Kiwalani finest
Member
- Jul 6, 2024
- 97
- 72
Baadhi ya Watia Nia Uenyekiti wa Mitaa na Vitongoji mliomwaga mihela ya rushwa mkapenya mmezienda kinyume taratibu za CCM na kuikiuka sheria iliyopelekwa bungeni na Rais na kupitishwa, mnatajikiwa msipigiwe kampeni bali mpelekwe jela kwa unyang’au wenu.
Nilisikika katika ulimwengu wa kiroho huko Ndotoni nikibwata bwato liumilo watu wajifanyao wanarudia makosa kwa maksudi wenye akili kama punda. Nikaanza. Tunapoandika na kuwawekea reference tunataka msome ili mbadilike kitabia na kuwa watu wema. Tunataka sura zenu ziwe na aibu kutenda mambo ya hovyo kinyume na viapo na ahadi kwa jamii.
Tunataka kila kiongozi asome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, toleo 2005, ibara yote ya 08(1) kwa umuhimu wake na kuiishi akiwa na hofu ya Mwenyezi Mungu. Nakumbuka tarehe 18/09/2024, Professor Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana, Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania, alisema: "Hauwezi ukawa kiongozi unazungumza jambo huna marejeo (references)." Kwa hiyo ukiona mpaka tunathubutu kusema ujue tuna mahali tukarejea. Kwa hiyo niwatoe mashaka, hatukusema tu kibaba baba. Tumesema kielimu.
Mwisho wa kunukuu, tusome Katiba ya CCM 1977, toleo 2022, ibara 15(3)(6)(7) uk 152 vifungu 1, 3, 6, 8, na 9. Ilani ya CCM 2020, uk 01 ibara 04. Nakumbuka tarehe 01/11/2024, Mheshimiwa Nicodemus Henry Maganga, Mbunge wa Mbogwe, akiwa Bungeni alisema: "Acha tuseme, hata watuuwe (jambo), hili halikubaliki mbinguni na duniani." Mwisho wa kunukuu.
Askofu Benson Kalikawe Bagonza wa KKKT Dayosisi ya Karagwe, nakumbuka tarehe 13/10/2024 alisema: "Mwenyezi Mungu anajihusisha sana na maisha yetu, na kila wakati akiona mambo yetu hayaendi vizuri, Mungu anatuma watu kutushtua." Mwisho wa kunukuu.
Tusome Katiba ya CCM 1977, toleo 2022, uk 153 kifungu cha 08 ili kuweza kusoma kitabu cha kanuni za uongozi na maadili za CCM na jumuiya zake toleo 2022, uk 02 ibara 04 inatueleza kwamba kutii katiba ya CCM na kanuni zake ni wajibu wa kila mwanachama wa CCM. Mwisho wa kunukuu. Tukitii kanuni hii maana yake tunakuwa hatuivunji sheria ya vyama vya siasa iitwayo The Political Parties Act, Chapter 258 inayovitaka vyama vya siasa kufuata maandiko yake kwa ukamilifu wake kama yalivyoandikwa.
Tunapoitii sheria hii ya nchi, tunakuwa tumeitii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, toleo 2005, ibara 26(1) uk 27 iliyoandikwa: "Kila mtu ana wajibu wa kufuata na kutii Katiba hii na sheria za Jamhuri ya Muungano." Mwisho wa kunukuu.
Tunaokiuka haya huku tukiwa na viapo vya kuyahifadhi, kuyalinda, na kuyatetea, huku tukiwa tumeapa kwa Mwenyezi Mungu kwa kushika vitabu vyetu vya imani zetu, huwa tunamtegemea nani?!? Kuna nyakati Professor Abubakar Bin Zuber Bin Ally Bin Mbwana, Mufti na Shekhe Mkuu wa Tanzania, aliwahi kusema: "Kama mtu hauko kwa Mwenyezi Mungu, uko kwa Shetani."
Mzee Joseph Sinde Warioba, Ex-Makamu wa Rais, Ex-Waziri Mkuu, nakumbuka tarehe 18/09/2024 alisema: "(Wananchi wanasema) wagombea tunao letewa sio tunao wataka, kwa sababu taratibu za vyama vile zinatuletea watu ambao hatuwataki. Pili, wagombea tunaoletewa ni watoa rushwa. Wameupata ugombea kwa kutoa rushwa. (Wananchi) wanasema kwa nini twende kupiga kura." Mwisho wa kunukuu.
