuka kuna siku taarifa ya habari hiyo ilitangaza mambo mawili tu ikaisha nayo ni Azimio la Arusha na Vita ya Vietnam.
Republican haikuwa tayari kabisa kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo walifanya kila mbinu washinde, hizo mbinu ndizo zilizaa kashifa ya Watergate.
Watergate yenyewe ni hotel ya kifahari iko ufukweni kabisa mwa bahari katika jiji la Washington, mahari hapo ndipo walipokuwa wanafanya mikutano ya kimbinu ya chama pinzani cha democratic, sasa nimesema chama tawala cha republican hakikuwa teyari kushindwa uchaguzi huo kwa hiyo basi walifanya kila mbinu ili washinde moja wapo ya mbinu hizo ni kujua democratic walikuwa wanajadili mbinu gani za ushindi katika ukumbi wa mkutano wa hotel ya Watergate? Walichofanya walipeleka watu wao wakatege kanda za kunasa mazungumzo ya wapinzani wao ndani ya mikutano ili wazijue mbinu zao pia kunasa mawasiliyano yao ya simu. Kwa hili walifanikiwa ila Democratic walianza kushangaa kwa nini kila wanachopanga Republican wanajua na wanatekeleza kila walichoazimia?
Kwa bahati mbaya vyombo walivyotega viliacha kufanya kazi inakisiwa kuwa chama cha Democratic kiligundua mtego huo kikategua na wakaweka na wenyewe mtego. Sasa si ma ba-burglary (kama wezi) wakarudi tena Watergare hotel kutengeneza hiyo hitilafu ili mawasiliano yawafikie tena repulican, ni kama unaenda kuiba mwenyewe anakuona, Democratic wakapiga simu polisi wale jamaa walikamatwa red-handed wakifanya hiyo kazi.
Kwa kifupi hicho ndicho chanzo cha kashifa yenyewe, ofcourse republican walishinda ila democratic walifungua kesi ya udukuzi kwa kutumia private investigator waliwabana vilivyo republican kwa kutumia kanda walizozinasa na zingine zilikuwa teyari ziko kwenye chama tawala ambapo mahakama iliamuru kiongozi wao Richard Nixson azitoe kama ushahidi , alikataa kwani kwa kufanya hivyo ni kama unapeleka kidhibiti Polisi.
Kwa sheria za Marekani alibidi Rais Nixson ajihudhuru ili ashitakiwe mahakamani kwa kashifa hiyo. Rais Nixson alijihudhuru kwa kashfa hiyo ya Watergate mwaka 74 na Makamo wake bwana Gerad Ford aliendeleza urais wake na akamsamehe rais wake asishitakiwe mahakamani.
Hii ni kwa kifupi sana.
Ebaeban
Tel.Aviv