Watoto mara nyingi hulia kwa sababu ya hasira

Watoto mara nyingi hulia kwa sababu ya hasira

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2022
Posts
3,644
Reaction score
4,315
Kwa nini watoto hulia?

Naamini kwamba tukiwachukua akina mama kumi wenye watoto wadogo na kuwauliza ni sababu zipi zinazopelekea watoto wao kulia watataja vitu kama; njaa, kutaka kunyonya, kukataa kunyonyeshwa, kwamba ameshiba (wakati wa kulishwa) maumivu, usingizi, joto, baridi, kutaka kubebwa, kutaka kushushwa chini, kiu na kadhalika. Hizi zinatambulika kama sababu za watoto kulia lakini kiukweli zinatatanisha kimantiki mfano hiyo ya mwisho: akitaka kubebwa analia na akitaka kushushwa pia anaangusha kilio!

Basi ndugu zangu wazazi, akina baba na hasa akina mama naomba tutambue kuwa kutokana na tafiti za kisaikolojia, zimeonesha kuwa watoto mara nyingi hulia kwa sababu ya HASIRA. Tukiliweka suala la hasira kama jambo la msingi basi hivyo vingine vitabakia kuwa visababishi tu vya hasira yake kuwaka ndani yake na sio sababu.

Mtoto akisikia njaa, hupatwa na hasira ya kwa nini hajanyonyeshwa na hivyo analia kwa hasira.Mtoto akishashiba na bado analishwa basi hupatwa na hasira kwamba ‘huyu mjinga’ bado ananilisha tu wakati mi nishashiba hivyo anaangusha kilio.Umemuweka kwenye hali ya hewa mbaya anakasirika(ga) sana na kujiuliza hivii, huyu mzazi ananichukuliaje haoni kama mi nasikia/joto baridi basi kanamaindi kanaliaa.Kametulia zake kanataka kulala au kamelala kanasikia makelele halafu kanaamka ghafla, hivi hawa wananichukuliaje? Hawaoni nimelala zangu hapa? Basi kanalia polepole muelewe. Mkijifanya bado hamsikii ndio kanapatwa na hasira zaidi kanapiga kelele hadi pumzi inaisha ndani.Vivyo hivyo wakati kitoto kinataka raha ya kubebwa au kubembelezwa au kuachwa huru kiyadadisi mazingira yake halafu kikanyimwa kimojawapo kati ya hivyo basi lazima kipatwe na hasira.

Kwa nini watoto, malaika wa Mungu wawe wepesi wa hasira kiasi hicho?

Jibu la swali hili ni jambo moja tu, UELEWA. Uelewa wa mtoto bado upo chini, hana muda wa kusumbua akili yake kutumia mantiki nzitonzito ili aelewe. Kwanza baadhi ya sehemu za ubongo hasa hizo za kufikiri kwa kina zinakuwa hazijakomaa. Wakati huo huo mifumo ya hisia (limbic system) inakuwa tayari inafanya kazi maana yenyewe ni ya kizamani zaidi (primitive) na sahili tu. Kwa hivyo tusiwashangae kwa kushindwa kwao kuelewa na wala tusiwakasirikie kwa hilo. Tukikasirika pia tunakuwa tumeungana nao katika kuwa na HASIRA.

Lakini kuna utofauti kati ya hasira ya mtoto na hasira ya mtu mzima. Hasira ya mtoto inatokana na KUSHINDWA KUELEWA WAKATI BADO ANAJIFUNZA wakati huo hasira ya mtu mzima hutokana na KUKATAA KUJIFUNZA NA KUELEWA. Moja yatokana na ujinga, moja yatokana na ujinga na upumbavu. Kuamua kuendelea kuwa mjinga panapokuwepo na uwezo na nafasi ya kujifunza na kuelewa ni upumbavu wa makusudi. Ilinenwa vema kabisa waliposema: Hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu. Nitafafanua;

Misiba: Misiba hugusa watu wote, wanaume kwa wanawake huweza kujikuta wakilia katika misiba. Tunalia misibani kwa sababu tunakuwa bado hatujaelewa ni kivipi? Kwanini hasa tupo katika hali hiyo ya msiba. Tuitumie tofauti kati ya wanawake na wanaume katika misiba kujenga hoja. Wanawake hulia sana katika misiba kuliko wanaume hii ni kwa sababu sehemu yao ya hisia ina nguvu zaidi ukilinganisha na wanaume. Hivyo hata kama itatokea wote wakawa na uwezo sawa wa kufikiri kwa kina basi itachukua muda zaidi kwa mwanamke kuacha kulia kuliko mwanaume. Lakini pia ikiwa ikiwa mwanaume anafikiri kwa kina zaidi ya mwanamke basi atawahi kuelewa na kuacha kulia au kutolia kabisa. Vyovyote vile, atakayewahi kuelewa na kupungua hasira ndiye atakayewahi kuacha kulia.

