Watoto kuchukia kunyonya na kula

Baba jayaron

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2015
Posts
4,324
Reaction score
5,933
Habari waugwana,

Leo nimekuja na changamoto ambalo limekua kwa kasi ajabu lakini likituacha wengi bila kujua nn chanzo chake.

Kunakesi kama kumi au zaidi nimezisikia na kuziona jinsi mtoto anavyokataa kabisa kunyonya maziwa ya mama yake tangia akiwa ndani ya mwezi mmoja wa kuzaliwa na wengine hata chochote hawataki.

Juzi mwenzangu alimpeleka ndugu yake mwenye mtoto mdogo wa miezi kama mitatu kwakua mtoto amekataa kula karibia wiki na zaidi kila wakimkaba hataki mpaka wamemchubua fizi na kumtoa vidonda mdomoni kwa kukaba kula hivo ikafikia mtoto amelegea na nguvu kuisha kabisa hivyo akawekewa drip na anaendelea na matibabu.

Pia mwenyewe ninamtoto wa mwaka mmoja nae ghafla hataki kula kabisa ukimlisha ni kilio na kukabana sana napo atakula kidogo sana wakati haikua kawaida yake, huyu nafuu maana ananyonya ila wengine hatakunyonya hawataki kabisa.

Wenye utaalam na expirience juu ya hili watujuze.

Karibuni
 

Tusubiri waje wataalamu! Na Mimi mtoto wangu hataki kula kabisa@
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…