mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,670
Kila kukicha hotuba za Rais SSH kwenye mikutano na dhifa mbalimbali zinaakisi kauli yake Mimi ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo inatuma ujumbe mzito kwa wateule wake kwamba wasithubutu kumdharau kwa kwa sababu ya jinsi yake. Hoja yangu hii inathibitishwa na maagizo anayoyatoa wakati wa kuapishwa kwa wateule wake.
Kwa mfano, leo hotuba yake baada ya kuapishwa kwa Makatibu Tawala, ambao kimsingi ndio watendaji wakuu wa Serikali Kuu mikoani, ni ya maagizo na maonyo makali. Amewambia, bila kupepesa macho, baada ya kuwasimamisha mmoja mmoja na Wakuu wa Mikoa, kuwa atawapima kwa matokeo ya usimamizi wao katika masuala yote kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Wateule wake, naamini wamemwelewa, wasisubiri vitanzi walivyofungwa shingoni vitumike kama vilivyokusudiwa. Tuwatakie kila la kheri.