Wildlifer
JF-Expert Member
- May 12, 2021
- 1,884
- 5,235
Mwaka 2008, nakumbuka nilisafiri kwenda huko Mpanda. Sasa basi tulilopanda, lilichelewa sana kuondoka. Abiria tulianza lalamika. Kondakta wa basi akatujibu 'kwanza hampaswi kulalamika, inabidi mumshukuru sana huyu Ali, maana amewasaidia sana kwa kuweka basi kwenye njia hii'. Kauli ile ilinikera sana, sababu huyo tajiri, habebi abiria bure, tunalipa nauli. Yeye anapata faida. Maana yake ameona sisi wasafiri na njia ile ni fursa. Hivyo, ni win win situation! Hatupi huduma. Nimemkumbuka kondakta huyu, baada ya kufuatilia Issue ya Manara.
Mjadala unaondelea dhidi ya Manara Vs Mo, watetezi wa Mo wanamjengea taswira kuwa ni mtu aliyejitolea kwa simba, ni mtu aliyetoa hela yake, na ameikoa Simba. Ni kama vile ameifanyia Hisani. Mimi siko upande wa Manara wala Mo, Sababu sijui mkweli nani. Ila hoja yangu, ni kuwataka mashabiki wa simba watetezi wa Mo, kuacha fikra za watu 'waliolewa dhiki ya maisha'. Ukilewa dhiki ya maisha, chochote kinachokuja maishani mwako, utaona hisani.
Simba ni klabu kongwe barani afrika. Ni klabu yenye mamilioni ya mashabiki. Hata mtoto anayezaliwa leo, lazima atakuwa na upande mmoja wa simba au yanga. Simba na Yanga, ni utambulisho wa Utanzania. Hivyo timu hizi ni bidhaa ambayo hata Sheikh Mansour anaweza itolea macho. Mtaji mkubwa wa Simba ni mashabiki, wafuasi, wanazi na wakereketwa. Hii ni hela. Ndio maana Mo, hakwenda Coastal Union au Pamba ya Mwanza, au kukomaa na African Lyon yake, au Singida United ya kwao Singida, anajua Simba (& Yanga) inacho ambacho Timu zote za Tanzania hazina; inacho ambacho matajiri wote wa Mpira wanakitaka. FAN BASE. Hivyo, Simba ni bidhaa ambayo haihitaji kubembeleza au kutukuza mtu! Ni Almasi Nyeusi. Hata Mo asingekuwepo, wawekezaji kwa Simba hawakosekani.
Kitu alicho nacho Mo (na alikuwa nacho Manji) wanajua kucheza na akili za mashabiki. Wanajua shida ya mashabiki wa Simba na Yanga. Wanajua ni wakereketwa wa Timu hizi. Wanajua matatizo ya miaka mingi ya timu hizi ni fedha. Wanajua ni watu wa kulewa mafanikio madogo madogo. Wanajua mkiishia Robo fainali ya CAF mnaridhika. Wanajua mkiifunga Yanga, mmeridhika kuliko Kuchukua Kombe. Wanajua mkiifunga Al Ahly ni kama mmetwaa Kombe la Shirikisho. Wanajua tuna fikra kama ya watu wenye lindi la umaskini. Hata anayekupa msaada wa pipi, huyo ni kama Masiah.
Tuache Ushamba, Simba na Yanga ni bidhaa za thamani sana. Na Mo anaihitaji Simba kuliko Simba inavyomuhitaji Mo.
Sent from my Infinix X688B using JamiiForums mobile app