Watoto, SEXUALITY

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Miaka ya nyuma ilikuwa mtu akipata mtoto wa kiume anafurahi mpaka basi, akipata wa kike anaanza kufikiria itakuwaje akipata mimba kabla ya kuolewa. Mtoto wa kike alikuwa analeta wasiwasi kwa baba/mama kwasababu ya 'AIBU' anayoweza kuwaletea wazazi na familia kwa ujumla. Mtoto wa kiume yeye alikuwa anaonekana hana 'AIBU' anayoweza kusababisha maana hata akimpa msichana mimba 'huo ndio uanaume'.

Ila siku hizi hata mtoto wa kiume anaumiza kichwa maana akiwa mkubwa anaweza akampelekea mzazi wake BOYFRIEND badala ya GIRLFRIEND. Yani mzazi anapumua pale mtoto anapokua kijana na kuonyesha dalili za kuvutiwa na watu wa jinsia tofauti na yake.

Binafsi sina uhakika nachukuliaje swala la ushoga (kuwa gay) linapoongelewa kwa ujumla bila kuhusisha mtu wa karibu yangu. Nadhani naweza nikawa sijali (yani sichukii wala sisupport) kwasababu ni maisha yao. Ila kichwa kinaniuma nikifikiria kwamba kaBebé kangu kanaweza kuangukia huko. Mungu amuepushie hali hiyo lakini nimejikuta nikijiuliza kama mzazi. .ikitokea akawa hivyo ntachukuliaje, ntaikubali hiyo hali,ntamsupport, ntamtenga? I don't know. Inabaki kuwa ni mtihani ambao namuomba Mungu aniepushe nao. Maadam nilizaa mtoto wa jinsia ya kiume basi awe attracted na jinsia ya kike.

Wewe je, ikitokea mtoto wako wa kiume au hata ndugu/rafiki akawa shoga utafanyaje? Utakubali hali yake na mkaendelea kuwa karibu kama awali? Utamtenga? Utakasirika? Utamsupport kwenye hali yake hiyo?
 
Kuna vitu huwa huwezi ku-predict reactions zake mpaka vikutokee. Na havina uzoefu, leo unaweza kureact hivi kesho vile na keshokutwa viiile na reaction zote zikawa mbovu.

So, ombea isikutokee tu.
 
Kama juhudi za kumrudisha kwenye mstari zimeshindikana. Sitovunja undugu nae, ila ntajitahidi kuwa mbali nae kadri inavyowezekana
 

Nahisi haupo sawa sawa!Upo vuguvugu kwenye masuala ya ushoga? Watu wa type yako siyo vyema wakawa kwenye nafasi za kufanya maamuzi kwa ajili ya maslahi ya jamii,
 
Moja kwa moja nitampinga mwanzo mwisho kwa kufanya juhudi za kumshuri na kumrejesha kwenye misingi na maadili yaliyokubalika tangu enzi na enzi na siyo haya yanayoletwa na mataifa yanayoleta usawa hata katika mambo yasiyo sawa kama ushoga na usagaji
 
Siwezi kuwa nyutro katika swala kama hili. Napinga ushoga na hata ikitokea ndugu/mwanangu akaangukia huko, nitatumia nguvu zote kumfanya arudi. Ikishindikana, nitajiweka pembeni na sitohusiana naye kwa lolote.
 
Dah! Hata sipati jibu.... Namuomba Mungu apishie mbali hlo janga
 
Siwezi kuwa nyutro katika swala kama hili. Napinga ushoga na hata ikitokea ndugu/mwanangu akaangukia huko, nitatumia nguvu zote kumfanya arudi. Ikishindikana, nitajiweka pembeni na sitohusiana naye kwa lolote.

Nyani Ngabu
 
Last edited by a moderator:

Navyo jua na nlvyo soma vitabu vya dini ni kuwa laana uweza kumpata mtu moja kwa moja au kudhuru kwenye kizazi cha muusika..kwa hyo mzazi wa kiume kama alipenda kuwakunja jinsia ya kiume au ya kike(kualawiti) basi laana hyo itaenda kwa mtoto..mtoto ataezaliwa baadae atakuwa shoga kwa maana baba alipenda kuwafanyia basi mtoto atafanyiwa tu..
 
Mnao pendaa vidogo au 0..watoto wenu wa kiume watavitoa 2..na mzidi kulaaniwa
 
Ktk hili name nikiri kwamba ni mtihani mgumu sana. Nimegundua hata unapokuja mjadala juu ya ushoga wengi wetu tunaongea tu juu juu na ninahisi kwamba hii inatokana na wanaojadili kutokuwa na uhusiano wa karibu na watu wa namna hii. Mathalani wanapojadili watu ambao kwenye familia zao tayari kuna watu kama hawa, kidogo mjadala unakuwa fair. Ila kuna watu wanajadili as if ni kitu ambacho kiko so far away from them and never expecting it to happen to their family members. Ushoga upo tena kwa kiasi kikubwa kuliko tunavyoweza kudhani. Mimi sikubaliani nao, ila kama mzazi ninaamini maombi pamoja na kujitahidi ktk kuwakuza vijana wetu kutasaidia. Mungu na awe nasi ktk mtihani huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…