WATHAMINI WALIO KULIPIA BILL

WATHAMINI WALIO KULIPIA BILL

fakhbros

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2013
Posts
384
Reaction score
658
Mzee wa makamo alie ongozana na mwanae walikuwa wameketi pembezoni mwa kuta za mgahawa pale mlimani city,

Hawakuonekana kuwa ni wazoefu wa maeneo hayo japo kijana alionekana kuwa mtanashati kutokana na mavazi yake niwazi huenda alikuwa ni mtumishi katika ofisi za Uma'

Mzee nywele zake zilichakaa kwa mvi miwani iliweza kuongeza uono wake japo hakuwa na kumbukumbu sahihi juu ya mambo mengi yalio jiri mbele yake,

Mhudumu mmoja wa kiume alikuwa amesimama mbele yao huku akiwaelimisha wateja wake aina ya huduma zinazotolewa katika mgahawa ule,

Kijana aliagiza vyakula aina mbalimbali kwa yule mhudumu na alitoa porch yake mfukoni nakuweza kulipia huduma alizo hitaji kupatiwa na yule mhudumu,

Baada ya muda yule kijana alikuja pale mezani akiwa na sahani za vyakula vilivyo agizwa,

Wakati wa kula, yule mzee mara kwa mara chakula kilianguka kwenye shati na suruali yake.

Watu wengine waliokuwa pale walimtazama mzee huyo huku nyuso zao zikiwa zimekunjamana kwa chuki kutokana na ulaji wake, lakini mwanawe alibaki mtulivu pasina kukeleka kwa lolote juu ya matendo ya baba yake kwa jinsi alivyokuwa akijitapakaza mabaki ya vyakula,

Baada ya wote wawili kumaliza kula, mwana, alimyanyua baba yake kimya kimya na kumpeleka chooni kumsafisha mabaki yalio kuwa yamechafua shati lake na uso wake uliokunjamana, na kuosha madoa ya chakula kutoka kwenye nguo zake; na kisha akamchana nywele zake zilizo jaa mvi,

Baada ya muda waliweza kutoka kule uwani, kimya kirefu kikatawala ndani ya mgahawa ule wa mlimani city,

Yule kijana akiwa tayari kulipa bili,

lakini kabla ya kuondoka, mwanaume mmoja mtu mzima alisimama na kumuuliza yule kijana! 'Je hufikirii kuwa umeacha kitu hapa?

Kijana akajibu:
'Hapana, sikuacha chochote.' Kisha yule mzee akamwambia: 'Umeacha somo hapa kwa kila mtu alie keti hapa, nina matumaini kwa kila baba! wa sasa na ajae amejifunza kitu kutokana namna unavyo mthamini mzazi wako"

Wakati wote pale mgahawani watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza yule mzee, kwa jinsi ukimya ulivyokuwa umetawala ungeweza kusikia mlio wa sindano ikidondoka.

Katika Maisha"
Moja ya heshima kubwa iliyopo, ni kuweza kuwatunza wale ambao waliweza kututunza tungali wadogo, kuishiwa nguvu wazee wetu haiwezi ikawa sababu ya wao kutengwa na sisi,

Ni jukumu la kila kijana kufahamu kuwa yupo hapo alipo sababu kuna watu walio jitolea kumfikisha kwa gharama na nguvu nyingi ili aweze kuifikia ndoto yake ni vyema kila mmoja akatambua kuwa yeye amekuwepo kwa sababu kulikuwa na mtu alieweza kulipia bill

Wazazi wetu na wale wazee wote ambao walijitolea maisha yao, kwa wakati wao wote, pesa na juhudi kwa ajili yetu, wanastahili heshima yetu kubwa.

Tuwapende wazazi na asante kwa kusoma,
893de11e58f04c38cb9fc0569e123461.jpg
 
Yote inategemea mtoto umemleaje, kama ulimlea hovyo basi sahau hilo hapo juu, kwanza hata muda wa kukupigia simu Hana...upweke wa uzeeni unatisha sana hasa kama ulikuwa paka na watoto ni panya.
 
