Wateule wachemsha Kilimanjaro Festival, wamuangusha Jay Moe

inspectorbenja

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2012
Posts
597
Reaction score
651
Da mimi kama mpenzi wa hip hop na mpenzi wa kundi la Wateule nilosikitishwa na performance yao mbovu pale jukwaani.

Mtu pekee aliyelitendea haki jukwaa ni Jaymoe, kwanza alikuwa anaimba bila play back halafu alikuwa anajaribu kumaliza nyimbo ila Mox alikuwa anamuingilia ingilia na kuharibu performance yake.

Jafarai yeye ndo alichemka mpaka basi ikabidi ikifika zamu yake wawe wanakata tu.

Mox ndo hovyo kabisa alishindwa kuimba. Yaani bila Jay Moe,Wateule wangedharirika vibaya mno.

Sasa nimeamini kwanini Jaymoe aliamua kwenda solo,hawa jamaa wanamyeyusha.
 
Wateule walitia aibu sana, sisi ma long timer tulisikia aibu! Wasanii wa zamani ni walalamishi kutopewa show lakini namna ile bora akina Harmo Rapa [emoji41]

Kwa ufupi wengi waache ulalamishi waendelee na mishe zingine! Makelele mengi, mara mikono juu, nyimbo zao wanazisahau! Sauti hakuna ...aibu aibu!
 
Kwa WATEULE,mwanamuziki na msanii pekee na kipaji ni Jay Mo tu.Hao wengine waliobakia ni Wasanii tu na walijikita huko kwakuwa hawakua na shughuli ingine ya msingi ya kufanya.
 
Tatizo mox daily yupo mitungi + mibangi huko kuimba atawezaje?
 
Hatahivyo Jaymoe hajawahi kufanya nao kazi kama kundi rasmi, walikuwa wanakutana tu kwenye baadhi ya nyimbo, Jafarai na Mox ndo waliwahi kuwa kundi
 
Tungepata hata ka video ingependeza.... Ili tujaji vizuri
 
Mkuu unapaswa kujua pia kwamba Mox na Jafari ni kama waliisha acha muziki kitambo sana
Jay Mo ndio bado mbishi anatoa nyimbo na zina hit fresh na shows anapiga kiaina sio kama akina Mox na Jafarai wanlewa na wanadeal na mambo mengine kabisa na hata wakiingia studio ni ile kama hobi tu kwamba na yeye bado yupo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…