Watoto ni taifa la kesho, upendo na amani kati yetu na wao itawale katikati yetu

Watoto ni taifa la kesho, upendo na amani kati yetu na wao itawale katikati yetu

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
WATOTO WANAFANYIWA UNYAMA.

Inasikitisha kuona watoto wanafanyiwa ukatili mkubwa wa Utekaji,ubakaji,ulawiti na matendo mengi maovu.

Ni nani atawalinda?
Ni nani atawatunza?
Ni nani atawapa malazi?
Ni yupi awape faraja?

PROFESSOR JAY aliona hili na akaamua kutunga wimbo kwa ajili ya watoto pitia lyrics hizi hapa
👇

PROFESOR JAY - TAIFA LA KESHO.

Verse . 1

Wanatia huruma watoto wanakosa raha/ wengine wamedumaa wengine wanakufa njaa/ kilio cha kila siku cha mtoto wa kiafrika/ kiongozi mtarajiwa wa kesho anatahabika/ ona zimeshamili ajili tu kwa watoto/ kitu ninachoona ni amani ndani ya moto/ napata sana uchungu watoto wanauza maji/ kila siku mnasema kwamba elimu ndio mtaji/ ni haki ya kila mtoto lazima apelekwe shule/ serikali imesema kwamba elimu ya msingi bure/ eti watoto wadogo wanatozwa na dalala/ wazazi wamewatenga leo wanawatoa kafala/ ndani ya usafiri mkubwa mdogo nani akae/ mimi nadhani mtoto ili nae akue nae azae/Mnaleta imani za zamani mkubwa ndie ale pacha mtoto ale kicwa na kwando mpate faraja/ mtoto ni mtoto wa kike na wakiume mpe malenzi bora akue ili ajitume/ ona watoto wengi wanatupwa majalalani mama yako angekutupa leo hii ungekuwa nani?

Chorus..

Baba....aaaaa Mama..aaaaa..kaka..aaaaa..nionee huruma dada nionee huruma baba × 2

Verse. 2

"Hata nyinyi vikongo zamani mlikuwa wadogo mbona nikisema saidia watoto mnanipa kisongo/ kila siku mnaimba watoto taifa la kesho/ wengi tunawapoteza na wanakufa kwenye mateso/ mola muweza wa yote saidia malaika hawa/ taifa linapotea na hali inakuwa mbaya/ sio lazima umchape mtoto anapokosa hapo ndipo naona wazazi wanapotoka/ viboko vinafundisha au viboko vinaumiza/ hilo ni swali la msingi tunapaswa kujiuliza maana vikizidi sana mtoto anakuwa nunda/ na kumpeleka shule ni heri kumnywesha maji punda/ ninavyoshauri hivyo sina maana umetekese/ hapana kwanza asome kisha mpe muda acheze/ Nafarijika moyoni kuona watoto wanaruka/ kila ninapopita naona watoto wananizunguka/ nacheza nao na nina jibu maswali yao/ nakula nao na ninaimba pamoja nao/ wazazi na walezi itikieni wito/ wapendeni watoto na msiwape kazi nzito..

Chorus..

Baba....aaaaa Mama..aaaaa..kaka..aaaaa..nionee huruma dada nionee huruma baba × 2

Verse . 3

"Ni vizuri wananchi tukiisaidia mahakama/ kuliko kushuhudia tu jahazi letu linazama/mzee na mvi zake eti anambaka mtoto/ hii imeshamili na wengi wamechomwa moto/ nashauri mahakama iongoze adhabu kali/kunyongwa au kifungo cha maisha hiyo ni halali/ nashangaa binadamu wana tamaa zaidi ya fisi/ mtoto wa miaka miwili eti wanamnajisi/ kiumbe wa mungu anakufa kwa sababu ya mabazazi/ hawastahili kuishi hawa ni bora wapingwe vitazi/ mbona mnawapa watoto wetu wakati mgumu/ona mtoto mdogo wa miaka mitano eti anavuta ndumu/ ameshaijua fedha nyaani ameshakuwa kibaka/ elimu haitambui ndio taifa mnalotaka/ sijui mnao au mmefumba Macho/ Siku watashika bunduki watafuata kile mlichonacho...

FOLLOW NA SHARE PAGE YETU YA UKWAJU WA KITAMBO
MAWASILIANO +255767542202
@followers @everyone
images-4.jpg
 
Back
Top Bottom