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, akiwa katika Harambee ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha wazee, nakumbuka tarehe 26/10/2024 alisema: "Wazee wana maarifa mengi." Mwisho wa kunukuu.
Tumemsikia Mzee Warioba, tujipange kulinda uaminifu na uadilifu wetu kwa jamii kwa kujikumbusha viapo tulivyoapa vya kutokuwa wabaguzi wala wapendeleaji ili tuweze kutumia sheria za nchi kutenda haki tuisemayo kwa kuwaengua watoa rushwa kupata vyeo, kwa vile ni watu wanajulikana.
Tukisoma ilani, katiba, kanuni, miongozo, na taratibu tutaona ukiukwaji na kisha kuwachukulia hatua wanaohusika kuliko kutenda dhambi ya kuwanadi huku tukiwapuuza mafukara malalamiko yao kisa tu hawana fedha za kutumia kupinga sheria. Kama manyang’au manafiki yavaao ngozi ya mwanakondoo yafanyavyo bila kuwa na aibu kisha kukimbilia nyumba za ibada yakijifanya yanataka kuombewa huku yakiwa yanapuuza hata maagizo ya viongozi wetu wakuu wa kitaifa.
Tunaopinda sheria tukawaacha watu wema wasiotumia rushwa, tukawachukua watoa rushwa na kuwalazimisha mafukara wawashangilie na kuwafanya viongozi wao. Sisi tuyafanyayo hayo, imani zetu ziko kwa nani?!? Tukiambiwa tumevaa ngazi za mwanakondoo tutajisikia vibaya?!? Hivi hatukuumbwa na nyuso zenye haya?!?
Ni lazima kuelezana uhovyo unaozidi kushamiri kwa msaada wa machawa ili turudishane kwenye msimamo sahihi wa kuijenga nchi. Nakumbuka tarehe 11/09/2021, katika kipindi cha Medani za Kisiasa, Mheshimiwa Fredrick Sumaye, Ex-Waziri Mkuu wa Tanzania, alisema: "Kwa mfano, Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi, kama anai criticize serikali yake kwa jambo la halali, tusikasirike. (Tujue Mbunge) huyo anatujenga. Kama anaikosoa serikali yake ili iweze kutenda vizuri zaidi, huyo anafanya kazi ya wajibu wake kama Mbunge. Tusione huyo ni msaliti fulani." Mwisho wa kunukuu.
Nami, kwa mujibu wa Katiba ya CCM 1977, toleo 2022, uk 10-11 ibara 15(7), ninao wajibu huo uliofungamanishwa na Ilani ya CCM 2020, ibara 04 uk 01. Wakili Jasiri na Msomi, Boniface Anyisile Mwabukusi, Rais wa TLS, nakumbuka tarehe 29/10/2024 alisema: "Nasema siku zote, usipozungumza na mimi, na mimi nisipozungumza na wewe, hutanifahamu mimi ni nani. Lakini tukijenga utamaduni wa kuzungumza kama taifa, tutalitunza taifa letu. Tutalinda sheria zetu, tutalinda haki za binaadamu, na tutaifanya nchi yetu iwe mahali bora kuishi kwa kila mmoja." Mwisho wa kunukuu.
Kwa mujibu wa Ilani ya CCM 2020, sisi wanaccm tuna mkataba na jamii ya Kitanzania ambapo tuliiahidi uadilifu na uaminifu kwa mifumo ya nchi. Tusome ilani ya CCM 2020 uk 298 ibara 251, uk 04-05 ibara 07 ili kwenda kusoma Ilani ya CCM 2015 uk i ibara (01) na uk 230 ibara 177, kisha turudi ibara 10 na 11 uk 08 wa Ilani ya CCM 2020 kuhitimisha kwa lengo la kuhuisha uk 161-168 wa Ilani ya CCM 2020-2025.
Tunapaswa kuto kuwafumbia macho viongozi wa hovyo ndani ya nchi ambao siku zote wamekuwa na furaha ya kurudia rudia makosa yale yale kwa maksudi kana kwamba walipoteza akili za kibinaadamu na kubakia na akili za punda.
