Wateule wa Rais JK bunge maalum la katiba waanza kumtusi

Wateule wa Rais JK bunge maalum la katiba waanza kumtusi

kidanha

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
188
Reaction score
14
JANA watanzania pamoja na dunia nzima iliona
jinsi ambavyo,mchakato wa kumtafuta Mwenyekiti
wa muda katika Bunge maalum ya katiba
mpya,ikiwa ni kikao cha kwanza,tangu mchakato
wa Tanzania kutafuta katiba mpya
ulipoanza,ikifuatiwa na uteuzi wa Rais Kikwete
wa wajumbe walioungana na wabunge wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na
wajumbe kutoka Baraza la Wawakilishi kutoka
Visiwani Zanzibar.
Zoezi la kumtafuta Mwenyekiti wa muda wa
bunge hilo maalum ilifanyika katika mazingira
ambayo watanzania hawakuyategemea,huku
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amier
Kificho akichaguliwa kwa jumla ya kura
393,kutokana na mihemuko iliyogubikwa na
mbwembwe,ushamba na utovu wa maadili kutoka
kwa baadhi ya wajumbe hao, huku kundi lililo
ongoza kwa utovu wa nidhamu ni lile kundi la
wajumbe kutoka baraza la wawakilishi Zanzibar
pamoja na baadhi ya wajumbe walioteuliwa na
Rais Kikwete.
Moja ya mizaha na tharau zilizofanywa
na wajube hao ni kitendo cha mjumbe
wa bunge hilo,Mussa Kombo Khaji
kutoka Baraza la wawakilishi Zanzibar,
kuumuliza mgombea wa nafasi ya
mwenyekiti wa muda Pandu Ameir
Kificho kwamba, "Mh Pandu Kificho
umekuwa kiongozi wangu wa muda
mrefu kwenye Baraza la wawakilishi,
leo unagombea uenyekiti wa muda wa
Bunge la Katiba"Je nikikuchagua
utafurahi?"
Hii inaonyesha ni jinsi gani mjumbe
huyu hakustahili kuingia katika bunge
hilo,ambalo lina ajenda za kitaifa kwa
mstakabali wa vizazi vya miaka 50 ama
100 ijayo, hii inaonyesha ni jinsi gani
mjumbe huyu amejiandaa kupokea
posho za tsh 300,000 kwa siku ambazo
ni fedha zinazotokana na kodi za
wananchi tena wale wanaoishi chini
ya dola 1 kwa siku.
Hicho ni sehemu tu ya kituko kilichotokea wakati
wa maswali kwa wagombea, waliokuwa wakiwania
nafasi ya uenyekiti wa muda,kituko kingine
kilitokea wakati wa kura kuhesabiwa,ambapo kura
zilizo hesabiwa zilikuwa ni nyingi kuliko idadi ya
wapiga kura walioandikishwa, hii ilionyesha
namna ambavyo zoezi la kura inavyo
chakachuliwa wakati wa chaguzi mbalimbali za
ndani ya nchi hususan chaguzi za ubunge
udiwani na urais.
Kabla ya kura kupigwa ndani ya ukumbi wa
bunge kulikuwa na wajumbe 548,lakini kura
zilizo hesabiwa zikawa kura 568 ikiwa ni
ongezeko la kura 20,swali la kujiuliza hapa ni
kwamba, kura zilizozidi zilitoka wapi? hata hivyo
kulikuwa na majibu mepesi na kihorera horera
kutoka kwa baadhi ya wajumbe hao
kwamba,mlango ulikuwa wazi na kwamba kuna
watu waliingia na kuendelea na zoezi hilo bila
kuhesabiwa.
Yawezekana majibu hayo yalikuwa sahihi, lakini
kutoka na jinsi yalivyokuwa yakitolewa bila
mpangilio, ilimfanya Mwenyekiti wa zoezi hilo
Oliva Luena kuchanganyikiwa huku akizidiwa na
mihemuko ya wabunge hao, hata hivyo swali la
msingi hapa ni kwamba, kwani wajumbe hao
hawakujua taratibu za upigaji kura? ambao uko
wazi kwamba kama hauku andikishwa ama
kuhesabiwa kabla ya zoezi la kupiga kura kuanza
hauruhusiwi kupiga kura?.
Swali lingine ambalo lilikosa majibu
ndani ya ukumbi huo ni kwamba,
kama wajumbe hao walifika ukumbini
na kukuta zoezi la kupiga kura
inaendelea je kalatasi za kupigia kura
walitoa wapi?, wakati kila mtu alikuwa
na karatasi lake tayari?.
Tukio hilo lilikuwa ni fedheha kwa
watanzania waliopewa nafasi chache
kutoka katikati ya watanzania zaidi ya
milioni 44, yawezekana wahusika
walipanga kupiga kura mbili ama
walichukuliana karatasi za kupigia
kura, ili mgombea wanao mtaka aweze
kupita kwa kura nyingi, bila kujali
kwamba kufanya hivyo ni makosa,nani
ishara ya wizi wa kura.
Ukiachilia mbali kituko hicho ambacho
kinaweza kutafasiriwa kwamba ni ushamba ama
udhaifu wa fikra za wajumbe, ambao wengi wao
ni wale walioteuliwa na Rais Kikwete kutoka
katika taasisi mbalimbali,tukio lingine lilitokea
baada ya Mwenyekiti Luena kuamuru kwamba
kura zirudiwe, hapa ndipo sura kamili ya aina ya
wajumbe ambao tunatarajia watuletee
