Wateule wa Trump wana mahaba yaliyopitiliza kwa Israel kuliko hata mawaziri wa Biden!

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika hatua za kuthibitishwa na seneti ya Marekani, Waziri mteule wa Ulinzi wa Marekani wa utawala wa Trump anasema anasapoti Israel "kuwaua" Hamas wote hadi wa mwisho kabisa!

Waziri mteule wa mambo ya nje wa Trump, Marco Rubio anasema Gaza itapata amani tu endapo Hamas watawaachilia mateka wote(sijui ni mateka gani ambao bado wanashikiliwa na Hamas mpaka sasa!). Pia anawaita Hamas "brutal savages". Ameishutumu vibaya mahakama ya ICC kwa kutoa hati ya kukamatwa Netanyahu akisema imepoteza muelekeo.

Anazidi kulishwa sumu na Republicans wenzake jinsi gani Biden ameipa nafuu Iran kwa kuilegezea vikwazo kupelekea uchumi waka kuimarika na kuifanya iweze kusapoti magaidi katika nchi mbalimbali Mashariki ya kati.

Moja ya mambo ambayo MAGA wafuasi wa Trump huko Marekani na hapa wa hapa Africa walikuwa wanapigia kelele ni utawala wa Biden kuikumbatia sana Israel na Ukraine na Marekani kuingilia migogoro ya mataifa mengine ambayo wanaamini haiwahusu!
 
Katika hatua za kuthibitishwa na seneti ya Marekani, Waziri mteule wa Ulinzi wa Marekani wa utawala wa Trump anasema anasapoti Israel "kuwaua" Hamas wote hadi wa mwisho kabisa!

Waziri mteule wa mambo ya nje wa Trump, Marco Rubio anasema Gaza itapata amani tu endapo Hamas

watawaachilia mateka wote(sijui ni mateka gani ambao bado wanashikiliwa na Hamas mpaka sasa!). Pia anawaita Hamas "brutal savages". Ameishutumu vibaya mahakama ya ICC kwa kutoa hati ya kukamatwa Netanyahu akisema imepoteza muelekeo.

Anazidi kulishwa sumu na Republicans wenzake jinsi gani Biden ameipa nafuu Iran kwa kuilegezea vikwazo kupelekea uchumi waka kuimarika na kuifanya iweze kusapoti magaidi katika nchi mbalimbali Mashariki ya kati.

Moja ya mambo ambayo MAGA wafuasi wa Trump huko Marekani na hapa wa hapa Africa walikuwa wanapigia kelele ni utawala wa Biden kuikumbatia sana Israel na Ukraine na Marekani kuingilia migogoro ya mataifa mengine ambayo wanaamini haiwahusu!
Trump na wafuasi wake wengi ni wajinga wajinga vichaa
 
Wewe tu hapo Mwananyamala Kisiwani kuwaona wajinga kisa wanachukia ugaidi hakuwezi kuwafanya wawe wajinga kwa mtazamo wa wengine hivyo hayo yanabaki tu kuwa ni mtizamo wako ambao hauakisi ukweli wowote.
 
Mtu asiye jua wanasiasa ni watu gani ndo anaweza kitilia maanani hizo ngonjera.
Kiufupi hayo ni maneno ya kisiasa yasiyo kuwa na uhalisia.

Hata Baden na mawaziri wake wangetamani Hamas ifutike kabisa na asiwepo mtu yeyote anajiita Hamas ndani ya dunia hii na ndio maana wanatoa silaha za kupambana nao na kuwauwa, lakini kiuhalisia hicho kitu hakiwezekaniki.

Alafu kusema eti Palestina haitokuwa na amani mpaka Hamas ifutike hizo ni propaganda na kijinga na kipumbavu kwa sababu Hamas imeanzishwa juzi juzi tu na kukuta Israel ikiwa imepigana vita kibao na wapalestina.
Na hata Hamas ikitokea ikafutika mgogoro hautaisha kwa sababu chanzo na chimbuko la mgogoro sio Hamas.

Kuhusu Netanyau kutafutwa na ICC kwani kuna waziri yeyote ndani ya baraza la Baden aliye unga mkono kukamatwa kwa Netanyau?

Kuhusu Iran ni propaganda zile zile kwasababu tangu Trump aweke vikwazo dhidi ya Iran walivyo dai ni vikali kuwahi kutokea mwaka 2018 ,Baden hajawahi kutoa kikwazo hata kimoja badala yake aneongeza vingine.
Kinacho fanya vikwazo vionekane vimefeli ni kwa sababu dunia imebadilika sana japo Wamagharibi na nyinyi wafuasi wake hamtaki kuukubali huo ukweli ambao ni mchungu kwenu.
Kwa sasa njia za kufanya biashara ni nyingi na ndio maana Urusi imetolewa kwenye mfumo ya SWIFT lakini bado unaendelea kufanya biashara za mabilion ya fedha duniani.
Iran haipo kwenye mfumo wa SWIFT lakini bado anafanya biashara za mabilion ya$ duniani kote.
Kwa hiyo kuhusu Iran hakuna chochote kitakacho badilika hata Trump angekaa ikulu miaka 20 labda waanzishe vita moja kwa moja na Iran.

Yaani Uchina au India waache kununua mafuta ya bei mlazo kutoka Iran kisa Marekani kasema ?huo wakati umesha pita.
Kuhusu Iran kuyadhamini makundi ya wanamgambo kwani Iran kaanza kuyadhamini baada ya Baden kuingia madarakani,au kwenye awamu ya kwanza ya Trump Iran ilikuwa haiyadhamini makundi hayo?
 
Unafahamu thamani ya Exports za Iran za mwaka jana ni sawa na za karibia miaka 10 iliyopita?
 
Exports nyinyi za Iran haziko kwenye rekodi rasimi kwa sababu bidhaa nyingi za Iran zina uzwa nje ya mfumo.
 
Back
Top Bottom