Na kinadharia kwa mtu huyohuyo mmoja, awe mwanamke, awe mwanaume ikitokea amefiwa na mzazi kilio chake sio sawa na kufiwa na mtoto wake wa kumzaa. Sababu ni kwamba ataelewa mapema zaidi hasa pale ambapo mzazi(babu) alikuwa na umri mkubwa sana kuliko kwa mtoto ambaye hata yeye mzazi (baba) amemzidi umri. Maswali ni mengi anapofariki mwenye umri mdogo kuliko anapofariki ambaye umri umeenda ndiyo maana watu wanachelewa kuelewa na hasira zinakuwa juu zaidi na vilio vinakuwa juu zaidi.

Katika ugomvi, kupotelewa kwa mali, ajali, kupatwa na hasara, usaliti na mambo mengine mengi ya kuumiza watu hupatwa na hasira na kulia. Wengine huelewa na kutulia. Wengine hupanga mikakati na kuja upya. Vilio ni vingi zaidi kwa wale wanaochelewa kuelewa na kukubali hali iliyotokea na hili pia huleta utofauti kati ya wanaume na wanawake. Uelewa ukiwa msingi wa hasira, na hasira ikiwa msingi wa kilio. Tumeelewana? Kuna swali? Kama lipo niachie kwenye maoni (comments).

Inatosha kuwaongelea watu wazima turudi kwa watoto wetu.

Mtoto anapojikwaa na kuumia hupatwa na hasira, kwa nini lile jiwe limekaa hapo hadi yeye amejikwaa? Basi hasira yake huwaka juu ya jiwe na ndio maana ukimfuata ukamsaidia kuhusiana na maumivu ataendelea kulia maana hasira yake bado haijatulizwa. Lakini ukimwambia tema mate tulichape jiwe, na ukaliadhibu basi hasira ya mtoto hutulia na anaweza hata kuacha kulia hata kama maumivu bado anayasikia. Wewe mwambie tu “tumeshamchapa huyo (jiwe) haya nyamaza totoo”. Inachekesha lakini inafanya kazi vizuri sana.Mtoto anapolia kwa sababu ya njaa (hasa yule aliyeacha kunyonya), wapo wazazi ambao humwambia tu haya subiri ninakupikia, akiendelea kulia basi wanamkasirikia mtoto kwa nini Analia njaa wakati tayari tunapika wanakauliza kwa hasira “sasa unataka nini wewe, chakula si ndio hiki tunapika, unalia nini sasa!”. Ukweli ni kwamba huyo mtoto kinachomliza kwanza ni hasira kwa nini haujapika hadi saa hiyo. Kwa hivyo anza kwanza kwa kumuomba msamaha ndio umuelekeze sasa unafanya nini kufidia ucheleweshaji wako. Hapo mtaelewana. Kumbuka tu kwamba yeye asipoelewa ni ujinga, ila wewe mtu mzima usipoelewa ni upumbavu HAMLINGANI.Hivyo basi hata kwa watu wazima tunaowaita watoto (baby) ukimuona Analia anza kwanza kuijali hasira kabla haujajihangaisha na sababu husika. Mmenipata?

Hayo ndio yangu kwa siku ya leo, ninawatakia mafanikio mema katika kuishi pamoja kwa watu wazima na watoto. Wakati unafanyia kazi visababishi, kumbuka kufanyia kazi na sababu yake ambayo haswa ni HASIRA.

October 9, 2024

©Sahilinet
 
Kabla ya yote mkuu naomba ukiweka bandiko uwe unanimention tafadhali,, napenda sana maandiko yako.

Pili naomba nichangie katika mada hii pendwa ya kulia kwa mtoto na hasira.

Mara nyingi huwa najiuliza kwamba ni nani kawafunza watoto kulia, amsjuajs mtoto kwamba kulia ndio kitu anatakiwa afanye soon baada ya kuzaliwa.

Je mtoto anaolia baada ya kuzaliwa yani nani amemfundisha kwamba anatakiwa alie pale anapohitaji kitu fulani? je ni upi mtazamo wako?
 
Lakin JUMA LOKOLE alilia (mpaka kuzimia) kwenye msiba WA Dida hiii nayo ni nini!?
 
Back
Top Bottom