mapendekezo ya katiba nzuri ilipoanza
kuonekana rasmi, baadhi ya wajumbe ambao
ndiyo walionekana kuwa wengi na wenye
mitizamo finyo waliposhindwa hata kuheshimu
kiti cha Mwenyekiti wao ni wale kutoka Baraza la
wawakilishi visiwani Zanzibar pamoja na wataule
wa Rais Kikwete.
Mwenyekiti wa Bunge hilo Oliva Luena alikumbwa
na wakati mgumu wa kuliongoza bunge hilo,
lenye wajumbe zaidi ya 548,katika mchakato wa
kumtafuta mwenyekiti wa muda,hali ilikuwa tete
ndani ya ukumbi huo wa bunge, baada ya kura
kuharibika kutokana na wajumbe zaidi 15
kuongezeka, badala ya wajumbe 548 waliokuwepo
wakati wa zoezi la kupiga kura, sasa kama
mchakato wa mwenyekiti wa muda tu mambo
yamekuwa hivi, vipi kuhusu mchakato wa
mwenyekiti wa kudumu? na Je vipi kuhusu sakata
la mjadala kamili wa katiba hiyo si tutaona
vituko vingi zaidi?.
Katika zoezi hili bila ya Mwenyekiti wa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
Freeman Mbowe, kutumia busara na hekma
iliyojaa maadili ya uongozi hali ingekuwa hatari
zaidi, Wajumbe hao waliokuwa wakizungumza
bila kufuata utaratibu kwa kutoa hoja dhaifu,
huku wakishindwa kumsikiliza Mwenyekiti wao
Luena, kutokana na kile walichodai kwamba kura
zilizozidi ziondolewe,huku wengine wakidai
kwamba kila mjumbe ahesabiwe kwa mtindo wa
namba moja hadi mwisho yaani kila mmoja
asema namba moja hadi wa mwisho na mwingine
akisema kwamba kila mtu asimame nyuma ya
mgombea anayemtaka.
Hata hivyo hali hiyo ilimfanya Mbowe asimame
na kuzungumza kwa hekma na busara huku
akimtaka Mwenyekiti huyo kufuata ushauri wake,
ambapo alisema kwamba, "Mwenyekiti naomba
utumie hekma kurudia zoezi la kura kupigwa
upya", kauli ambayo ilipingwa na baadhi ya
wajumbe.
Mbali na kupingwa vikali na baadhi ya wajumbe
waliokuwa ndani ya ukumbi huo wa bunge, huku
mjumbe mmoja akizungumza ovyo na kusema
kwamba kila mmoja asimame nyuma ya mgombea
anayempenda ndipo wahesabiwe badala ya kura
kurudiwa upya.
Pamoja na wajumbe hao kushindwa kuzingatia
hata heshma ya kiti aliyokalia mwenyekiti Oliva
Luena kuwapa nafasi, Mbowe bado hakutaka
kutumia jazba badala yake akaendelea kusisitiza
kwa kauli ya upole,hekma na busara kumuomba
mwenyekiti huyo kukubali ushauri wake wa kura
kurudiwa.
Mbowe alisema,"Mwenyekiti mimi nina mambo
matatu ya kukushauri katika zoezi hili, moja
milango yote ifungwe ili watu wasiokuwepo huku
ndani wasiingie kuvuruga uchaguzi huu,pili
wajumbe wote wakae chini,tatu karatasi za
kupigia kura,zigawiwe kwa kila mjumbe kwa
kupelekewa kwenye kiti chache, kwani kwakufanya
hivi tutakuwa tumekwepa historia mbaya ya kura
kurudiwa ndani ya nchi hii".Hatimaye Mwenyekiti
wa bunge la mpito Oliva Luena, alikubaliana na
ushauri huo na kuamuru zoezi la upigaji kura
urudiwe. Wagombea waliokuwa wakipigiwa kura
ni pamoja na Pandu Ameir Kificho ,Magdalena
Lubangila,Professa Coaster Rick Mahalu.
Kama wajumbe hawa hawatajirekebisha na
kuacha kufanyakazi kwa mihemuko ya kisiasa na
kuweka itikadi za taasisi zao pembeni,lakini pia
wasipo zingatia kwamba wako Dodoma kwa kodi
za wakulima na wamachinga, ambao kila siku
wanapigwa mabomu kila wanapotafuta mahali pa
kufanyia bishara, pamoja na wafanyabiashara
wanaopigwa mabomu kwa kugomea kodi kubwa
wanaokatwa katika manunuzi za mashine za EFD
hatuta pata katiba ambayo tunaitarajia.
Ingawa ni mapema kuanza kumrushia lawama
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete, kwa uteuzi mbovu wa wajumbe
alioufanya,lakini pia naliona suala hilo kama tusi
kwa Rais wetu, wajumbe hao wameanza kumtusi
Rais wetu matusi na kejeri, kutokana na mambo
waliyoanza kuyafanya, siku zote uteuzi wa Rais
huwa ni uteuzi wa heshma na burasa zaidi,kuliko
hata uteuzi unaofanywa na wananchi ama
vikundi vya watu.
Habarimpya.com pamoja na watanzania wote
kwa ujumla, tulitegemea kwamba wajumbe hao
wangekuwa ni mfano wa kuigwa na kutoa tofauti
kati yao na wabunge,ambao kila siku hufanya
kazi kisiasa zaidi, ili kuwafurahisha wapigakura
wao,lakini katika hili hali imeanza kuwa tofauti
kiasi ambapo wabunge hao ndiyo wameanza
kuonyesha busara kuliko wateule wa Rais
Kikwete.

