Watia nia wana nia gani?

Watia nia wana nia gani?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,713
Reaction score
6,121
Kwa mujibu wa Takwimu zisizokuwa rasmi ndani ya Chama Cha Mapinduzi idadi ya watu waliochukua fomu ni zaidi ya 500 na bado wanaendelea kuchukua.

Wanaochukua fomu ina maana kwamba ni wanachama HAI wa CCM na kwamba wanayo kadi ambayo wanailipia.Kama gharama ya Fomu ni TZS 100,000 ina maana kwamba CCM itakusanya sio chini ya TZS Milioni 50 katika zoezi la uchukuaji wa fomu za ubunge na udiwani.Pamoja na hayo naamini kabisa kuna michango mingine ambayo wanachama wanatoa katika kuunga mkono chama.

Swali la kujiuliza ni Je CCM inafanya Biashara ya kuuza FOMU za KUGOMBEA uongozi?Wakati huo huo CCM ina vitega uchumi vingi kuliko chama chochote kile cha siasa hapa nchini na zaidi ya hayo CCM inayo access ya Rasilimali mbalimbali za serikali ambazo inaweza kuzitumia katika shughuli za kisiasa ikiwamo "STATE MACHINERY"

Katika CCM hiyo hiyo inategemewa kwamba Mgombea wa nafasi ya uongozi atajigharamikia kwa kiasi shughuli zake za kampeni(HILI linahitaji uthibitisho rasmi) na kwa hio pesa zote za CCM zitatumika katika kuhakikisha wanashinda ikiwamo pesa za watia nia wao ambao wengi wana ukwasi wa namna moja ama nyingine.

Wakati huo vyama vingine havina hata bajeti ya uchaguzi na inategemewa kwamba wagombea wake wajigharamikie kampeni.Aina ya wagombea waliojitokeza katika upinzani wengi ni watu wa Kipato cha chini ingawa taifa letu ni la kipato cha kati.

Wakati huo huo inasemekana kwama Tume yetu ya uchaguzi haiko huru katika maamuzi yake(Hili nalo linahitaji kuthibitishwa) na wengi wa wagombea wanaamini kwamba NEC imeelekezwa kutangaza Wagombea wa CCM tu kuwa wameshinda.

Sasa katika mazingira haya, utaona kwamba Uchaguzi wetu wa mwaka huu HAKUNA NAMNA UNAENDA KUWA FREE AND FAIR ELECTION.

Tusidanganyane kwamba kuna uchaguzi HURU na wa HAKI katika mazingiri ambayo kabla hata Mechi haijaanza Mshindi anaonekana.

Ila kuna jambo moja la kujipa MOYO.Sisi kama wananchi Tuendelee kujitokeza kwa wingi na SISI kuchukua fomu ili na sisi tuende bungeni tukangonge Meza au tuende kwenye halmashauri tukajipe TENDA za kuzoa taka.Sio kwamba tutashinda hapana.Tujitokeza ili wajue kuwa na SISI tunataka kula pia.

Wakikata Majina yetu katika KURA ZA MAONI Ndani ya CCM tusijali turudi UPINZANI,Kuna vyama ka TLP,NCCR,UDP,TADEA ACT ETC ambao vitakuwa tayari kuwapa JUKWAA baada ya kukatwa ndani ya CCM.Tukifika huko tugombee.

Tufanye Kampeni ya Nguvu,tuzungumze na raia mmoja mmoja kwa heshima na staha bila kutukana wala kukejeli na tuwaeleze maono yetu juu ya TAIFA letu.Tuwaambie kuhusu UNIVERSAL HEALTH SERVICE kwa watu wote,Tuwaambie kuhusu ELIMU BUZRE,Tuwaambie kuhusu tatizo la ajira,Tuwaambie kuhusu tatizo la huduma mbovu katika taasisi za umma,Tuwaambie kuhusu Rushwa.Tuwaambie ili wajue kwamba tunajua.

Tusisahau kuwaambia kwamba sisi hatuna uwezo wa kuiangusha CCM bali wao wanao uwezo wa kuiangusha CCM.Tuwaambie Tatizo sio CCM kama chama,Tuwaambie kwamba tatizo ni CCM kama MFUMO.

Tuwaambie ukweli kwamba Mfumo CCM ni kandamizi,Mfumo CCM ni Baguzi,Mfumo CCM ni Nyonyaji,Mfumo CCM ni Nyanyasaji,Mfumo CCM kandamizi.

Tuwaambie wapiga kura kwamba Mfumo CCM lazima ubadilishwe,ndani ya CCM na nje ya CCM.

Hata kama Chama cha Mapinduzi kitabaki lakini MFUMO CCM uondoshwe katika nchi yetu.

Tuwaambie kwamba namna ya kwanza ya kuondoa MFUMO CCM ni kwa kuweka Wapinzani WENGI BUngeni,Tutengeneze BUnge ambalo lina 75% ya Wapinzani.

Lakini tuwakumbushe umuhimu wa kupiga KURA.Tuwaambia kwamba tukipiga KURA wote hata wakiziiba watakosa ujasiri wa kusimama mbele zetu,Watajua tumewakataa na tumekataa MFUMO CCM

Tukiweza kuwapa ujumbe huo kwa hakika watabadilika.ULE MSEMO WA CCM NI ILE ILE UTAKO.MFUMO CCM UTAKUFA NDANI NA NJE YA CCM.

Ila TUJIULIZE hivi kweli kuna uchaguzi HURU na HAKI katika Mazingira ya DAVID na GOLIATH?Labda tutafute siri ya Kombeo la DAUDI tuitumie.Tuweke JIWE KATIKA Kombeo ambalo ni sanduku la KURA na TUUPIGE MFUMO CCM kwenye.

Kwa Pamoja tutashinda.
Kizito S.
Mbunge wa Wananchi
 
Back
Top Bottom