Mzee wa makamo alie ongozana na mwanae walikuwa wameketi pembezoni mwa kuta za mgahawa pale mlimani city,

Hawakuonekana kuwa ni wazoefu wa maeneo hayo japo kijana alionekana kuwa mtanashati kutokana na mavazi yake niwazi huenda alikuwa ni mtumishi katika ofisi za Uma'

Mzee nywele zake zilichakaa kwa mvi miwani iliweza kuongeza uono wake japo hakuwa na kumbukumbu sahihi juu ya mambo mengi yalio jiri mbele yake,

Mhudumu mmoja wa kiume alikuwa amesimama mbele yao huku akiwaelimisha wateja wake aina ya huduma zinazotolewa katika mgahawa ule,

Kijana aliagiza vyakula aina mbalimbali kwa yule mhudumu na alitoa porch yake mfukoni nakuweza kulipia huduma alizo hitaji kupatiwa na yule mhudumu,

Baada ya muda yule kijana alikuja pale mezani akiwa na sahani za vyakula vilivyo agizwa,

Wakati wa kula, yule mzee mara kwa mara chakula kilianguka kwenye shati na suruali yake.

Watu wengine waliokuwa pale walimtazama mzee huyo huku nyuso zao zikiwa zimekunjamana kwa chuki kutokana na ulaji wake, lakini mwanawe alibaki mtulivu pasina kukeleka kwa lolote juu ya matendo ya baba yake kwa jinsi alivyokuwa akijitapakaza mabaki ya vyakula,

Baada ya wote wawili kumaliza kula, mwana, alimyanyua baba yake kimya kimya na kumpeleka chooni kumsafisha mabaki yalio kuwa yamechafua shati lake na uso wake uliokunjamana, na kuosha madoa ya chakula kutoka kwenye nguo zake; na kisha akamchana nywele zake zilizo jaa mvi,

Baada ya muda waliweza kutoka kule uwani, kimya kirefu kikatawala ndani ya mgahawa ule wa mlimani city,

Yule kijana akiwa tayari kulipa bili,

lakini kabla ya kuondoka, mwanaume mmoja mtu mzima alisimama na kumuuliza yule kijana! 'Je hufikirii kuwa umeacha kitu hapa?

Kijana akajibu:
'Hapana, sikuacha chochote.' Kisha yule mzee akamwambia: 'Umeacha somo hapa kwa kila mtu alie keti hapa, nina matumaini kwa kila baba! wa sasa na ajae amejifunza kitu kutokana namna unavyo mthamini mzazi wako"

Wakati wote pale mgahawani watu wote walikuwa kimya wakimsikiliza yule mzee, kwa jinsi ukimya ulivyokuwa umetawala ungeweza kusikia mlio wa sindano ikidondoka.

Katika Maisha"
Moja ya heshima kubwa iliyopo, ni kuweza kuwatunza wale ambao waliweza kututunza tungali wadogo, kuishiwa nguvu wazee wetu haiwezi ikawa sababu ya wao kutengwa na sisi,

Ni jukumu la kila kijana kufahamu kuwa yupo hapo alipo sababu kuna watu walio jitolea kumfikisha kwa gharama na nguvu nyingi ili aweze kuifikia ndoto yake ni vyema kila mmoja akatambua kuwa yeye amekuwepo kwa sababu kulikuwa na mtu alieweza kulipia bill

Wazazi wetu na wale wazee wote ambao walijitolea maisha yao, kwa wakati wao wote, pesa na juhudi kwa ajili yetu, wanastahili heshima yetu kubwa.

Tuwapende wazazi na asante kwa kusoma,View attachment 3088334
Uzi mzuri, ila wengine baba zetu tumewapoteza kabla hawajala matunda yetu, tumebakia na mama, wengine wamepoteza wazazi wote wawili, sasa sijui tutamtunza nani.
 
Kuna Wengine wanadhani k ni Bora kuliko wazazi choo kinaanguka kijijini....umekazana na kumpa mchepuko Raha za Dunia ...mama Yako kitenge hakijui wewe unampeleka mchepuko shopping ya nguo......karma is bitch itakukula.
 
Vipi kuhusu sisi tulio ishi maisha Kama ya ndege. Kwa shangazi, kwa mjomba kwa Bibi kwa majirani. Wazazi hawakuwa na muda na sisi si kifedha Wala ushauri Kama tumekuja kwa bahatimbaya
 
Back
Top Bottom