Tatizo la kulawitiwa kwa watoto linalizidi kushika kasi nchini huku idadi ya visa vilivyoripotiwa kwenye kipindi cha mwaka 2016-21 vikiwa ni 5716 huku 87% ya visa hivi vikihusisha watoto wa kiume.
Mgawanyiko wa idadi ya wahanga ipo kama ifuatavyo-
Mwaka 2016, wasichana walikuwa 50 na wavulana 487
Mwaka 2017, wasichana walikuwa 59 na wavulana 442
Mwaka 2018, wasichana walikuwa 133 na wavulana 1,026
Mwaka 2019, wasichana walikuwa 212 na wavulana 1,193
Mwaka 2020, wasichana walikuwa 115 na wavulana 885
Mwaka 2021 kwa pamoja jumla ya watoto 1,114 walilawitiwa
Unadhani nini chanzo cha kuongezeka kwa janga hili? Kipi kifanyike kulikomesha?