Watia nia CHADEMA hopefully mnaielewa katiba ya chama pamoja na taratibu zake

Watia nia CHADEMA hopefully mnaielewa katiba ya chama pamoja na taratibu zake

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
Kwema wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye mada. Miezi ya hivi karibuni kuliibuka mtindo uliopachikwa jina la "Kuunga Mkono Juhudi" ambapo Viongozi mbalimbali waliokua upinzani walijiondoa na kujiunga na Chama tawala cha CCM.

Wengi wa hawa waunga mkono juhudi walitokea Chama cha CHADEMA, na mmojawapo ya sababu walizozitoa kwa wale wabunge ni kua wanalazimishwa kuchangia chama kutoka kwenye posho na stahiki zao za ubunge.

Viongozi wa CHADEMA walijitetea kua michango hiyo iko kikatiba, na matumizi yake yako kwenye taratibu za chama ambazo zinafahamika, na kua Waunga mkono juhudi hao wameamua kudanganya umma.

Sasa basi, sasa tuko kwenye kinyang'anyiro kingine, cha kuwapata Wabunge wa awamu ingine. Nina uhakika kabisa chama hiki kikapata wawakilishi wa awamu hii ingine inayokuja.

Ni vyema wawakilishi watarajiwa nyinyi mkaisoma Katiba ya chama inasemaje, pia msome na mjifunze taratibu za matumizi zikoje. Mtaonekana Wajinga sana kama sasa mnaomba kupitishwa na chama ambacho hamjui hata Katiba yake ikoje.

Mjue tu kua uungaji wenu Juhudi mkiwa mmechaguliwa mtaitia nchi hasara ya zaidi ya Billion 1 kwa kila Mbunge atakaeunga mkono Juhudi, fedha ambazo zingeweza kutumika kufanya mambo mengine ya Maendeleo.

Yangu ni hayo tu kwa ufupi kwa Weekend hii.
 
Msitegemee mabadiliko ya maana inchi hii kama mtaendelea na kuchagua CCM kila siku.
 
CCM ndio iliyotufikisha hapa,moja ya nchi maskini duniani lakini iliyojaa rasilimali.
 
Msitegemee mabadiliko ya maana inchi hii kama mtaendelea na kuchagua CCM kila siku.
Mabadiliko ya nguvu yameanza kuonekana kwenye utawala huu wa mkombozi wa uchumi na miundombinu ya nchi Magufuli mtumishi wa Mungu kwa watanzania.
 
Mabadiliko ya nguvu yameanza kuonekana kwenye utawala huu wa mkombozi wa uchumi na miundombinu ya nchi Magufuli mtumishi wa Mungu kwa watanzania.
Hii post yako iko nje ya mada husika
 
post number 2.ipo nje ya mada ila kwasababu nae ni nyumbu unaona ipo sawa tu.
Sio kila Faulo lazima Refa apige filimbi,
Na Kila Refa hua nae ana timu yake.
 
18 Julai 2020
Kibamba, Dar es Salaam

Ernest Mgawe atia nia ubunge ateuliwe CHADEMA eneo jimbo Kibamba

 
TUKIUPATA UBUNGE TUNAKULA HADI KUVIMBIWA NA MICHANGO TUNALIPA BILA SHIDA,TUKISHAVIMBIWA VYA KUTOSHA DAKIKA ZA MWISHO NDIYO TUNAANZA KULALAMIKIA MICHANGO HIYO
 
Back
Top Bottom