NI KAWAIDA YA CCM KUDHARAU VITU VINAVYOWAGUSA WANANCHI
 
tulisema rais atatuletea wajumbe washabiki pamoja na michoko kama huyu mwenye mapengo ya meno kama kingunge ngombare mwiru.
 
Kama watu walikubali mchakato huu pamoja na madudu yote ambayo tulisema yapo katika mfumo wake; hamna jinsi sasa bali kukubali tu na matokeo yake..
 
Hakuna jipya...Tusipoteze muda, sisi tunaojielewa tujipange kisha 2015 tufanye kile ambacho kitakuja kusifiwa na vizazi vyetu vijavyo...
 
mimi nilitazama mchakato mzima kwa kweli ilikuwa ni comedy ya kuhuzunisha kwani wanawake hasa wale wazanzibar wameonesha udhaifu wa hali ya juu hivi kweli mtu anaweza akasema kura zigawanywe mara tatu????? kweli?? eti alafu zupunguzwe rondomly yaani ni utumbo na utoto hata watoto wa shule ya awali hawezi kufanya huo utumbo jamai inahuzunisha sijui itakuaje watatoa maoni gani jamani unaweza ukalia na kutoa machozi kwa ajili ya nchi hii lakin ukitafakari yote haya yanatoka kwenye kile chama ulichokiweka madarakani kwa nguvu zote,,jamani tuamke mimi na wewe tufanye mabadiliko 2015
 
Haya ndo matunda ya kukusanya kiholela mradi tu mtu (rais) anataka sifa uliiona wapi katiba anajadiliwa na waganga, watoa maruhani na wachawi . hawa si wana matambiko yao?
 
Back
Top Bottom