Watoto wa Cleopa Msuya watinga mahakamani kugombea mali

Hapa ni engineer TU wanawaza wasiwe na njaa, nikuhakikishie TU huyo daktari, sijui mkaguzi wa tehama Wana njaa TU , na huenda bila mirathi ya baba yao wangekuwa sakala flani,
Hawawezi kuwa na njaa sbb era yao sio km hii ya kukosa ajira bwana
 
Kwa
Kwa nini wenzake hawamshirikishi huyo aliyeenda mahakamani
 
Baba yako ananikumbusha marehemu baba yangu. Yeye kwa bahati mbaya aliishia la Pili, lakini alifanya juhudi sisi wengine tupate elimu.
Kuna wakati nilipopata kazi nikaanza kusaidia ndugu zangu, Mzee akasema:
"Dogo, ukiona watu wanakusifu kama wewe ni mzuri, ni kwa sababu wanakuwa machawa. Angalia andaa maisha yako ya baadaye utakapokuwa na familia yako.
Mimi na mama ukitaka utusaidie iwe kama una nyongeza, lakini sisi siyo muhimu; muhimu ni wanao na mkeo. Wakikosa elimu huko baadaye wakipata maisha magumu hawatanilaumu mimi, bali wewe uliyewaleta duniani.
Na mimi kazi yangu ilikuwa kukusomesha wewe, na wewe huna deni la kunilipa mimi kwa sababu mimi ndiye niliyekuleta duniani."
Wazee wenye weledi walikuwa wanawapa watoto wao ushauri, siyo kuomba pesa.
 
Mkuu ulivyoelezea kwa kina na kwa namna unavyoifahamu hiyo familia...wewe ni nani? George, Job, Joyce, John au Angela?
 
Mzee wangu alituzaa wengi na Kwa mama tofauti tofauti, na Kila mtu alisoma kadri ya akili zake na uwezo wake. Na alihakikisha Kila mtu kampatia urithi wake ,na Leo kupitia Mali za urithi hakika maisha yanaenda maana bila urithi Mimi mwalimu ningekufa Kwa umaskini,note somesha watoto wale urithi wao na wote wajue ,toto lile halikusikii FUTA kwenye idadi ya watoto wako na wambie wenzake Kwamba huyu fala Hana chake
 
Kijana wa Ifoza kusoma ni jambo moja na njaa/tamaa ya mali ni jambo jingine.

Wewe huoni huo mgogoro tayari kama kuna wasimamizi wanahofiwa kufanya maamuzi bila ridhaa ya wengine? Si ndiyo njaa zenyewe hizo?
 
Dr. Joyce Msuya Mpanju – Mtaalamu wa masuala ya mazingira na microbiology, aliyefikia hadi kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP na sasa ni Afisa Mwandamizi wa ngazi ya juu kabisa Umoja wa Mataifa (UN).
Huyu Mpanju nilidhani miaka yote kuwa ni Mhaya! Au kuna Mpanju mwingine, na atokee kupitia kwenye nafasi hizo hizo ulizotaja?
 
huu ndio upuuz wa kuishi bila kuacha wosia. andikeni wosia wazee kifo ni maumbile lazima utakufa. hapo ungekuta.kila mtu anakufa na chake.
 
Wanagombea Mali walizipata Kituo cha kwanza ni Bar
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…