Watoto wa (Kikristo) hasa kipaimara na komunio wanadhalilishwa kisaikolojia na walezi wao wanapopelekwa kwenye kumbi za sherehe kuungana na walevi

Resilience

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2023
Posts
1,096
Reaction score
4,948
Wakristo jaribuni kutenganisha dhambi na Mungu: mnapotaka kusali salini mkiwa mmevaa unyenyekevu. Mnapotaka kulitumia neno la Mungu au kufanya sala wekeni vitu vyote visivyompendeza Mungu mbali nanyi. Ndivyo biblia inavyotaka na ndivyo tunapaswa kuishi.

Wakristo kuna kitu mnaita ubatizo, komunio nk ambavyo mnafanya kwa watoto wenu. Baada tu hakumaliza tendo la baraka kama biblia ilivyoelekeza mmeibuka na tabia zakufanya sherehe. Mkifanya hizi sherehe mnawaalika watoto wadogo washirikiane na mwenzao. Naomba kuwakumbusha kwamba mnachafua hekalu la Bwana.

Watoto wadogo wanawekwa kwenye sherehe zenye vilevi vya kila aina kuanzia saa moja hadi saa sita usiku. Watu wanakunywa, wanalewa, wanafanya matendo ambayo watoto wasingepaswa kuyashuhudia. Matengeneza kizazi cha aina gani?

Hawa watoto mavazi wanayokutana nayo ukumbini mnaamini yanawabariki? Kisses wanazopeana walevi adharani ukumbini zinajenga nini kwenye akili za watoto? Kwanini msifanye mambo yanayoendana na umri wa mtoto?

Kwanini sherehe za watoto wachanganye watu waliokosea maisha ? Mwenyenzi Mungu mnaamini atasimama kuwalinda watoto wenu kama mlivyomwomba?

Mambo wanayofanya wazazi wa siku hizi kwa watoto hasa kipindi hiki cha likizo si yakuvumilika. Wakristo acheni kumdharau Mungu. Acheni kumfedhehesha Mungu.
 
Cha msingi mimi naona bora waje upande wa pili..
Maana huku naona kama kupo vizuri hivi!,
Hakuna chengachenga, wanamafundisho mazuri kweli..

Al Quran: 5:90
---
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّمَا الْخَمْرُ وَالْمَيْسِرُ وَالْأَنصَابُ وَالْأَزْلَامُ رِجْسٌ مِّنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ فَاجْتَنِبُوهُ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Translations:
---
Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi, na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya Shet'ani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.
-- Ali Muhsin Al-Barwani

---
 
Back
Top Bottom