Shekhe Twaha Suleiman Bane, akitoa mawaidha tarehe 20/07/2022, alisema: "Mtu akikerwa lakini yeye (mtu huyo bado) anaifurahia kero (mtu) huyo ni sawa na punda. Utu unataka mtu akikuudhi (na wewe lazima tu) uudhike. Ila sasa kwenye malipizi uzuie moyo wako usifanye hivyo." Mwisho wa kunukuu
Watoa Rushwa wanashangilia kwa vigoma huku wakijua wamepenya kwa rushwa. Viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya wanawalazimisha watu wema kusema na kuwashuhudia watoa rushwa kuwa ni watu wema wanaoweza kuiinua jamii kiuchumi.
Tusome ilani ya CCM ya 2020 uk. 04-05 ibara 07, kisha tuendelee kusoma ilani ya CCM ya 2015 uk. 233-234 ibara 185(c) kwa msisitizo, ili kujua msimamo wa chama kuhusu masuala ya rushwa.
Mheshimiwa January Makamba, ex Waziri, MNEC, na Mbunge, alikumbuka akifanya mahojiano na Medani za kisiasa tarehe 16/09/2013, ambapo alisisitiza kuwa rushwa ni tatizo kubwa linalosababisha viongozi wasiotokana na utashi wa watu kuchaguliwa. Alisema rushwa inawafanya watu wenye uwezo wa uongozi wakose nafasi ya kuwa viongozi kwa sababu tu hawana fedha za rushwa.
Tusome katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 toleo 2005 ibara 34(4) na ibara 35(1), ambayo inaweka wazi wajibu wa viongozi na wasaidizi wa kumsaidia Rais. Sisi tunaojinasibu kama wasaidizi wa Rais, tunapaswa kutenda kwa mfano mzuri kwa jamii. Tunapoendeleza mambo ya hovyo, tunapelekea ujumbe gani kwa jamii ili izidi kutuamini?
Tunazungumzia sheria za nchi, lakini tunawashangilia watoa rushwa kwa kisingizio cha kusema chama lazima kishike dola. Uadilifu wetu kwenye masuala ya rushwa ukoje? Viongozi watoa rushwa wanapata vyeo, lakini mafukara, vibaka na wezi wa kuku wanahukumiwa kwa sheria zipi?
Askofu Augustino Ndeliakyama Shao, Askofu wa Jimbo la Zanzibar, aliongea tarehe 28/10/2024 akisema kuwa dhambi inaanza kwa kujificha, na kwa sababu hakuna anayekemea, watu wanarudia dhambi na kuona rushwa ni jambo la kawaida. Hii inadhihirisha kuwa rushwa imekuwa mazoea katika jamii yetu.
Mtume na Nabii Josephati Elias Mwingira wa Kanisa la Efatha, tarehe 15/10/2018, alisema kuwa Tanzania inapaswa kujiunga kwa haki na sheria ya Mungu ili Mungu aibariki nchi yetu. Alisisitiza kuwa Mungu haangalii Serikali, bali anatuangalia sisi tulio okoka.
Tuache tabia za kulala makaburini huku tukiwahangaisha mafukara kwa kusema kesho tutavunja sheria mbele ya umma. Tunataka kuona watoa rushwa wakitenguliwa na kuchukuliwa hatua, huku viongozi wema wakiongoza na bila rushwa.
Mheshimiwa January Makamba alikumbuka wakati akimsaidia Rais ambapo walizungumzia suala la rushwa kwenye chaguzi. Alikumbuka hotuba ya Rais mwaka 2005 ambapo alisisitiza lazima kuwe na sheria za kuthibiti matumizi ya fedha za uchaguzi. Rushwa katika chaguzi ni tatizo kubwa ambalo limeathiri nchi yetu.
Kwa msingi huu, watu wameshindwa kupata majibu kuhusu ukiukwaji wa mifumo, lakini wameonyeshwa dharau. Hatuwezi kushiriki katika kupinga sheria ya Rais huku tukiwashangilia watoa rushwa kupata vyeo. Tunahitaji kurekebisha hali hii.
Padre Dkt Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki wa Tanzania (TEC), alikumbuka tarehe 26/10/2024 akisema kuwa watu lazima wakubali kutawaliwa na sheria. Alisisitiza kuwa utawala wa sheria umeshuka, na nchi inaongozwa na sheria sio na mtu.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Mathias Mugerwa Kahinga